Sakata la Dangote kaa la moto

Sakata la Dangote kaa la moto

comrade igwe

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2015
Posts
7,295
Reaction score
3,951

SIKU moja baada ya Kiwanda cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara kuripotiwa kwamba kimesitisha uzalishaji, watu mbalimbali wakiwamo, wanasiasa, wachumi na wachambuzi wameibuka na kuishangaa Serikali namna inavyoshughulikia suala hilo.

Akizungumza na MTANZANIA kwa simu jana, Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT -Wazalendo) alisema suala la Dangote halikupaswa kufikia hatua hiyo kwani linatoa picha mbaya kwa wawekezaji waliopo na wanaotarajiwa kuja nchini.

Alisema kama Serikali inataka kuendelea na ajenda yake ya maendeleo ya viwanda ni lazima iboreshe namna yake ya ushirikiana na wawekezaji.

“Ukitazama kwa umakini utaona Dangote anakomeshwa kwa sababu ya hisia kuwa kuna wanasiasa wa awamu ya nne wanaubia naye, mawazo ya husda na chuki ndiyo yanayoongoza uamuzi wa baadhi ya watu serikalini, haifai kabisa, yanayotokea ni sawa na mtu ambaye wakati wa baridi anachoma moto nyumba yake ili aote moto.

“Serikali iache utoto, ishughulike na suala hili ili uzalishaji uendelee, lakini pia isikilize kilio cha wenye viwanda kuhusu gharama za uzalishaji kwa sababu ni kubwa mno, ruzuku kwa wazalishaji ni muhimu ili kuzalisha ajira isibishane kwa sababu ya ubishi, ” alisema Zitto.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Dk. Dalali Kafumu, amesema anashangazwa na hali tete inayojengeka kati ya Serikali na kiwanda hicho.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Dk. Kafumu alisema mvutano huo unaweza kuathiri taswira ya uwekezaji nchini na kuiomba Serikali ikae na mwekezaji huyo ili kumaliza tofauti zao.

Dk. Kafumu ambaye ni Mbunge wa Igunga (CCM) alikuwa akitoa maoni yake binafsi, ambapo ameonekana kuguswa na sakata hilo na kusema kuwa haoni busara za Serikali katika kumaliza mzozo huo zaidi ya ubabe.

Alisema kamati yake haijui chochote kuhusiana na mzozo huo na kueleza kuwa amezungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, akutane na kamati yake ili wabunge watoe ushauri wao kunusuru kiwanda hicho.

“Kwa maoni yangu binafsi, kwa namna tunavyoona kwenye vyombo vya habari, hapa kunatatizo, Dangote ni mwekezaji mkubwa suala hili linahitaji utulivu katika kulishughulikia.

“Inavyoonekana wakati mwekezaji huyu anakuja, kulikuwa na makubaliano na Serikali iliyopita labda masuala ya misamaha, masuala ya kodi, bei nafuu ya gesi na mengine.

“Sasa leo kumwambia tu usitumie makaa ya nje lazima utumie ya ndani, sawa inawezekana lakini mnajuaje kama huyu mtu ana mikataba na huko anakotoa hayo makaa?

“Dangote ni mwekezaji mkubwa, ana viwanda vingine huko duniani akifunga kiwanda chake hasara itakuwa ya kwetu. Serikali hii imejielekeza kwenye uchumi wa viwanda, leo unaposikia msuguano kama huu unapata shida kuelewa inakuwaje?,” alihoji.

Kafumu aliendelea kusema. “Mawaziri wanasema Serikali haipaswi kulaumiwa isipokuwa Dangote mwenyewe, wanasema alipewa kibali cha kuvuta gesi hakuvuta, tujiulize kwanini hakuvuta?

“Mara hakusaini mkataba wa kununua makaa ya mawe, ujiulize kwa nini hakusaini? Serikali ikae na Dangote wazungumze, kwa namna hii ni kama Serikali inafunga urafiki na mwekezaji huyu, jambo ambalo si zuri,” alisema Dk Kafumu.

Waziri Kivuli

Naye Waziri Kivuli wa Viwanda na Biashara, Anthony Komu alisema anasikitishwa na mwenendo wa sakata la Dangote, kwani linapaswa kushughulikiwa haraka ili kulinda maslahi mapana ya Taifa.

“Tuna tatizo kubwa juu ya ukweli wa jambo hili kutoka serikalini, kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa, Serikali imekuwa ‘difensive’ mno, nadhani kwa hali hii hatuwezi kwenda kabisa. Siku zote tunaambiwa mambo yanakwenda vizuri sasa iweje tushuhudie hali hii.

“Kwanza Watanzania wengi watapoteza ajira, unafuu wa upatikanaji wa saruji utapotea kama zamani, ulipaji kodi utashuka, bei ya saruji itapanda mara dufu… haya yote ni mambo ya msingi ambayo yanapaswa kuangaliwa kwa kina,”alisema Komu.

Profesa Semboja

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM) Profesa Hajji Semboja alisema katika kipindi hiki ambacho serikali iko kwenye mchakato wa kuanzisha viwanda, wanapaswa kushirikiana na wawekezaji wanaokuja nchini akiwamo Dangote na kuangalia matatizo yanayojitokeza na kuyafanyia kazi.

“Kiwanda hicho ni kikubwa ambacho kimezalisha ajira na saruji ambayo inauzwa kwa gharama nafuu hata mwananchi wa kawaida anaweza, hivyo serikali wanapaswa kukaa pamoja na kuangalia tofauti zilizopo na kuzifanyia kazi.

TPDC

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba alisema taarifa zilizotolewa na uongozi wa Dangote juzi hazina ukweli wowote.

“Kama TPDC tunapenda kukanusha taarifa zinazoenezwa na Kampuni ya Dangote pamoja na washirika wake kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kudai kuwa tumeshindwa kukiuzia gesi asilia kwa bei rahisi na kwamba ndiyo moja ya sababu ya kusimamisha uzalishaji wake,” alisema.

Alisema TPDC hufuata kanuni na utaratibu wa kupanga bei ya gesi asilia kulingana na aina ya mteja na kwamba wateja wamegawanyika makundi tofauti kama vile wateja wa viwandani, majumbani, magari, pamoja na wazalishaji umeme.

Alisema bei elekezi ambayo inapendekezwa na TPDC ni lazima iridhiwe na ipitishwe na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ndipo ianze kutumika na si mtu binafsi kujipangia bei yake.

Alisema TPDC hufuata kanuni na utaratibu wa kupanga bei ya gesi asilia kulingana na aina ya mteja na kwamba wateja wamegawanyika kufuatia makundi tofauti kama vile wateja wa viwandani , majumbani, magari, pamoja na wauzalishaji umeme.

“Dangote kama mtumiaji wa viwandani amekuwa na mazungumzo ya muda mrefu na TPDC kuhusu bei ya gesi asilia , ambapo kiwanda chake kimeomba kupewa gesi kwa bei ambayo hapa kwetu ni kidogo, kiasi hicho cha bei ndicho kinacholipwa kwenye kununulia gesi ghafi kutoka kisimani.

Akifafanua zaidi, Kaimu Mkurugenzi huyo wa TPDC alisema Dangote alikuwa anataka auziwe gesi hiyo kwa Dola za Marekani 4.7.5 na baadaye akakataa akitaka ishuke zaidi ingawa bei iliyopo kwa sasa ni Dola za Marekani 5.1.4 kwa kipimo cha energy jambo ambalo alisema halitawezekana.

“Dangonte amekuwa akibadilika badilika ambapo alianza na Dola milioni 2 akaja 4 na hii ya mwisho alitaka iwe hiyo ya Dola za Marekani 4.7.5 na bei hizi zinaitwa Dola chini ya kipimo ambapo kitaalamu inajulikana kama MMBTU.

Kuhusiana na utumiaji wa makaa ya mawe ambayo yanazalishwa hapa nchini, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi John Shija alisema mkakati wa serikali ni kuhakikisha viwanda vyote vinavyozalisha saruiji nchini vitumie makaa ya mawe yanayozalishwa na Mgodi wa Ngaka uliopo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.

Lengo la serikali kufanya hivyo ni kulinda mgodi huo ambao unatija kwa Watanzania wote na tayari baadhi ya viwanda vinavyozalisha saruji hapa nchini vimeshaingia mkataba na mgodi huo isipokuwa Dangote.

“Lakini mpaka sasa upande wa kiwanda cha Dangote wako kimya hawajasema chochote kuhusiana na hili, hivyo tutaangalia ni hatua gani zaidi za kuchukua iwapo tutakosa ufumbuzi wa baadhi ya viwanda kutotumia makaa ya mawe yanayozalishwa hapa nchini,” alisema.

Kuhusu ubora wa makaa hayo, alisema kila kiwanda kina aina yake ya matumizi na kusema kuwa mgodi wa Ngaka una maabara ambayo inatumika kupima makaa hayo kwa ubora unaostahili kinyume na inavyoelezwa kuwa hayafai.

Utajiri wa Dangote

Kinara huyo wa utajiri barani Afrika mwenye umri wa miaka 58 anashika nafasi ya 51 duniani akiwa na Dola za Marekani bilioni 15.4 nyuma ya James Simons mwenye utajiri 15.5 bilioni.

Dangote amejipatia ukwasi huo kupitia uwekezaji katika uzalishaji wa saruji, sukari na maua ambapo uwekezaji wake wa hivi karibuni aliufanya katika nchi za Cameroon, Ethiopia, Zambia, nyumbani kwao Nigeria and na hapa Tanzania.

Pia amewekeza katika nchi za Benin, Senegal, Ghana, Afrika Kusini na Togo, huku kampuni yake ikizalisha mara 30 zaidi ya kipimo cha tani za metriki kwa mwaka na akitegemea kuzalisha mara mbili ya hapo ifikapo 2018.

Chanzo: Mtanzania
 
Nauliza tu uwezo anao au ni mkwara tu ili ashinikize matakwa yake ? Na kama anao huo uwezo ni nani atalipa gharama ya uwekezaji wote? Ikumbukwe hiki ni moja kati ya Viwanda vyake vikubwa, sasa Je ana uwezo kupoteza hiyo hela au ndiyo tujiandae kwa Mapinduzi ya Serikali yetu kupindiliwa?
 
Hapa kuna shida.....tena shida kubwa tu, Serikali ichukue hatua stahiki, kama kweli hizi figisu zinachangiwa pia eti kwa vile kuna watu wa awamu ya 4 wana mikono hapo ndani, basi kweli ni utoto kama asemavyo Zitto.
 
Kiwanda ni cha nani? Kwann asifunge kama hakimlipi?

Kwahiyo mnaacha kutumia akili na formula za kiuchumi mnajipa moyo hawezi kufunga kiwanda.

Nyie jamaa mna shida sana kwenye suala la kufikiri asee
 
Tuliposema tna hitaji viwanda hatukukusudia viwanda huvyo bali viwanda vya kuchakata fedha
 
Acha tukomoane kwanza!! Hilo ndilo la muhimu kwanza,viwanda siyo issue kubwa kwetu! Subirini tumkomoe mtu kwanza!!
 
Mkuu ni kama ulikuwa kwenye kichwa change......nilitaka kuhoji hivi hivi....... Hawa watu sijui wana akili gani, kweli inawezekana wanawaza eti kwa vile uwekezaji ni Mkubwa basi hawezi kufunga kiwanda hivyo tumkomoe.......ajili za ajabu kabisa.
 
Napata tabu sana kuelewa mantiki ya mtoa mada asee.

Eti nani analipa gharama za uwekezaji mkubwa! Kwahiyo kipi afadhali apate hasara ya uwekezaji mkubwa peke yake au apate hasara ya uwekezaji mkubwa na hasara za ku run kiwanda kwa hasara!!
 
Hapa kuna shida.....tena shida kubwa tu, Serikali ichukue hatua stahiki, kama kweli hizi figisu zinachangiwa pia eti kwa vile kuna watu wa awamu ya 4 wana mikono hapo ndani, basi kweli ni utoto kama asemavyo Zitto.
Zitto na amtaje huyo/hao wa awamu ya nne wanaohisiwa vinginevyo yeye ZZK ndio analeta utoto na yale mambo ya ff
 
Kiwanda si cha kwake.. Sasa atashindwaje kukifunga??
Au mara hii mmeshakigeuza kuwa ni kiwanda cha serikali katika vile mlivoviahidi mtavijenga??

Mana hamshindwi nyie vijana wa Lumumba.

Nasikia kile cha Chamazi cha Bakhresa mnasema chenu.
 
Napata tabu sana kuelewa mantiki ya mtoa mada asee.

Eti nani analipa gharama za uwekezaji mkubwa! Kwahiyo kipi afadhali apate hasara ya uwekezaji mkubwa peke yake au apate hasara ya uwekezaji mkubwa na hasara za ku run kiwanda kwa hasara!!
Inabidi tuwaze kama watu wa aina hiyo ndio wamejaa wanamshauri mheshimiwa Rais basi kuna Giza Nene sana mbele ya safari.
 
Nauliza tu uwezo anao au ni mkwara tu ili ashinikize matakwa yake ? Na kama anao huo uwezo ni nani atalipa gharama ya uwekezaji wote? Ikumbukwe hiki ni moja kati ya Viwanda vyake vikubwa, sasa Je ana uwezo kupoteza hiyo hela au ndiyo tujiandae kwa Mapinduzi ya Serikali yetu kupindiliwa?

Mali yako utashindwaje kuifunga na kuihamishia nchi yoyote hata Msumbiji.Wawekezaji wenye pesa kama Dangote wanaliliwa Duniani kote.
 
Nauliza tu uwezo anao au ni mkwara tu ili ashinikize matakwa yake ? Na kama anao huo uwezo ni nani atalipa gharama ya uwekezaji wote? Ikumbukwe hiki ni moja kati ya Viwanda vyake vikubwa, sasa Je ana uwezo kupoteza hiyo hela au ndiyo tujiandae kwa Mapinduzi ya Serikali yetu kupindiliwa?
Enzi za vitisho kulee! ! Mlipoambiwa mnaacha reli mlidhani siasa, sasa mkabili na matokeo ya kujaribu uchumi wa kizamani
 
Nauliza tu uwezo anao au ni mkwara tu ili ashinikize matakwa yake ? Na kama anao huo uwezo ni nani atalipa gharama ya uwekezaji wote? Ikumbukwe hiki ni moja kati ya Viwanda vyake vikubwa, sasa Je ana uwezo kupoteza hiyo hela au ndiyo tujiandae kwa Mapinduzi ya Serikali yetu kupindiliwa?
yule ni mfanyabiashara mkubwa sana hvyo kabla ya kuanizsha biashara anauwa ameshapiga mahesabu pamoja na kuweka uwezeano wa mambo km hayo kutokea kwahio yanapotokea mambo kama hayo solution cku zote huwepo...hawez wekeza mamilion ya dollar kichwakichwa tu hivihivi lazima atakuwa na plan b ikiwa mambo yatakuwa hayaeleweki
 
Akili za kipuuzi kwelikweli, kwani yeye si ndiyo alikijenga, iweje ashindwe kukifunga kama hakimlipi.

Kwa hiyo mna muwekea vikwazo mkidhani hatoweza kukifunga??

Wahed!
 
Akifafanua zaidi, Kaimu Mkurugenzi huyo wa TPDC alisema Dangote alikuwa anataka auziwe gesi hiyo kwa Dola za Marekani 4.7.5 na baadaye akakataa akitaka ishuke zaidi ingawa bei iliyopo kwa sasa ni Dola za Marekani 5.1.4 kwa kipimo cha energy jambo ambalo alisema halitawezekana.

“Dangonte amekuwa akibadilika badilika ambapo alianza na Dola milioni 2 akaja 4 na hii ya mwisho alitaka iwe hiyo ya Dola za Marekani 4.7.5 na bei hizi zinaitwa Dola chini ya kipimo ambapo kitaalamu inajulikana kama MMBTU.

Haya wale wa mahesabu tiririkeni.

5.1.4
-4.7.5
3 .9 tofauti hiyo.

Dr.Kafumu nadhani amehoji maswali ya msing yanayohitaji majibu ilikupata undani wa tatizo.
Je kwa wenzetu bei ikoje?
 
Busara inatakiwa itumike maana Tajiri bilionea tena wa kimataifa kama Dangote akifunga biashara zake ina maana wawekezaji karibu wote duniani watatishika sana na hali ya uwekezaji nchini.Tena wakikumbuka na utaifishwaji uliotokea baada ya Azimio la Arusha,taswira ya Tanzania inaweza kuchafuka vibaya sana kimataifa.
 
Nauliza tu uwezo anao au ni mkwara tu ili ashinikize matakwa yake ? Na kama anao huo uwezo ni nani atalipa gharama ya uwekezaji wote? Ikumbukwe hiki ni moja kati ya Viwanda vyake vikubwa, sasa Je ana uwezo kupoteza hiyo hela au ndiyo tujiandae kwa Mapinduzi ya Serikali yetu kupindiliwa?
Mmmh kupinduliwa?? How?
Kuna uhusiano gani kati ya kiwanda cha dangote na taasisi ya uraisi tanzania?
 
Back
Top Bottom