issenye
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 3,781
- 5,205
Umenikumbusha stori moja ya rubani aliyekuwa katekwa na majeshi ya Garang enzi hizo. Siku BBC wakimsifia Garang basi mateka siku hiyo watapewa kikombe kidogo cha mchele wapike wale na glass ya whysky wanywe. lakini siku wakimkosoa itakuwa ni siku ya kichapo kwa kwenda mbele. Ndivyo inavyokuwa kwa serikali ya awamu ya tano na ya milele, hawataki kukosolewa.BBC wamekua wepesi sana kurusha matamko dhidi ya Tanzania yatolewayo na shirika la afya duniani kupitia wakurugenzi wake kuhusiana na ugonjwa wa covid 19 hasa yale yenye kuonyesha mbinyo kwa nchi yetu.
Jana pia dira ya mchana lilitolewa tamko na mkurugenzi mkuu kanda ya Afrika lenye kuitaka Tanzania ijitafakari kuhusu chanjo na iwe tayari kushirikiana na nchi za kiafrika, kwangu mimi hili ni debe la biashara tu.
Jana hiyohiyo KM wa afya, professor Mchembe aliipangua kauli ya MD huyo kanda ya Afrika. Ufafanuzi wa Mchembe ulikuwa makini na wenye kufikirisha sana kwa anae jitambua.
Professor Mchembe alisema Tanzania haiko tayari kwa chanzo hizo, kwani nchi nyingi zimetengeneza chanjo ya virus hivi, China, Amerika, Russia, German, Brazil, India nk, Je? Tutumie chanjo ipi ambayo ni salama ikizingatiwa virus hawa wanajibadilisha kila uchao.
Kwakuwa professor Mchembe maelezo yake yalimfunika MD wa WHO kanda ya Afrika, BBC wakaipotezea habari hii yenye kufumbua macho waafrika.
Kwangu mimi hii ni kauli thabiti sana,
Na ndipo suala la uharaka wa chanjo hizi zilizogunduliwa kwa kukiuka kanuni utajua zimelenga biashara, yaani tatizo limetengenzwa ili kujipatia faida kubwa huku baadhi ya wanadamu wakiangamia pasi hatia yoyote.
Naipongeza serikali kwa kua makini sana katika kucheza ngoma hii ya ma babylon.
Namalizia kwa kusema BBC na DW ni radio za wakoloni zenye kazi moja tu ya propaganda mfu dhidi ya anayepinga udhalimu wa mabeberu, chukua tahadhari