Sakata la Corona: BBC acheni unafiki, heko (KM) Wizara ya Afya, Prof. Mchembe kwa nyundo yako jana

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
7,117
2,000
BBC wamekua wepesi sana kurusha matamko dhidi ya Tanzania yatolewayo na shirika la afya duniani kupitia wakurugenzi wake kuhusiana na ugonjwa wa covid 19 hasa yale yenye kuonyesha mbinyo kwa nchi yetu.

Jana pia dira ya mchana lilitolewa tamko na mkurugenzi mkuu kanda ya Afrika lenye kuitaka Tanzania ijitafakari kuhusu chanjo na iwe tayari kushirikiana na WHO na nchi za kiafrika, kudhibiti covid 19, kwangu mimi hili ni debe la biashara tu.

Jana hiyohiyo KM wa afya, professor Mchembe aliipangua kauli ya MD huyo kanda ya Afrika. Ufafanuzi wa Mchembe ulikuwa makini na wenye kufikirisha sana kwa anae jitambua.

Professor Mchembe alisema Tanzania haiko tayari kwa chanzo hizo, kwani nchi nyingi zimetengeneza chanjo ya virus hivi, China, Amerika, Russia, German, Brazil, India nk, Je, tutumie chanjo ipi ambayo ni salama ikizingatiwa virus hawa wanajibadilisha kila uchao.?

Kwakuwa professor Mchembe maelezo yake yalimfunika MD wa WHO kanda ya Afrika, BBC wakaipotezea habari hii yenye kufumbua macho waafrika.

Kwangu mimi hii ni kauli thabiti sana.

Na ndipo suala la uharaka wa chanjo hizi zilizogunduliwa kwa kukiuka kanuni utajua zimelenga biashara, yaani tatizo limetengenzwa ili kujipatia faida kubwa huku baadhi ya wanadamu wakiangamia pasi hatia yoyote.

Naipongeza serikali kwa kua makini sana katika kucheza ngoma hii ya ma babylons.

Namalizia kwa kusema BBC na DW ni radio za wakoloni zenye kazi moja tu ya propaganda mfu dhidi ya anayepinga udhalimu wa mabeberu, chukua tahadhari.
 

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
4,883
2,000
Mkuu issue ni kupambana na Korona Mzee, watu wanakufa au Tanzania hatufi? Issue ya kujifukiza still ni controversial, imekuwa successful Kwa vijana lakini wazee wanashuka kaburini mkuu, boss wetu yeye kaukimbia mji yupo porini na inasemekana kama Una Korona huwezi kumsogelea m100 away. Na za chini chini keshalamba chanjo, anachohofia ni cost ya chanjo na si vinginevyo.
 

HOPECOMFORT

JF-Expert Member
Feb 25, 2012
3,187
2,000
Kama chombo cha habari kazi yake ni ku report sioni kosa lao. Kama wamefikisha ujumbe kama walivyopokea.

Kama korona ni janga la dunia na Tanzania ni moja ya hizo nchi za duniani kwani kupokea ushauri kuna tatizo gani.. Kama nyie hamtaki basi sawa..tambulisheni chanjo yenu na dunia ijue. Tuwasaidie na wengine pia.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
41,182
2,000
Mkuu issue ni kupambana na Korona Mzee , watu wanakufa , au Tanzania hatufi? Issue ya kujifukiza still ni controversial , imekuwa successful Kwa vijana lakn wazee wanashuka kaburini mkuu, boss wetu yeye kaukimbia mji yupo porini na inasemekana kama Una Korona huwez kumsogelea m100 away .... Na za chini chini keshalamba chanjo , anachohofia ni cost ya chanjo na si vinginevyo
Well said mkuu watu wanaumia sana.
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
5,920
2,000
Wachina wanasema " haijalishi rangi ya paka, kilicho muhimu ni kuwa anakamata panya". Kila nchi itafanya uamuzi wa chanjo ya aina gani ya kutumia kutokana na uwezo wake wa kifedha, uwezo wake wa kuisambaza kwa wananchi wake na hali yake ya miundombinu.

Haitakuwa na maana kuagiza chanjo zinazohitaji kuhifadhiwa katika ubaridi wa minus 70 degrees kwa hospitali zetu za vijijini ambazo jokofu tu ni changamoto, hata kama hizi ni bora sana.

Busara zitatuelekeza kuagiza zile zenye bei nafuu, ambazo zinadumu muda mrefu bila ku expire na hazihitaji mazingira maalum ya uhifadhi. Huo ni uamuzi wa serikali yetu na sio WHO. Aidha, tusizikataze zile taasisi zenye uwezo wa kuhifadhi dawa za Pfizer BioNTech kwa ajili ya wateja wao wenye uwezo wa kuzilipia.

Amandla....
 

Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
12,983
2,000
Hakuna jazba katika hili, Data zitasema tu. Uk wameshasema wamechoma watu Million 11 chanjo ya kwanza na number za wagonjwa kulazwa zinashuka kila leo sasa haya ndio tunataka ushahidi wa Data sio nadharia. ukweli utakuwa wazi tu ni muda tu.
Namba hazidanganyi. hapa ndipo ambapo wanaficha data maana wataonekana hawakudanya kitu.
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
15,083
2,000
Dikteta amesababisha wasomi waonekane ni watu wa hovyo sn kila mtu ana pambana kumfurahisha
Laiti kama huyo kibwengo 👿 asingekuwa kwenye hiyo ofisi kuu, yaani angekuwa anatoa maoni au matamko yake kama raia au mwanasiasa wa kawaida.

Kila mtu angeomba huyo mtu apelekwe Mirembe.

Ila nguvu ya ofisi anayoikalia IMEVURUGA kila kitu.

Hata kesho akisema watu waanze kula mavi ya popo, surely kuna watu wataanza kula Live mbele ya TV ili wamfurahishe.
 

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
4,141
2,000
Tupo wangapi, wameambukizwa wangapi na wamekufa wangapi ukiweza kujibu haya unaongea kama msomi vinginevyo ni kama yule prof wa chemistry tu.

Yy kila kitu anaona wanaojua wanamfitini kwa kipi haswa?
 

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
7,117
2,000
Kama chombo cha habari kazi yake ni ku report sioni kosa lao...kama wamefikisha ujumbe kama walivyo pokea.

Kama korona ni janga la dunia na Tanzania ni moja ya hizo nchi za duniani kwani kupokea ushauri kuna tatizo gani.. Kama nyie hamtaki basi sawa..tambulisheni chanjo yenu na dunia ijue ...tuwasaidie na wengine pia.
Chanjo ni biashara za watu jomba ,hukuona Madagascar walivyopingwa kwa haraka sana na MD wa WHO siku moja tu wakivyotangaza kuwa na dawa hiyo bila ya MD huyo kuifanyia uchunguzi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom