Mambo mengine hayahitaji kushangilia, na hasa kama huna taarifa za ndani na za uhakika.
Kwanza ni ukweli kuwa hakuna mfanyabiashara au mwekezaji anayeweza kuamua kugombana na Rais au serikali, kama una nia ya kuendelea kuwekeza au kufanya biashara. Wafanyabiashara/wawekezaji wana ethics zao, na wengi wao ni watu werevu, wenye akili kubwa, mara nyingi kuwazidi hata watawala. Hawakiuki maadili yao kiurahisi.
Kwa kawaida wafanyabiashara/wawekezaji huwa wana namna yao ya kugombana/kuipinga serikali au mtawala. Huwa au wanafunga biashara au wanaacha kuwekeza, huwa hawaendi kwenye press kueleza kuwa wanampinga mtawala au serikali. Kusimamisha biashara au kuacha kuwekeza huwa ni upingaji wenye nguvu na athari kubwa kwa serikali kuliko upingaji wa maneno ambao mara nyingi hufanywa na wanasiasa, vyama vya siasa na wanaharakati.