Sakata la Coco Beach: Manji asitisha mpango wa kuchukua ufukwe wa Coco Beach kwa lengo la kuwekeza

pamoja ya kuwa sometimes magu anazidisha ubabe lakini namuunga mkono wahindi hawa ni corrupt na wanyanyasaji sana....alipe na kodi zote alizokwepa shenzy taip
Hiyo ID yako tu unaonekana ni mtu wa wapi
 
Sawa. Ila Manji ananyanyasika sana ktk utawala huu. Sijui chanzo ni zile mil. 725 zilizokamatwa Chimwaga ??
Anajinyanyasa mwenyewe kwa kufikiri yupo juu ya sheria kutokana na fedha zake. Siyo kweli kwamba fedha zinaweza kuwa jawabu kwa kila kitu.
Kila awamu ina style yake ya kutawala. Inaonekana kwenye awamu hii mwenye fedha siyo kila kitu bali hata mnyonge ana haki. Manji ni maarufu lakini dola ndiyo kila kitu. Awe mpole tu.
 
Naona waswahili wenzangu mnanyooshana kweli kweli kwenye mitusi.

Hiviiii........... huyu si ni mmoja kati ya wale watatu waliomwambia mkuu wa kaya kipindi kile akiwa waziri wa Miundo mbinu kuwa "Hatuongei na mbwa, tunaongea na mwenye mbwa"
 
Mambo mengine hayahitaji kushangilia, na hasa kama huna taarifa za ndani na za uhakika.

Kwanza ni ukweli kuwa hakuna mfanyabiashara au mwekezaji anayeweza kuamua kugombana na Rais au serikali, kama una nia ya kuendelea kuwekeza au kufanya biashara. Wafanyabiashara/wawekezaji wana ethics zao, na wengi wao ni watu werevu, wenye akili kubwa, mara nyingi kuwazidi hata watawala. Hawakiuki maadili yao kiurahisi.

Kwa kawaida wafanyabiashara/wawekezaji huwa wana namna yao ya kugombana/kuipinga serikali au mtawala. Huwa au wanafunga biashara au wanaacha kuwekeza, huwa hawaendi kwenye press kueleza kuwa wanampinga mtawala au serikali. Kusimamisha biashara au kuacha kuwekeza huwa ni upingaji wenye nguvu na athari kubwa kwa serikali kuliko upingaji wa maneno ambao mara nyingi hufanywa na wanasiasa, vyama vya siasa na wanaharakati.
 
Manji tulikuonya humu mapema sana ila jeuri na dharau zako ndizo zilikuponza hadi sasa umesubiri ' umeshabinywa ' na ' kukamuliwa ' vya kutosha huku Vyanzo vyako vyote vya Pesa vikipigwa ' pini ' ndipo unasalimu amri. au ulidhani JPM ni yule ' Mkwere ' wako ambaye ulikuwa unampelekesha unavyotaka?

Ukome!

Jamaa huyu jeuri kupindukia - we mtu hata kama una jeuri ya pesa unaweza kweli kutaka kushindana na Dola, kutaka kujibizana jibizana na Rais wa nchi!!! Lakini looking back now kwa watu wanao juwa background ya Quality Garage wala atuwezi kushangazwa na tabia yake - walisha tuona Waswahili ni watu wa kuwa manipulated easily - chukulia mifano ya mifuko yetu ya hifadhi ya jamii ilivyo chezewa, je, zamani National Insurance Corporation nalo ni Shirika la UMMA nini kilikuwa kinaendelea huko!!!

Tushukuru Mungu kwa kutuletea mtu mwenye uchungu wa kweli kuhusu Taifa letu - huyu ndiye mwarobaina wa kurudisha nidhamu kwenye ofisi za Serikali na Mashirika yetu ya UMMA, mambo ya kuishi kimchoro mchoro kutegemea Mashirika ya UMMA JPJM amekwisha yawekea PIN.
 
SAKATA LA UFUKWE WA COCO:

Mfanyabiashara Yusuph Manji asitisha mpango wake wa kulichukua eneo la Ufukwe wa COCO ili kuliendeleza, amwomba radhi Rais Magufuli.

93a4454ad7b7930c9e39f1dfd944285f.jpg
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom