Sakata la bomoabomoa Dar lachukua sura mpya

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
4,150
2,000
Baada ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kutoa notisi ya siku 30 ya kubomoa nyumba, kuta, uzio au fremu za biashara katika hifadhi ya Barabara ya Morogoro, wakazi wa maeneo hayo wamesema hawakubaliani na hatua hiyo kwa kuwa hawajalipwa fidia.

Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na kuthibitishwa na Kaimu Meneja wa Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam, Eliamin Tenga, wanatarajia kuanza kuboresha eneo hilo hivi karibuni ili kuondoa changamoto ya foleni.

Katika barua hiyo ya juzi iliyoelekezwa kwa Ofisa Mtendaji Kata ya Kimara, Tanroads inasema uboreshaji huo unafanyika kwa lengo la kuondoa msongamano wa magari unaoanzia Kimara Korogwe hadi Ubungo.

“Tunapenda kukutaarifu kuwa Serikali kupitia Tanroads Dar es Salaam, imetenga fedha kwa ajili ya kutatua changamoto za msongamano wa magari Kimara Bucha hadi Kimara Resort,” inaeleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa barua hiyo, hifadhi ya Barabara ya Morogoro ina upana wa mita 90 kutoka katikati ya barabara kila upande kuanzia Ubungo hadi Kimara Stop Over.

Tenga alieleza katika barua hiyo kuwa, tangu mwaka 1997, 2014 na 2017, ofisi ya meneja wa Tanroads ilitoa notisi za kuondoa majengo, kuta na vibanda vya biashara katika eneo hilo la hifadhi ya barabara.

bomoa pc

Akizungumza na Mwananchi baada ya kikao chao na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimara Baruti, mkazi wa eneo hilo, Jesse John alisema wamekubaliana kuandika barua ofisi ya Tanroads kutaka wakutane nao wajadili suala hilo kwa pamoja.

“Katika barua hii ambayo Mwenyekiti ndiyo ameiandika, imeonyesha ambavyo hana taarifa kuhusu sisi kuondolewa, jambo la pili imeeleza kuwa utaratibu haujafuatwa na pia ameomba kikao kati ya wananchi na Tanroads,” alisema John.

Mwananchi ilizungumza pia na mkazi wa Kimara Bucha, Hemed Ramadhan ambaye alisema nyumba yao inayotakiwa kubomolewa ilijengwa na baba yake tangu mwaka 1972, hivyo barabara imeikuta nyumba hiyo.

Alidai kuwa Tanroads wanataka kutumia nguvu kuvunja nyumba za watu bila kufuata sheria ya kuwalipa fidia yoyote.

“Waliolipwa fidia ilikuwa mita 30 wakati huo wa Rais wa awamu ya tatu, akaja Rais wa awamu ya nne walilipwa, lakini awamu hii hatujalipwa chochote,” alidai Ramadhan.

Hata hivyo, alisema hakuna uwiano kwa watu wanaovunjiwa kwa sababu Tanroads wameweka alama ya X kuanzia nyumba zilizopo Kimara Bucha hadi Kimara Resort, huku maeneo mengine wakiyaacha.

“Hakuna uwiano kabisa, hii kiukweli inatutia shaka, kuna nyumba nyingine wameishia mita 40, nyingine mita 90 na nyingine zimeachwa kabisa. Kikubwa sisi hatuzuii wasifanye wanachokitaka ila tunataka tufidiwe,” alisema Ramadhani.

Aliongeza kwa kuwa kesi hiyo ilishafika mahakamani na hukumu ipo ikiwaonyesha wameshinda, kama jambo hilo limeshindikana watarejea tena mahakamani.

Mkazi mwingine, Avelina Marwa alisema amehamia Kimara tangu mwaka 1985 na hujui anakwenda wapi, hivyo Tanroads inatakiwa ifuate sheria na taratibu zinazotakiwa.

“Kwanza hata hiyo jana (juzi) walivyokuja kuleta barua walifika hawajui mwenye nyumba wala mpangaji wanampa mtu yeyote tu, tumeshtukia barua ziko kwenye fremu zetu tu, yaani kiukweli tunaona kama kuna usanii unafanyika,” alisema Avelina.

Godwin Mneng’ene alisema nyumba yake imejengwa tangu mwaka 1980, hivyo anataka alipwe fidia na muda uliotolewa kuvunja nyumba zao hautoshi.

“Angalau wangetupatia japo miezi sita na kuendelea kama wenzetu waliowahi kubomolewa, sio sisi wanatupa muda mfupi tena bila hata fidia, hatukubaliani na jambo hili,” alisema Mneng’ene.

Mwenyekiti anena

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Baruti, Mohamed Kilongo alisema ameshangazwa na jambo hilo, kwa sababu Tanroads hawakumpelekea taarifa rasmi, yeye amezipata kwa wananchi wake.

Alisema wameshaandika barua kwenda Tanroads na amewaagiza wananchi wake kuunda kamati itakayokwenda kusimamia hatima yao.

“Nilipiga simu kutoka kwa watu hawa ambao nyumba zao zimewekwa X, ikanibidi nimpigie mtendaji wangu akasema amepokea barua na anaendelea kufuatilia. Sisi tumeandika barua tunataka kuonana na Mtendaji Mkuu wa Tanroads tujue hatima ya wananchi hawa,” alisema Kilongo.

Alipotafutwa meneja huyo wa Tanroads, alisema tayari amekwenda kuzungumza na wananchi katika maeneo hayo.

Mwananchi
 
Jameel2013

JF-Expert Member
Aug 21, 2014
753
1,000
Hivi serikali inakosa hela hata kidogo tu ya kuwafidia hawa walengwa hata wawafafidie kiwango kimoja tu cha hela hata MILLION 25 kwa kila muathirika wakatafute viwanja huko ile maisha ya endelea.
 
Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
7,138

Hivi haya maeneo yanapokuwa yanavamiwa, wahusika waliokuwa wanatakiwa kuhakikisha kuwa hayavamiwi walikuwa wako wapi? Kabisa mimi huwa sioni logic ya kuwabomolea watu wakati wenye makosa siyo wao. Mathalani, huwezi ukalala umeacha mlango wazi nyumbani kwako kisa tu unajua kuna sheria inayoweza kum-convict mtu anayeweaa kuja kuiba nyumbani kwako wakati ukiwa umeacha mlango wazi. Kwa hili wanahusika pia wale walioacha maeneo hayo yakavamiwa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom