Sakata la Bandari na DP World, kipi hasa kinapingwa?

Sakata la Bandari na DP World, kipi hasa kinapingwa?

Shida ya watanzania kushindwa kuendesha ni nini ? (Kwanini tusitafute hio shida ili tuanze kuitibu kuliko kuwarisisha vituu mikataba ya kuendelea kuwa manamba sababu ya uzembe wetu sisi)

Mambo kama Bandari sio manual labor tena kuna automation ya kutosha; hivyo basi kama shida ni automation kwanini tusinunue na kuwekeza (kama shida ni technical know how; kwanini experts wasije na kutufundisha) kama shida ni utamaduni wa wizi (kwanini sheria zisichukue mkondo wake) ?

Mimi shida katika haya mambo sio Bandari Per-se bali ni mentality mbovu ya kudhani kwamba hakuna unachoweza na utamleta mtu akufanyie kila kitu kila mahali na bado ubaki na percentage kubwa - Badala ya kuwaza kufanyiwa, tungewaza kampuni zetu ziende kufanyia watu wengine huko kwao....

Ila ndio hivyo Mentality yetu inapiga hatua kuelekea nyuma siku baada ya siku....

Binafsi mimi hao jamaa ningewapa huko Tanga au Kigoma wakajinafasi na hapo Dar hata hayo Magati tofauti ningewapa wawekezaji tofauti kwa lease fupi fupi za kama miaka mitano mitano na kila anayechemsha anapigwa chini na mwingine anaomba (after all kama tumeshindwa kuwasimamia hawa Wamatumbi pindi wanapoiba unadhani unaweza ukaisimamia a Multi Corporation ili isiibe ?) Au watakwambia sababu tumepata Hasara au Covid 3.0 imekuja hivyo itabidi badala ya sisi kukulipa mtulipe hasara ya tuliyowekeza ? (After all kama kuna 10% unadhani watu wetu watakataa)

Au wakitumia Hii Bandari kama Collateral ya kwenda kuombea mikopo ili kuchukua Bandari nyingine kadhaa (nani wa kuwabishia ? Na siku wakienda Pear Shaped ndio hivyo vitu kupigwa mnada)
Nakubaliana na wewe kabisa. Hii mentality ya hatuwezi ndiyo imekuwa tatizo.

Serikali kama serikali wenyewe huwezi kutaka wa akili wameshindwa. Wala CCM hutawasikia wakidai wameshindwa hivyo wanaomba msaada. Yaani wote wanaweza isipokuwa kwenye taasisi za serikali.

Worse enough, Mkurugenzi mwenyewe wa Bandari anatangulizwa mbele kutetea mkataba. Yaani a akubali hawezi hiyo kazi yake. Sasa kwa nini asiwapishe wengine au wampishe mwenye uwezo.

Hao DPW wenyewe wakija wanaleta experts tu. Wao wamewekeza pesa. Wanaajiri wataalamu. Kwa nini na sisi tusiwekeze kwenye expatriates kama wao!?
 
Sema wewe
Mpaka sasa %kubwa ya wanaopinga hawajui wanacho pinga.

1.Maana Wanasiasa wakisema Mkababa mbovu basi nawao wanasema hivyo.
2.Wanasheria wakisema kuna vipengele vibadilishwe vinatubana nawao wanase hivyo.
3.Viongozi wa Dini wakisema tusimpe mwekezaji nawao wanasema hivyo.
Basitu ilimradi waonelane nawao hawapo nyuma
Sema wewe mwenyewe ndio haujui nini kinaendelea, unafuata upepo na wakati mwingine hauna uhakika kama upepo umepita au bado, kk mnashida sana.
 
Washindani? Haahaaa embu tuwe serious mkuu!!
Niko siriaz 101% labda nifafanue. Hii ishu Ni kuanzia kukwambia kwa ujenzi wa bandari ya bagamoyo. Hii haikuwa bahati mbaya bali USA na hawa Waarabu waliweka mkono wao.

Sababu: ikiwa bandari ya bagamoyo ingejengwa na ikiwa shughuli za bandari ya dar zitapanuliwa na kufikia viwango vikubwa Basi Dubai itakuwa hatarini kwasababu:
uchumi wa Dubai inategemea bandari.

Km bagamoyo itajengwa na dar kufikia viwango vya juu maanake mizigo 80% inayotoka china kuja ukanda huu wa Afrika haitapitia Dubai Tena. Itakuja moja kwa Moja Bagamoyo.

Hivyo wakiweza kuiendesha bandari ya dar wataweza kubalansi hii ishu.


Kikubwa ndiyo maana ktk huu mkataba wameweka kipengele kwamba Ni LAZIMA km kutakuwa na fursa au shughuli yyte mpya ya bandari lazima wajulishwe wao kwanza.Hii Ina maana wao ndiyo Alfa na omega.

Ukitaka kuijenga bagamoyo lazima uwaambie wao. Huu Ni utumwa.

Sijui km nimeeleweka.
 
Katika wiki mbili hizi zilizopita kumekuwa na mvutano mkubwa juu ya Serikali kuingia mkataba na kampuni ya DP World kutokea Dubai na mvutano huu umepelekea wananchi kupinga vikali makubaliano yoyote kati ya serikali hizi mbili.

Swali langu ningependa kujua kipi hasa kinachopingwa kati ya hivi viwili;
1. Vipengele vilivyo katika mikataba hiyo ya makubaliano
2. Uwekezaji wowote kutoka nje ya nchi katika bandari yetu

My take: Tunatakiwa tuwe makini sana na vipengele vya kwenye mikataba yoyote ya kiuwekezaji inayofanyika nchini na kuhakikisha tunakwepa unyonyaji wa aina yeyote lakini pia nina uhakika kuwa sisi kama watanzania bado hatuna ufanisi wa kuendesha bandari (hili limethibitika kwenye kila sekta inayoendeshwa na serikali kuanzia TANESCO, Idara za maji, Reli, TTCL n.k)
Wengi wanapinga kwa sababu za kibaguzi tu kwa kuwa wawekezaji Waarabu aka Waislam.


Nje ya hayo ni porojo tu.
 
Toeni maoni yenu na serikali imekiri itayapokea kabla ya kusain huo mkataba,acheni na wanaopotosha mara uzanzibar mara bandari imeuzwa,hao wameshavurugwa

Bora kidogo umetoa neno lenye maana bira kukashifu wagalatia. Maoni na ushauri ni wa muhimu sana kwenye huo mkataba. Kwanza na la muhimu mkataba uwe na kikomo ata Kama ni miaka mia sawa. Pili Zanzibar isiachwe nyuma kwenye kufaidi hii cake ya DP world maana bandari ni suala la muungano hivyo sio vizuri tanganyika kufaidi wao tu
 
Back
Top Bottom