Diwani
JF-Expert Member
- Oct 25, 2014
- 2,672
- 2,697
Tangu kuanza kwa sakata la bandari mapema mwezi Julai kumekuwa na mgongano wa Mawazo kati ya Wanasiasa na Wanaharakati wa Kisiasa maeneo na Taasisi mbali mbali nchini.
Tumekuwa na Jadi ya mijadala kama nchi ya Kidemokrasia kwa muda, ila hili la DP World, limedhihirisha masuala yafuatayo ambayo labda hayana uhusiano kabisa na sakata (Mkataba) wenyewe.
Mambo yenyewe ni.
1. Amani yetu haitokani na umoja na mshikamano, bali kuvumiliana, Uoga na Unafiki. Si kweli kwamba tunapendana au tumeshikamana, ila tunachukuliana kwa vijicho vya misingi ya dini zetu.
2. Tunawatazama wawekezaji kwa dini zao. Nchi inasumbuliwa na UDINI. Waislamu wanawatazama Wazungu kama Wakristo, na Wakristo wanawatazama Waarabu kama Waislamu.
3. Hakuna uelewa kuhusu masuala ya bandari. Kundi kubwa la watu halijui masuala ya Mikataba, lenyewe linafuata tu upepo wa Taasisi zao zinasemaje.
4. Tunaongozwa na Kiongozi Muoga; Ishara ya "Kunyamaza" sio ishara nzuri, Taifa halisimamishi kiongozi wake ili anyamaze? Nani anaogopwa hapa?
Tujitafakari, kuna mahala tumefika.