Sakata la Askofu Alex Malasusa lachukua Sura Mpya, Watoto Watoroshwa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
MUME wa mwanamke anayedaiwa kumkamata ugoni Askofu Dk Alex Malasusa wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania (KKK) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, (DMP) anatafuta watoto waliotoroshwa kwa maelekezo ya Malasusa na Jeshi la Polisi,
Akizungumza na MwanaHALISI online baada ya kuachiwa huru kutoka polisi kwa tuhuma za kushambulia, amesema watoto wake walichukuliwa na raia mmoja mjerumani aliyeolewa na mtanzania, anaitwa Caroline Shedafa.

Caroline Shedafa ametuhumiwa kuwa ametumia mwanya wa malalamiko ya Mwakilima na Malasusa kwa sababu ya urafiki alifanikiwa kuwatorosha watoto hao na kwamba ana mpango wa kuwasafirisha kwenda nje ya nchi wakati wowote.

MwanaHALISI limemtafuta Shedafa kwa tuhuma hizo, alipokea simu na baada ya kuambiwa kuwa anaongea na MwanaHALISI alikata simu na kukataa kuongea suala hili na mwandishi.

Malasusa anadaiwa kuwa anadaiwa kushirikiana na mfanyakazi wa hospitali ya Muhimbili anayeitwa Julieti, aliyewaambia ndugu wa mume anayenyang’anywa mke wake na malasusa kuwa atakiona.

“Huyu kaka anajidai mjuaji, hapti kitu, utaratibu uko tayari wa kuwasafirisha watoto kwenda nje ya nchi na hatawaona tena, ataishia kuwasikia tu, mimi ni mtu wa Karibu na Askofu Malasusa ndo nawaambia”. Alinukuliwa dada huyo akiongea kwa ujasiri.

Hadi sasa watoto wanaotafutwa na baba yao ambao Jeshi la Polisi linadaiwa kushirikiana na Malasusa licha ya taarifa zao kufika polisi kituo cha Wazo na kutochukuliwa hatua ni Sijenuni, Sephania, na Simon wote wanadaiwa kuwa watoto wa Venance Mwakilima.

Taarifa za leo usiku zilizofikiwa MwanaHALISI online zinadai kuwa baadhi ya Maaskofu Jijini Dar es Salaam wameamua kujitokea kulinda heshima ya uaskofu baada ya kudhalilishwa na Malasusa.

Maaskofu ambao hawakupenda kutajwa majina yao kwa kuwa si wasemaji wa vikao halali wamesema “hili suala tunalichukua,

Malasusa ana tuhuma nzito nchini, na baada ya gazeti kuandika watu wamejitolea kujieleza tunaomba muda kesho (Jumanne) tutaliongelea hadharani baada ya kukutana na mume wa me.

Aidha Malasusa hakupatikana kwenye simu zake wala kujibu ujumbe wa simu aliotumiwa tangu juzi wakati gazeti la MwanaHALISI likiendelea kufuatilia sakata hili.
 
Huu uongo uliodumu kwa karne nyingi kutoka mashariki ya kati uko karibu saana kushtukiwa na watu....its matter of time..hizi tamaduni mbili za waarabu na wayahudi zimenufaisha saana watu kwa muda mrefu...naona ziko ukingoni now
 
Ama kweli binadamu huwezi kwenda kinyume na maumbile, maaskofu oeni au kama vipi mhasiwe basi!
 
MUME wa mwanamke anayedaiwa kumkamata ugoni ,,,,MSETO…


..MSETO…[/QUOTE]

Huyu Sayed Kubeneasalam hawajui waliompigia kura mpaka anamchafua kiasi hiki Kiongozi wao wa Kiroho kwenye kijarida chake cha UDAKU. Anawakilisha maslahi ya nani katika hili? Mafisadi ambao Askofu amekuwa akiwakemea au ni Siasa chafu?. He is just fighting a loosing war, to tarnish the image of our spiritial leader. Kanisa limekuwepo toka zama, jana na leo na kesho lipo tu na linakua kwa kasi. Hivi Mh. Mbowe anayekaa viti vya mbele pale KKKT Azania Front kama alivyokuwa Mareh Baba yake Aikaeli ameshindwaje kuliona hili taka linalopikwa na Mbungi wake? Shame thing! We stand unmoved by your mud slinging campaign, We trust and love our Bishop!
 
Kuna uwezekano huyo jamaa amenyanyaswa sana mpaka akafikia kuweka mambo hadharani especially pale inakuja kumtuhumu mtu mwenye hadhi ya Malasusa. Hawa ni watu hatari, wanaaminika kwenye jamii, anaweza kukupoteza kweli sababu hakuna mtu ataamini story yako.

Watu kama Malasusa wakiamua wanakufanya maisha yako yawe miserable kabisa sababu wao wanaonekana hawawezi kutenda dhambi Kabisa na pia kanisa haliwezi kukubali kuingia kwenye kashfa za namna hiyo wao watamuadhibu askofu kwa utaratibu wao ila sio public ijue.

Huyu jamaa kama story yake ina ukweli na ana ushahidi basi anahitaji kutumia akili ya hali ya juu kufight hiyo battle maana mke anahakikisha status yake inalindwa na Malasusa nae anafanya hivyo hiyo na kanisa pia linafanya hivyohivyo so ni vita nzito he must be brave and fight bravery!

Nachoweza kusema ni kwamba hawa wanawake tuwaone tu kwenye sketi akiwa mkeo jifunze kuishi nae kwa akili na busara kubwa otherwise wanakuingiza kwenye mambo ya ajabu mwishowe unajikuta umempiga na kumuabuse lazima uwe na akili.

Mwanamke anakukosea na anakufanyia visa, ukiwa na ubongo mwembamba utajikuta umemuabuse, mwanaume lazima ufikirie mara mbili, kwa nini amekukosea? Kwa nini anakujibu hovyo? Lakini kwa nini umpige hata kama anakujibu hovyo na kweli una ushahidi amekukosea? Hapo unamuacha and just move on hata kama mna watoto kumi go and live your life.
 
Kama askofu alimtumia makonda kumfungulia kesi mume wa mchungaji hawara wa askofu, huyu mume nae amtumie makonda kuwataarifu askari kuwa askofu kaiba watoto wa mtuhumiwa, ndio si makonda anajali ulinzi na usalama wa raia wake? basi isiwe kwa wakubwa tu hata wanyonge pia, watoto wamepotea ni wananchi wake wa Dar. Na kumsaidia makonda baba wa watoto akatoe taarifa kwenye TV watoto watangazwe kupotea.
 
Huu uongo uliodumu kwa karne nyingi kutoka mashariki ya kati uko karibu saana kushtukiwa na watu....its matter of time..hizi tamaduni mbili za waarabu na wayahudi zimenufaisha saana watu kwa muda mrefu...naona ziko ukingoni now
Kweli kabisa ukiangalia kilichopo behind hizi dini kuna upuuzi mwingi sana unafichwa ili kulinda madhehebu haya
 
Back
Top Bottom