minda
JF-Expert Member
- Oct 2, 2009
- 1,068
- 67
WANA JF SOMENI HII HBR KUTOKA MWANANCHI LA HIVI KARIBUNI:
Thursday, 03 June 2010 22:32
0diggsdigg
Habel Chidawali, Dodoma na James Magai, Dar
MGOGORO uliolikumba Kanisa la Anglikana Tanzania, unazidi kupamba moto hasa baada ya uongozi wa kanisa hilo,kusisitiza kuwa wenzao waliojitenga, hawatambuliki tena kuwa ni maaskofu kwa kuwa walishafukuzwa.
Katibu mkuu wa kanisa hilo, Dk Mwita Akiri, aliliambia gazeti hili jana kuwa watu hao wanaoendelea kujitambulisha kuwa ni maaskofu, wanapaswa pia kuzuiwa wasisajili kanisa jipya.
Mwita ambaye pia ni Askofu Mteule wa Dayosisi ya Tarime, alisema kitendo cha kujitenga na kanisa kilichofanywa na Askofu Ainea Kusenha, David Matonya na Naftari Bikaka ni uhaini kwa kanisa hasa ikizingatiwa kuwa kililenga katika kulidhalilisha Kanisa la Anglikana.
Lakini wakati Mwita akitoa msimamo huo dhidi ya maaskofu waliojiengua kutoka katika Kanisa la Anglikan na kuanzisha Kanisa la Anglikani la Kiinjili Tanzania, wamejibu mapigo kwa kusema kuwa Kanisa Anglikana, halina uwezo wa kuiamuru serikali iwachukulie hatua.
Wachungaji hao jana walikutana jijini Dar es Salaam na kutoa tamko kuhusu sakata hilo.
Walisema wao wanalindwa na katiba ya nchi inayotoa haki kwa watu kuabudi dini wanayotaka ili mradi hawavunji sheria za nchi.
Walisema kwa msingi huo, ni haki yao kujiondoa kutoka Kanisa la Angalikana na kuanzisha kanisa jipya.
Akisoma tamko hilo Mchungaji Isaya Chiyungu, alisema kauli ya maaskofu hao haina msingi kwa kuwa katiba inatoa uhuru kwa kila mtu kuamini na kuabudu dini inayotaka.
Alisema wao wameamua kujiengua katika kanisa hilo kwa kuwa hawataki malumbano wala ugomvi na kwamba wanataka demokrasia katika kuabudu.
"Tumeamua kuanzisha kanisa hili kwa kuwa tunataka kuabudu kwa uhuru amani na utulivu, ndio maana tumeamua kufuata taratibu zote za kikatiba,"alisema Mchungaji Chiyungu.
Alisema wanaamini kuwa kwa sasa hakuna kanisa lolote nchini lililosajiliwa kwa jina la Kanisa Anglikani la Kiinjili Tanzania na kuiomba serikali iwape usajili ili waweze kudumisha na kuendeleza amani.
Askofu Naftali Bikaka wa Kigoma alikanusha kauli kwao wao ni waasi na kwamba waasi ni watu wanaoacha kufuata maadili na imani ya Ukristo.
Alitoa wito kwa waumini wengine wa kanisa hilo na mengine wanaona kuwa hawana uhuru wala amani na utulivu katika kuabudu, kujiunga na kanisa hilo wakati