Sakata la Amri ya Kuwakamata Maaskofu : Mahakama yetu haijawa ya Kadhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la Amri ya Kuwakamata Maaskofu : Mahakama yetu haijawa ya Kadhi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OgwaluMapesa, Jun 16, 2011.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  SERIKALI yetu haina dini.Iliamuliwa hivi na kutambuliwa na katiba yetu yenye viraka.Natamani ibaki hivi hata katika katiba mpya itakayokija kama watawala wetu hawatabadili mawazo yao.  Kwamba,Watanzania wenye dini wawe huru kuabudu wanavyotaka ,kwa jinsi wanavyoona inafaa.Wakiamua kuwa na viongozi wachaguane kwa jinsi wanavyokubaliana na wasivyokubaliana .Naam wafanye hivyo ilimradi kufanya hivyo kusivunje sheria na kuwantima wengine uhuru wao wa kuabudu na kutoabudu.


  Kwa Mazoea yetu,mambo ya ndani ya dini zote Nchini ni kwa mujibu wa katiba zao na hata wale wanaoabudu bila katiba .Baadhi ya dini zina mahakama zao hazitapitiwa na mahakama nyingine yoyote kwa sababu hazitambuliki wala kuheshimiwa na sheria yoyote iliyotungwa na bunge letu.

  Mazoea yetu haya ,ni sehemu ya vyanzo ya amani ya Taifa Letu.Hakuna dini rasmi ya serikali hata kama baadhi ya viongozi wa dini wanaweza kujifanya au kufanywa kuwa ni wazito kuliko wengine.Mbele ya sheria za Nchi ,kiongozi wa dini au wa jadi mwenye tunguli na kiongozi wa dini mwenye msalaba wa dhaabu au kiongozi wa dini mwenye ndevu zinazotisha-wote hawa wako sawa .Dola yetu na vyombo vyake havina mamlaka ya kuhingia hulo kwenye dini kuamua ni jinsi gani Nzuri ya kuabudu ,kiongozo gani anaifaa dini ile,na Mahubiri gani yanafaa kwa ajili ya muumini kuwa karibu na muumba kuliko mengine

  Watu huenda huko kwa utashi na huondika kwa utashi wao au uondolewa na sheria huko huko kwenye dini.Asiyekubaliana na jinsi mambo yanavyokwenda huko ndani, atoke aanzishe dini yake itakayofanya anavyopenda yeye na kundi lake.

  Aidha mahakama zetu huendeshwa na fedha za walipa kodi wote wenye dini na wasio na dini ,na kwa hiyo si haki kabisa kutumia fedha zetu katika dini yoyote inayohudumia waumini wa dini hiyo tu.

  Habari za amri ya mahakama kuwakamata na kuwafungulia mashtaka ya jiai ,Maaskofu wawili wa kanisa la Anglikan huko Arusha-Askofu mkuu Dr Valentino Mokiwa na Stanley Hotay,zimeyeyusha imani yetu ndogo iliyokuwa imebaki katika mahakama zetu.Tulio wengi tulidhani mjadala wa ama kuanzisha au kutoanzisha mahakama ya kadhi ulikuwa bado haujaamuliwa bado na kwa hiyo ,mahakama zetu bado hazina dini wala uelewa wowote juu ya mambo ya dini


  Maaskofu Valentino Mokiwa ambaye ni askofu mkuu wa kanisa Anglikana Tanzania na Askofu mpya Stanley Akonay,Wanashtakiwa kwa kukaidi amri ya mahakama iliyowazuia wasifanye ibada ya Kumsimika Askofu Stanley Hotay ili awe askofu wa eneo la Arusha.Wao wanajitetea kuwa Askofu Stanley Hotay hakusimikwa kuwa Askofu wa eneo la Arusha ,na badala yake ilifanyika ibada ya Kumfanya stanleY Hotay awe askofu wa Kanisa Anglicana Tanzania.

  Kuna hatari mbele yetu : leo ni kuzuia Ibada ,Kesho maubiri yatazuiwa ,keshokutwa mfungo utaombewa kibali na baada ya hapo ubatizo itabidi ujadiliwe mahakamani .Kimsingi baadhi yetu tunashangaa na kwa nini jaji hakuamuru hata wakristo walioudhuria akiwamo mkuu wa mkoa wakamatwe! Hii ni kwa sababu hakuna ibada kama hakuna watu.Kumkataza Askofu mkuu na Askofu aliyefanywa Askofu bila kuwakamata waliodhuria ibada ni kuonyesha kasoro ya uelewa kuhusu ibada aliyoizuia .Yawezekana tuna tatizo kubwa zaidi ya tunaloliona -kwamba ,labda baada ya mahakama kukosea njia na kuhingia mahali pasipo pake imechangiwa na kukosa njia ya kutoka.Ni hatari sana kwa mahakama zetu kuhingilia masuala ya dini ,na pengine ndio maana hata waislaam wanapata taabu sana kukubali mahakama hizi ziendelee kushughulikia mashauri ya kiislam yenye suluhu ya kidini

  Sio siri kwamba majaji wazoefu wanalazimika sasa kuwa viranja wa kusimamia Majaji wapya wanaotanguliza mamlaka zao zisizohojiwa na kuacha kutumia muda wa kutosha kujielimisha juu ya masuala yanayoletwa mbele yao.

  Na kwa kuwa anayeteua ni mwanasiasa ,tunaanza kuona majaji wanaonuka siasa katika maamuzi yao.Kwa hili la kuwakamata maaskofu kwa kosa la kufanya ibada ,watu hawawezi kuacha kulihusisha na matukio mengine yaliyowaweka maaskofu uso kwa uso na watawala,

  lipo suala la tuhuma kwa Askofu Mokiwa alipelekewa mamilioni ya fedha ili akae kimya wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopota.Lipo tuhuma nyepesi nyepesi za makada wa Chama tawala kuwa Maakofu wanajihusisha na siasa wakiegemea kuviunga mkono vyama vya Upinzani,Lipo tuhuma za Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Jakaya kikwete kuwa kuna maaskofu wanauza madawa ya Kulevya,Wengine tumekwenda mbali zaidi na kuhoji ni kwanini mwakilishi wa Rais Kikwete Steven Wasira hakufika kwenye hafla hiyo ya Arusha? Alijuaje kuwa ibada itazuiwa na Mahakama? Hata alipojulishwa na serikali ya mkoa ,Bado alishindwa kufika na kuwajulia hali viongozi wa kanisa ilihali amri ya mahakama ilitoka ijumaa na ibada ilikuwa jumapili

  Ni vema tukakubaliana kwamba mapema kuwa, Siasa Chafu,Rushwa katika mahakama zetu haviwezi kuondolewa kwa kuvigeuza kuwa mahakama za Kadhi
   
 2. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Maaskofu wanaisema sana serikali sasa mzee wa visasi amebuni njia ya kulipa kisasi huyu bwana anajaribu kwa kiasi kikubwa kuivunja nchi hii usalama wa taifa haupo tena. Israel walipomwo Yitzak labin anakwenda kama huyu wakwetu alipigwa chuma akawekwa mtu mwingine. sasa kabla nchi haijaharibiwa na huyu bwana bora aondolewe kwa njia yeyote ile wa kujilipua mpo?
   
 3. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapa ni kwamba jaji ameshindwa kutumia common sense, sheria zinakwenda na common sense, huwezi kutumia sheria tu bila common sense na ukawa umetenda haki. Kutokana na maelezo ya pande hizo mbili, uchaguzi ulifanyika aprili, walalamikaji hawakuchukua hatua kama waliona kuna kasoro, leo watu kutoka pande mbalimbali za dunia wameshaarikwa na wamefika kuhudhuria ibada hiyo eti mahakama inatoa zuio, no, busara na common sense vinahitajika hapo. Zaidi ya hayo jaji inatakiwa awe makini sana anaposhughulikia maswala ya dini kwa kuwa naamini hana utaalam nayo, na ndio maana askofu kampiga chini jaji kwa kutoa hoja kwamba alichofanya ni kumsimika kuwa askofu wa anglikana na sio wa jimbo lenye kubishaniwa, hapo askofu tayari kwa akili ya kawaida kamshinda jaji labda tu kama jaji akiamua kutumia madaraka yake vibaya na hapo ndo atakuwa ameharibu kila kitu, waswahili walisema "heri ya nusu shari kuliko shari kamili. Na hapa linakuja suala la kisheria, hii ni kesi kati ya mtu na mahakama, yaani mahakama ndiyo mlalamikaji kwamba imedharauliwa, nani ataamua kesi hii? sio haki kisheria kuamuliwa na mahakama hii tena kwa sababu no one can be judge in his own course.
   
 4. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mahakama ya Kadhi imeingiaje? Am I missing the point?
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  JK ni miongoni mwa marais waliofeli kuongoza kwa kuwa hana upeo na ni mbumbumbu ....i really doubt about his capacity to think in logical terms?? i have serious doubt on him!!!!
   
 6. shemasi

  shemasi Member

  #6
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  busara itumike zaidi kwenye jambo hili
   
Loading...