#COVID19 Sakata Askofu Gwajima dhidi ya Bunge, Mawaziri na Baadhi ya Wananchi limechora Uhalisia wetu

Upigaji umerudi kwa kasi ya 4G, kiukweli watumishi wa umma hawaogopi kabisa saiv, kwenye tenders huko pesa zinapigwa vibaya mno, michezo ya mzabuni kulipwa 60m ikiwa zakwake halali ni 25m, zinazobaki za wapigaji, ndio michezo imetamalaki kwa sasa, ngoja report ya CAG inayofuata mtaona vichekesho.
Thibitisheni hayo madai yenu, msiandike tu kujilizaliza bila sababu.
 
Wwe niambie maana ya Uaskofu, Maana me najua Askofu maana yake ni muangalizi wa kanisa


Askofu ni mtu mwenye cheo cha juu katika Kanisa. Kwa kawaida huliongoza katika eneo la dayosisi (jimbo) akisimamia shirika au parokia nyingi.


Haijazungumziwa shule au chuo cha kusomea. Hamna
 
Uliungana naye wewe sio Watanzania.Ushindi gani watu wanaendelea kufa kwa Covid.We fala sana na huyo Kibwetere wenu

Iko siku isiyo na jina ambapo wenye ndugu zao waliokufa baada ya kuchanjwa watapaza sauti na watasikika.
 
Kuna toleo jipya ya Chanjo J&J dozi 2 yenye uwezo wa 94%
Ile Chanjo ya msaada tuliambiwa ni Salama inafaa kwa matumizi.
wenye Chanjo wametengeneza wamekuja Na Toleo jipya.
Bila kusema uongo Toleo la kwanza la J&J litakuwa na mapungufu kwenye utendaji.
Kama lingekuwa na uwezo wasingetengenezo Toleo Jipya.
 
Naona wale maadui watatu aliowaainisha Mwalimu Nyerere miaka ya 1960 bado wapo imara 50 years later na sasa wamekuwa nguvu kuliko wakati ule wa uhuru. Hasa adui ujinga.
 
Limeisha. Mshindi amekuwa Askofu Gwajima. Pascal Mayalla kwa mara nyingine tena amepigwa KO. Nakumbuka alivyokuwa akishadadia Gwajima afukuzwe ili yeye Pascal arudi tena kwenda kuomba Kura katika lile jimbo.

Gwajima amebaki na msimamo wake pamoja na wana Kawe ambao walisema wazi wazi bila kumung'unya maneno " HATUCHANJIIIIIIII" mbele ya Rais Samia Suluhu.

Kilichoonekana ni Ujasiri ambao wengine walikosa. Gwajima alikuwa nao na Watanzania wengi wakaungana naye. Sasa niambie wapi zinaimbwa tena zile nyimbo za Chanjo?

Tushapokea msaada nchi imerudi kwenye flight mode. Rais anapangiwa safari tu watu wanagawana zile pesa za msaada. Angalia jinsi ATCL wanavyipana.

Angalia semina ambazo zinatoka Dodoma kuja kufanyika Dar. Angalia jinsi Mawaziri,Makatibu wanapishana Dar kila Uchwao. Haya maisha ndiyo tuliyotaka kwa kweli. Hakuna kufuatiliana. Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.

Yule mama Waziri naona Kampeni naye imemshinda....sasa hatuoni watu wakipost picha na videos wakichanja.nchi hii tunaishi kinafiki sana. Zile chanjo inasemekana zimesha expire. Chanjo Mil 1 katika nchi yenye watu wanaostahili kuchanja zaidi ya milion 20 bado hazijaisha.

Gwajima Askofu ameibuka mshindi kwa KO na bado anashikilia mkanda mwingine wa kuwa na msimamo wa kile anachoamini.
Bado anatoa mahubili kila jumapili kuwaambia wajinga wake pale kanisani?
 
Majuzi hapa tumetangaziwa hapa kwenye dispensari ya Kijiji zimeletwa chanjo za covid hivyo hakuna haja ya kwenda wilayani, maajabu sasa wananchi wameapa hawaendi kutibiwa hapo wasije wakachomwa chanjo hizo bila wao kujua...huduma zimesusiwa bhagosha!!!
 
Kusutana si kuzuri hata kidogo. Nawashauri nyote hivi.

" Aliyechanjwa amuombee heri ambaye hajachanja. Ambaye hajachanja amuombee heri ambaye amechanja. Aliyechanja akipata madhara ambaye hajachanja awahi kumsaidia aliyechanja; vivo hivyo, ambaye hajachanja akipata madhara aliyechanja awahi kumsaidia ambaye hajachanja.

Ni kwa msingi huu, tutawashinda kirahisi sana wale wote wanaotaka kutugombanisha, kuvuruga amani, umoja na ushirikiano wetu kwa kutumia chanjo".

Tutakianeni kila la heri.
 
Back
Top Bottom