Nashauri bunge, Serikali na Mahakama waachane na Gwajima, wana mambo mengi na ya msingi kwa manufaa na ustawi wa taifa

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
8,256
9,085
Kamati ya nidhamu ya bunge baada ya kumaliza kazi yake iliwasilisha taarifa yake mbele ya spika na bunge kwa Ujumla na kupitisha azimio dhidi ya Gwajima na Jerry Slaa.

Kwangu mimi sikuona haja ya kuwaadhibu wabunge hao adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili ya bunge,kwani adhabu hiyo imeumiza wananchi waliowachagua kuwawakilisha.

Ni bora wangewaacha wahudhurie mikutano bila posho,ingependeza sana ,kwasababu ingewaathiri wao moja kwa moja .

Leo tena Askofu Gwajima kaeleza kilichojiri kwenye kikaango cha kamati ya nidhamu, na kaelezea msimamo wake na wa familia ya kanisa lake ya kuendelea na hiari ya kutochanja .

Ameongea kwa tahadhari na umakini mkubwa sana bila kushambulia yoyote yule ,akiwa na reference mbalimbali duniani kuhusiana na madhara ya chanjo.

Maswali ya Gwajima ni kwamba anataka wataalamu wafafanue kwa kina madhara ya muda wa kati na mrefu wa chanjo hizi mwendo kasi ,hapa ni muhimu sana.

Kingine, hata bungeni na serikalini kuna viongozi wengi wanaungana na hoja za Gwajima sirini .

Kutunishiana misuli na Gwajima ili kuzima hoja zake si sawa hata kidogo,ikizingatiwa msimamo wa serikali miezi michache kabla ya hayati Magufuli kufariki unajulikana na uko wazi kwa watanzania wote ,teknolojia haiongopi .

Mwisho kwa kuwa imeonekana short moja ya chanjo haitoshi,huu ni mzigo mkubwa sana serikali kuubeba,utaturudisha nyuma sana,tujihadhari nao sana
 
Sio sahihi kumuachia huyu mtu awapoteshe watu.
Babu wa Loliondo alisababisha vifo vya watu wengi kwa kuachiwa aendeleze upuuzi wake nadhani pia unakumbuka ya Kibwetere,
 
Soma link mbalimbali duniani uone Gwajima alivyo sahihi
 
Kamati ya nidhamu ya bunge baada ya kumaliza kazi yake iliwasilisha taarifa yake mbele ya spika na bunge kwa Ujumla na kupitisha azimio dhidi ya Gwajima na Jerry Slaa.

Kwangu mimi sikuona haja ya kuwaadhibu wabunge hao adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili ya bunge,kwani adhabu hiyo imeumiza wananchi waliowachagua kuwawakilisha.

Ni bora wangewaacha wahudhurie mikutano bila posho,ingependeza sana ,kwasababu ingewaathiri wao moja kwa moja .

Leo tena Askofu Gwajima kaeleza kilichojiri kwenye kikaango cha kamati ya nidhamu, na kaelezea msimamo wake na wa familia ya kanisa lake ya kuendelea na hiari ya kutochanja .

Ameongea kwa tahadhari na umakini mkubwa sana bila kushambulia yoyote yule ,akiwa na reference mbalimbali duniani kuhusiana na madhara ya chanjo.

Maswali ya Gwajima ni kwamba anataka wataalamu wafafanue kwa kina madhara ya muda wa kati na mrefu wa chanjo hizi mwendo kasi ,hapa ni muhimu sana.

Kingine, hata bungeni na serikalini kuna viongozi wengi wanaungana na hoja za Gwajima sirini .

Kutunishiana misuli na Gwajima ili kuzima hoja zake si sawa hata kidogo,ikizingatiwa msimamo wa serikali miezi michache kabla ya hayati Magufuli kufariki unajulikana na uko wazi kwa watanzania wote ,teknolojia haiongopi .

Mwisho kwa kuwa imeonekana short moja ya chanjo haitoshi,huu ni mzigo mkubwa sana serikali kuubeba,utaturudisha nyuma sana,tujihadhari nao sana
Gwajima hawezi kuachwa, huyo ni kirusi kwa usalama wa Taifa,inatakiwa apewe stahiki yake
 
Tatizo Ndugai anjifanya much know , aache watanzania wauseme ukweli hata kama ni mchungu
 
Back
Top Bottom