Saini zakusanywa kumng’oa Makinda

Saini zakusanywa kumng’oa Makinda

sijaona hoja ya msingi hapo ya kumng'oa spika. Kuna mambo mazito na ya msingi ambayo anaweza kusimamia na kushinikiza kung'oka kwa spika, lakini kwa hoja hiyo ni kama kumpigia mbuzi gitaa.
 
Mkuu maana ya Kigwangala ni kwamba iwapo Spika ataingia leo Bungeni na kusema haya Wote mulipwe hizo laki 4 na thelathini basi hoja yake ataiondoa .Huyo Chenge haja chaguliwa leo alikuwa wapi sikuzote kulalamika...nadhani tatizo hapo ni maslahi tu kama ni Kanuni hapana...hapana... Kigwangala asitudanganye na hatudanganyiki

Kinachonifurahisha mie binafsi ni jinsi Tundu Lissu anavyojua kutia kachumbari ndani ya hoja hii ya wanaCCM
 
Kigwangwala,kama wanafiki wengine bungeni,hajawahi kuwa mtu wa kusikilizwa kwa makini.Ni mpiga kelele wa kawaida tu.....!
 
Kigwangwala,kama wanafiki wengine bungeni,hajawahi kuwa mtu wa kusikilizwa kwa makini.Ni mpiga kelele wa kawaida tu.....!
Hata hoja yake ya wabunge kujilipa posho ya sh 430,000/= kwa siku hutaki kuisikiliza? Watanzania tunayo matatizo sana.
 
Mbona nasikia wanataka kumuondoa kwenye kiti cha uspika nitazimsi sana zile senki yuu vere macheeee zake.
 
Kingwangalla anatafuta kukatwa mapembe, shauri zake: panya anapochimba shimo mara nyingi huzingatia size ya mlango wa shimo maana anajua kuna mapanya buku pia yataingia kupitia mlango ule ule

jamaa anatafuta namna ya kutoka ingawa Spika anahitaji kuwekewa utaratibu wa kisheria katika kutoa malipo ya posho za wabunge. Kwa utaratibu huu wa kutegemea leo karidhikaje akaidhinisha posho kwa rate fulani na kesho kwa kuangalia kamati anayodhani inastahili kulipwa zaidi anafanya hivyo. Lazima kuwe na specified/approved rates za posho kwa kazi mbalimbali za bunge. Huu ni ufujaji wa kodi zetu. Ngoja kwa kutafuta sifa, Kigwangala anaweza kuibua nidhamu katika taasisi hiyo nyeti nchini.
 
sisi tupo nje hoja yake pengine ina mashiko kama angeweke uthibitisho hapa jamvini ili tumuelewe anatetea nini mara nyingi hawa jamaa hawaaminiki wanatetea nini ,kosa ni kuwa yeye kapewa posho kiduchu au nini hasa
 
Tumsupport kigwangala na yey kamati yake iongezewe iyo posho labda mzee kule kijijin anaweza pata pesa ya matibabu baada ya ili zoezi!!!
 
Kweli nimeamini ule usemi usemao kuwa pesa ndio chanzo kikubwa cha ugomvi, Yaan Ndugu Kigwangala siku zote bunge linaendeshwa kwa upendeleo na wao kupitisha mambo ya kijinga kwa Kutumia uwingi wao lakin yeye huwa na imani na Spika lakini leo yeye kapunjwa Posho ndio imani na spika imetoweka!! Kaazi kwelikweli.
 
mwacheni ajaribu bahati yake huenda akafanikiwa who knows!!!!!???
 
Kigwangwalla anatapata anajuwa kikomo cha yeye kuwa mbunge muda umebaki mdogo sana kwahiyo anataka kuvuna asichokipanda kwa kodi zetu.
 

“Si kweli kwamba Kamati ya Bajeti inalipwa fedha za ziada kila wakati, hapana, ni pale tu wanapoomba malipo hayo kutokana na sababu ambazo lazima Spika aridhike nazo. Ieleweke kuwa siyo kamati hiyo tu,
kwa sasa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ambayo inachambua miswada mingi nayo imekuwa ikiomba na baada ya Spika kuridhia basi nao wanapewa,” alisema Dk Kashililah.
Dah! Hapa ndo ninapoipendea Siasa! Yaani Mheshimiwa Tundu Lissu hapa anasifinya kimyakimya; akirudi bungeni "waalimu mishahara haitoshi, wabunge wa CCM mnataka posho zaidi!"
 
Kigwangalla anatishia NYAU, hakuna kitu hapo. Ataitwa na Sophia Simba na kupewa VIDONGE vyake halafu atafyata mkia kama mbwa koko. Au mmesahau Hawa Ghasia alivyompatia vidongo vyake wakati fulani akaufyata.

Ninaweka REHANI KICHWA changu Kigwangalla atakusanya hizo saini! Mnaoamini atakusanya saini za kutokuwa na IMANI na Spika, basi mtaamini kila kitu katika DUNIA hii mtakachokuwa mnasikia/kuambiwa!
 
Anatafuta Cheap Popularity. Ndo leo anajua kuwa Makinda anavunja sheria? Mbna Ndugai anavyovunja hakutaka kumng'oa?
 
Hii ni baada ya spika kukiuka vifungu na kanuni ndani ya bunge leo hii
 
Back
Top Bottom