Saini zakusanywa kumng’oa Makinda

Saini zakusanywa kumng’oa Makinda

rosemarie

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
6,887
Reaction score
3,445
Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla, (CCM), leo anatarajiwa kuanza kukusanya saini za wabunge akitafuta kuungwa mkono katika hoja ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa madai kwamba amekuwa akikiuka kanuni za Bunge.

Dk Kigwangalla aliibua hoja ya kutokuwa na imani na Spika katika kikao cha wabunge wote cha kuelezea shughuli zitakazofanywa na Bunge katika mkutano wa 13, kilichofanyika juzi jioni kwenye ukumbi wa Pius Msekwa.

Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, jana alithibitisha kuwapo kwa mjadala huo katika kikao cha wabunge, lakini hakuwa tayari kueleza kwa undani na badala yake alisema kwamba leo ataanza kukusanya saini za wabunge kwa ajili ya kukamilisha hoja ya kutokuwa na imani na Spika Makinda.

Chanzo chetu kutoka katika kikao hicho cha wabunge kilibainisha kuwa Kigwangalla alihoji kuhusiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge (CCM-Bariadi Magharibi) kuteuliwa na Spika wakati katika kamati nyingine wenyeviti na makamu huchaguliwa na wajumbe wa kamati husika.

Pia Dk Kigwangala alisema Spika Makinda alivunja kanuni kwa kuwapa posho ya Sh430,000 kwa siku wajumbe wa kamati inayoongozwa na Chenge wakati wajumbe wa kamati nyingine wamekuwa wakipewa Sh130,000.

Anachokifanya Spika ni matumizi mabaya ya fedha za umma, inakuwaje wengine wafanye kazi hata bila posho lakini wao (Kamati ya Bajeti), walipwe posho ya Sh430,000 kwa siku?” chanzo hicho kilimkariri Dk Kigwangalla akihoji. Hata hivyo, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah akizungumza na gazeti hili jana alisema mazingira ya kamati fulani kupata malipo ya ziada tofauti na viwango vya kawaida hutokea pale uongozi wa kamati husika unapoomba kwa Spika.

“Si kweli kwamba Kamati ya Bajeti inalipwa fedha za ziada kila wakati, hapana, ni pale tu wanapoomba malipo hayo kutokana na sababu ambazo lazima Spika aridhike nazo. Ieleweke kuwa siyo kamati hiyo tu, kwa sasa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ambayo inachambua miswada mingi nayo imekuwa ikiomba na baada ya Spika kuridhia basi nao wanapewa,” alisema Dk Kashililah.

Katibu huyo wa Bunge alieleza kuwa zaidi ya kamati nane zimewahi kuomba malipo ya ziada kwa maana ya kutaka posho zaidi, ulinzi, usafiri na hata chakula, ikiwa zinakabiliwa na majukumu ya ziada pia katika mazingira tofauti nje ya utaratibu wa kawaida.

“Kimsingi, kamati nyingi zinapewa malipo tofauti, watu wanaweza kuwa na kazi mpaka saa saba au nane usiku, au wanakwenda kufanya kazi katika mazingira yasiyokuwa ya kawaida, taratibu zinamruhusu Spika kama akiridhika na maelezo ya kazi husika, basi anaruhusu kutekelezwa kwa maombi hayo,” alisema Dk Kashililah.

Kuhusu Serukamba

Aidha, Dk Kigwangalla alinukuliwa akisema Spika amekiuka kanuni kwa kumchagua Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Peter Serukamba (Kigoma Mjini-CCM), kuwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti.

“Hakuna mbunge yeyote aliyepo katika kamati mbili lakini hata kungekuwa na sababu maalumu basi wa kuteuliwa angekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Mahmoud Mgimwa (Mufindi Kaskazini-CCM) ambaye TRA (Mamlaka ya Mapato Nchini) ipo chini ya kamati yake,” kilisema chanzo hicho.

 
Heh teh teh!Kingwangala ana ajenda ya siri!

Hana imani na Makinda,lakini ana imani na JK!

Hana imani na Chenge,lakini ana imani na Dr Shukuru Kawamba!
 
ngoja tuone kama hii "ndoto" ni ya kweli
 
Chezea hicho chama wewe!! Huyu kumng'oa si rahisi, ilikua CDM vs CCM sasa naona vita inaongezeka imeanza CCM vs CCM wenyewe, mambo yanazidi kuharibika
 
Kingwangalla anatafuta kukatwa mapembe, shauri zake: panya anapochimba shimo mara nyingi huzingatia size ya mlango wa shimo maana anajua kuna mapanya buku pia yataingia kupitia mlango ule ule
 
Hana lolote huyo.. Anatafuta umaarufu! Kwani hakumbukwi
 
Nilitaka kushangaa kidogo kwa kufikiri labda kuna hoja ya msingi anayotaka kuijenga Kigs. Lakini ukitazama msingi wa malalamiko ya Kigwangala ni posho tu. Ina maana kama yeye angekuwa kwenye kamati anayoilalamikia kupewa posho nyingi asingelalamika. Wao na posho, posho na wao tu. Naskia pia wanataka waongezewe mishahara na posho kwakuwa wapiga kura wao eti wanawaombaga hela. Mweeee!
 
duuuuh hadi Kigwangalah naye anaona Spika kakiuka kanuni? tatizo kubwa hapa naona ni maslahi hizo laki nne wanazopew kamati ya chenge ndo zimewauma sana Spika amekuw akivunja kanuni toka mwanzo tu alipochaguliwa lakini tatizo limekuja baada ya kamati ya Chenge kupokea hiyo posho na kamati nyingine ikiwemo ya kwake kutokupokea ila inawezekana na kamati yake yake ikipewa posho kama hiyo anaweza akanyamaza
 
Katumwa na MEMBE huyu,kwani makinda nae huenda akagombea urais 2015
 
vp Kigwangala wananchi walikupatia majina ya wauza unga au bado
 
Kingwangalla anatafuta kukatwa mapembe, shauri zake: panya anapochimba shimo mara nyingi huzingatia size ya mlango wa shimo maana anajua kuna mapanya buku pia yataingia kupitia mlango ule ule

Kigwangala kwenye pesa hanaga ndugu, rafiki wala uchama/U-CCM, kule kwao Halimashauri ya Nzega ilipewa pesa toka Mgodini za maendeleo ya wilaya yao kama billioni moja na ushehe hivi, Basi Mkurugenzi aliyekuwepo alizidhibiti vizuri zisitumiwe hovyo bila mpango wa kuwa na tija...basi walivutatana naye akisaidiwa na Madiwani kutia fitina, uongo wa kila aina kwa JK mpaka mtu wa watu Mkurugenzi safi asiyekubali kuyumbishwa akahamishwa Nzega sijui kapelekwa wapi...

Sasa hivi yeye na Madiwani wanahomola mipesa hayo kama kuchota toka kapu la mjinga, Mikutano ya kumwaga kila wiki, mkutano wa siku moja basi utafanywa siku tatu au nne posho mlima, Hawaangalii shida ya maji Nzega, shida ya shule za Nzega, Shida ya Zahanati za Nzega, Shida zilizopo Hospitali ya Wilaya etc Kama Billioni ni kubwa kiasi hicho basi tubnasubiri tuone matokeo ya huu urafi wao,

KWA UJUMLA KWENYE HOJA YA POSHO POPOTE PALE USISHANGAE KIGWANGALLA AKAUNGA HOJA YA HASIMU WAKE MKUU BASHE
 
vita sasa imenoga, ni maccm kwa maccm

yetu macho, ukifanikiwa itakuwa heri ingawa una hoja dhaifu
 
duuuuh hadi @H kigwangala naye anaona Spika kakiuka kanuni tatizo kubwa hapa naona ni maslahi hizo laki nne wanazopew kamati ya chenge ndo zimewauma sana Spika amekuw akivunja kanuni toka mwanzo tu alipochaguliwa lakini tatizo limekuja baada ya kamati ya Chenge kupokea hiyo posho na kamati nyingine ikiwemo ya kwake kutokupokea ila inawezekana na kamati yake yake ikipewa posho kama hiyo anaweza akanyamaza

Mkuu maana ya Kigwangala ni kwamba iwapo Spika ataingia leo Bungeni na kusema haya Wote mulipwe hizo laki 4 na thelathini basi hoja yake ataiondoa .Huyo Chenge haja chaguliwa leo alikuwa wapi sikuzote kulalamika...nadhani tatizo hapo ni maslahi tu kama ni Kanuni hapana...hapana... Kigwangala asitudanganye na hatudanganyiki
 
Nikionacho hapa ni mtoto mdogo akililia kuongezewa hela na mama/dada yake kisa tu mdogo/mkubwa wake kapewa zaidi yake.
 
Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla, (CCM), leo anatarajiwa kuanza kukusanya saini za wabunge akitafuta kuungwa mkono katika hoja ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa madai kwamba amekuwa akikiuka kanuni za Bunge.

Dk Kigwangalla aliibua hoja ya kutokuwa na imani na Spika katika kikao cha wabunge wote cha kuelezea shughuli zitakazofanywa na Bunge katika mkutano wa 13, kilichofanyika juzi jioni kwenye ukumbi wa Pius Msekwa.

Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, jana alithibitisha kuwapo kwa mjadala huo katika kikao cha wabunge, lakini hakuwa tayari kueleza kwa undani na badala yake alisema kwamba leo ataanza kukusanya saini za wabunge kwa ajili ya kukamilisha hoja ya kutokuwa na imani na Spika Makinda.

Chanzo chetu kutoka katika kikao hicho cha wabunge kilibainisha kuwa Kigwangalla alihoji kuhusiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge (CCM-Bariadi Magharibi) kuteuliwa na Spika wakati katika kamati nyingine wenyeviti na makamu huchaguliwa na wajumbe wa kamati husika.

Pia Dk Kigwangala alisema Spika Makinda alivunja kanuni kwa kuwapa posho ya Sh430,000 kwa siku wajumbe wa kamati inayoongozwa na Chenge wakati wajumbe wa kamati nyingine wamekuwa wakipewa Sh130,000.

Anachokifanya Spika ni matumizi mabaya ya fedha za umma, inakuwaje wengine wafanye kazi hata bila posho lakini wao (Kamati ya Bajeti), walipwe posho ya Sh430,000 kwa siku?" chanzo hicho kilimkariri Dk Kigwangalla akihoji. Hata hivyo, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah akizungumza na gazeti hili jana alisema mazingira ya kamati fulani kupata malipo ya ziada tofauti na viwango vya kawaida hutokea pale uongozi wa kamati husika unapoomba kwa Spika.

"Si kweli kwamba Kamati ya Bajeti inalipwa fedha za ziada kila wakati, hapana, ni pale tu wanapoomba malipo hayo kutokana na sababu ambazo lazima Spika aridhike nazo. Ieleweke kuwa siyo kamati hiyo tu, kwa sasa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ambayo inachambua miswada mingi nayo imekuwa ikiomba na baada ya Spika kuridhia basi nao wanapewa," alisema Dk Kashililah.

Katibu huyo wa Bunge alieleza kuwa zaidi ya kamati nane zimewahi kuomba malipo ya ziada kwa maana ya kutaka posho zaidi, ulinzi, usafiri na hata chakula, ikiwa zinakabiliwa na majukumu ya ziada pia katika mazingira tofauti nje ya utaratibu wa kawaida.

"Kimsingi, kamati nyingi zinapewa malipo tofauti, watu wanaweza kuwa na kazi mpaka saa saba au nane usiku, au wanakwenda kufanya kazi katika mazingira yasiyokuwa ya kawaida, taratibu zinamruhusu Spika kama akiridhika na maelezo ya kazi husika, basi anaruhusu kutekelezwa kwa maombi hayo," alisema Dk Kashililah.

Kuhusu Serukamba

Aidha, Dk Kigwangalla alinukuliwa akisema Spika amekiuka kanuni kwa kumchagua Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Peter Serukamba (Kigoma Mjini-CCM), kuwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti.

"Hakuna mbunge yeyote aliyepo katika kamati mbili lakini hata kungekuwa na sababu maalumu basi wa kuteuliwa angekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Mahmoud Mgimwa (Mufindi Kaskazini-CCM) ambaye TRA (Mamlaka ya Mapato Nchini) ipo chini ya kamati yake," kilisema chanzo hicho.


nimependa signature yako tu..
 
Hana lolote huyo.. Anatafuta umaarufu! Kwani hakumbukwi

Hili ndo tatizo kubwa la kuwa mnafiki mkuu. HK kasahu kuwa, ni yeye pia ambae huwa anaongea utumbo na kushabikia mambo ya kipuuzi bungeni kisa tu, kiti au CCM inashambuliwa, leo ndo anajifanya kuona hayo madudu
 
Back
Top Bottom