Saikolojia: Makundi manne ya watu katika mapenzi

Saikolojia: Makundi manne ya watu katika mapenzi

Waswahili tunawajua ao introvert km watu
Wanaoringa
Wanajiskia
Wanajivuna nk


Uswazi raha sana
 
Ni sawa na kuubadili ubongo!
Kuhama kundi ni kazi sana tena sana maana hizo ni tabia it's like your coded!!

Mtu anaweza kubadili baadhi ya tabia kundi utahangaika sana Tena Sana.. hebu niambie mtu kama Sanguine na machepele yake atapendaje kuwa phlegmatic au melancholic..?
sio kwa muda mfupi, ni kitendo cha muda mrefu....
 
Ambivert + Introvert = The best combination. Pia kwa sababu ya ku'boost' IQ ya kizazi cha baadaye.

Extrovert wanaelewana wenyewe tu hao. Kama wewe ni Introvert, kwao ni kutafuta mateso tu.
Otherwise, for biological reasons.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyongeza.

Mazingira hurahisisha zaidi kumtambulisha mtu tabia ya kundi lake kwa urahisi hasa makundi ya Extrovert.

Kuna wengine wanahitaji zaidi muda na kushirikiana naye ili kumjua undani wake.
Mtu huonyesha tabia alizonazo kutokana na mazingira kuna tabia mtu atazionyesha mbele ya watu na nyengine nje na pale.. itategemea na kundi lake

Hata wewe ukiwa ugenini kuna vitu hutavionyesha mpk uzoee anaeweza hayo ni Sanguine muda mchache tu mwenzio ameshaunda urafiki na watu shazi mitaa anaijua yote! N.k

Mazingira yanatoa msimamo mkubwa ktk tabia za watu kuanzia malezi,hali za hewa,sheria au utamaduni wa watu husika n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu KENZY
Kuna hoja mbili zimekuja na mifano. Mmoja anataka kujua kama inawezekana kuhama kundi au kuwa na sifa za kundi zaidi ya moja.

Nadhani Psychology ina upana wake. Lakini nitatoa mfano(kama utafaa nitafurahi).
Kuna watoto wanapata malezi ambayo siyo sahihi hasa chini ya miaka 7. Hali hii huwafanya waathirike kisaikolojia hivyo kufanya waoneshe tabia ambazo si sahihi kwao wala asili yao.

Unaweza kukuta mtoto ni mkimya sana, si kwa sababu ni Introvert, bali athari ya makuzi iliyopelekea kutojiamini na kuwa mkimya.
Ukimpima kwa vigezo vingine utagundua kuwa ile si tabia yake halisi.

Kwa wale wenye tabia za kundi zaidi ya moja ni sahihi lakini siyo rahisi kuhama kundi(kwa utashi).

Itoshe tu kusema mazingira, elimu, imani/itikadi, mila & desturi, muingiliano n.k. vinamchango mkubwa katika Psychology ya mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akikujibu nitag, sometimes nahisi mie ni extrovert lakini sipendi interaction..muda mwingi napendelea niwe mwenyewe na siku ikatokea nikachangamana Niko very charming, namake friends easily, nina hasira za karibu. Nk

Mimi nina hasira za mbali sana...

Naomba hasira zako uwe unazimalizia kwangu... 😷


Cc: mahondaw
 
Cjui nipo wap

Its not over until its over...[emoji769]
Kama utakuwa huru andika hapa tabia zako,vitu unavyopenda kufanya ambavyo hupendi..
Kama haupo huru si lazima au kama vipi pm ipo..!
 
Hizi habari huwa zinachanganya sana mfano mimi si mpole ila naambiwa naonekana mpole sasa sijui ndio sijijui au hawanijui.

Hii imekaa vipi mkuu?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hizi habari huwa zinachanganya sana mfano mimi si mpole ila naambiwa naonekana mpole sasa sijui ndio sijijui au hawanijui.

Hii imekaa vipi mkuu?


Sent from my iPhone using JamiiForums
Ha ha!
Mkuu nafikiri itakuwa wanamaanisha muonekano wako I mean sura yako na pozi your all body umekaa kipolepole.. ila kitabia nadhani ndo hivyo unavyojiona mkali..
 
Hizi habari huwa zinachanganya sana mfano mimi si mpole ila naambiwa naonekana mpole sasa sijui ndio sijijui au hawanijui.

Hii imekaa vipi mkuu?


Sent from my iPhone using JamiiForums

Hii ni personality/characteristic na huendana na nyota.

Nyota inabeba tabia, zinazooneka na zisizoonekana.
Tabia huonekana kwa Maneno, matendo na Haiba.

Na hizo sio ndio tabia zako kwenye Mapenzi.

Ndio maana nina amini Tabia za Mapenzi sio rahisi kama Mtoa mada alivyoandika.




Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Umesahau makundi mawili muhimu sana


Empaths & narcissistic..

Hawa empaths ni gifted people.They have ability to smell/feel people/things

Hawa narcissistic ni opposite ya hawa empaths,very self centred.

Empaths sifa zao ni
1.Ana hisia sana
Akiona ajali siku nzima anakuwa nje ya mood,akiona mgonjwa roho inamuuma kama anaumwa yeye.sa nyingine anapata maumivu ya mpenzi wake mwilini mwake
2.Ana machale
Anaweza kumuangalia mtu nakujua huyu mtu ni mbaya au mwema bila kusikia lolote
3.Ana mood changes
Anafyonza hisia za watu hivo mood yake inabadilika sana anaweza kuwa na furaha mara huzuni bila kujua nini sababu
4.anahitaji mda wa kukaa mwenyewe kujirefresh
Hapendi maeneo yenye kelele sana na msongamano,mataa taa.
5.anapenda kusaidia watu automatic tu na watu wanamfuata sana wakiwa na shida.
6.anapenda mambo ya kiroho
7.mshauri mzuri sababu anawajua watu zaidi ya wanavyojijua.
8.Anahisi km hakutakiwa kuwa dunia hii
9.Penda sana wanyama na huruma nyingi
10.shy kidogo
11.Ndoto za kweli

Narcissistic ni kinyume ya hao
1.hana huruma
2.anajiwazia mwenyewe tu
3.anataka asaidiwe yeye tu
4anatumia ucheshi kupata anachokitaka na kukandamiza wengine
5.anakufanya ujisikie huna thamani ili akutawale
6Anakupenda km una manufaa kwake km huna anatema.
7mbinfsi

Empaths are 10% of population,very gifted ila kama hujui kuwa wewe ni empaths utahisi km umelaaniwa,You will smell people na hutataka kuwanao karibu sababu unawaona deep down jinsi walivyo dhaifu..
 
Umesahau makundi mawili muhimu sana


Empaths & narcissistic..

Hawa empaths ni gifted people.They have ability to smell/feel people/things

Hawa narcissistic ni opposite ya hawa empaths,very self centred.

Empaths sifa zao ni
1.Ana hisia sana
Akiona ajali siku nzima anakuwa nje ya mood,akiona mgonjwa roho inamuuma kama anaumwa yeye.sa nyingine anapata maumivu ya mpenzi wake mwilini mwake
2.Ana machale
Anaweza kumuangalia mtu nakujua huyu mtu ni mbaya au mwema bila kusikia lolote
3.Ana mood changes
Anafyonza hisia za watu hivo mood yake inabadilika sana anaweza kuwa na furaha mara huzuni bila kujua nini sababu
4.anahitaji mda wa kukaa mwenyewe kujirefresh
Hapendi maeneo yenye kelele sana na msongamano,mataa taa.
5.anapenda kusaidia watu automatic tu na watu wanamfuata sana wakiwa na shida.
6.anapenda mambo ya kiroho
7.mshauri mzuri sababu anawajua watu zaidi ya wanavyojijua.
8.Anahisi km hakutakiwa kuwa dunia hii
9.Penda sana wanyama na huruma nyingi
10.shy kidogo
11.Ndoto za kweli

Narcissistic ni kinyume ya hao
1.hana huruma
2.anajiwazia mwenyewe tu
3.anataka asaidiwe yeye tu
4anatumia ucheshi kupata anachokitaka na kukandamiza wengine
5.anakufanya ujisikie huna thamani ili akutawale
6Anakupenda km una manufaa kwake km huna anatema.
7mbinfsi

Empaths are 10% of population,very gifted ila kama hujui kuwa wewe ni empaths utahisi km umelaaniwa,You will smell people na hutataka kuwanao karibu sababu unawaona deep down jinsi walivyo dhaifu..
Tukisema tuchambue makundi mengi ya watu utawachanganya maana yanafika hadi 8 na hata 16!.. saikolojia ni pana ndio maana kiujumla nikaona nizungumzie hayo manne na hapo Kuna wengine bado nimewachanganya..

Binadamu ni kama kitabu kikubwa mno ambacho kila siku kurasa zinaongezeka!.
 
Somo la saikolojia ni pana kama zilivyo pana tabia za viumbe husika hivyo upana wa somo hili la saikolojia inatokana na upana wa kitabia tulionao.

Ningependa kugusia makundi manne ya watu haswa katika mapenzi. Tabia zetu moja kwa moja huathiri vitu mbalimbali ktk maisha yetu,ila tu itategemea kuathiri huko kutakuwaje kutokana na tabia zetu..

Hakuna asiyefahamu nguvu ya mapenzi ktk maisha yetu. Wengi wameshanena mengi juu ya mapenzi na kila mtu na mtazamo wake.

Kwa uchache ktk mengi nitaandika nijuavyo namna makundi haya manne ya watu namna tabia zinavyoweza kuathiri sekta ya mahaba..

Kwanza kwa wasiofahamu nitaandika kiufupi kuhusu makundi haya ili walau mtu upate picha ya kile ninachoandika. Wataalum waligawa kwanza makundi mawili ya kisaikolojia ambayo ni Introvert na extrovert.

Introvert ni aina ya watu ambao wapo na haya (aibu), hupenda kukaa pekee na ni watu wenye taratibu wasiopenda kujiongezea n.k kimsingi waweza sema ni watu wenye hisia za ndani.

Katika introvert kuna makundi mawili ndani yake ambayo ni Phlegmatic na Melancholic. Nitagusia sifa zao kwa uchache kama ili tuweze kuelewana Ila sifa nilizozitaja ktk introvert ni sifa zao kiujumla ndio maana wanatoka kundi moja.

MELANCHOLIC
Kwanza ktk makundi yote hawa kiakili wapo juu!
Wana uweza mpana wa kufikiri na kutoka na majibu..
Ni aina fulani ya watu ambao ili kufanya kitu atahitaji mpangilio wenye uhakika (perfect).
Hawa ni watu wanaoishi kwa logic.. humbebi tu na kumtendesha kitu bila kukuuliza kwanini..?
Kivipi..?
Wapi..?
Itakuwaje..?
Kiufupi wanataka kujua kiundani..
Ni watu wenye kujitenga na watu.
Wapole na wataratibu ktk utendaji wao hawataki kukosea.
Hupendelea mazungumzo mapana yenye kutafakarisha Sana..
Hizo ni baadhi ya sifa zao ila zipo nyingi mno.

PHLEGMATIC
Hawa kiakili hufuata wenyewe baada ya melancholic..
Hupenda kujenga hoja na wanaweza kukushika vizuri tu kwa hoja zao!.
Wana tafakari nzuri pia..
Wapole tena upole wao unaweza ita upole wa kijinga Ila wao wanakuchora tu😅
Hawajali Sana ndio maana wanasamehe haraka tofauti na melancholic wao wanaweza samehe ila bado akabaki nalo ndani lamkereketa!.
Wepesi kuhairisha Jambo!
Sio watendaji wazuri!.
Wanapenda Sana amani,wapo radhi wakose vitu Ila wapate amani.. na hilo huwafanya kuwa wazuri ktk usuruhishi wa migogoro hasa kidiplomasia.
Wao ni kaa mezani tuyamalize na yupo radhi ile kwake lkn suruhu ipatikane..
Kwa maana nyengine ni waoga panapotokea ugomvi na kama asiposuruhisha yakimshinda hula kona moja mbaya😅
Sifa ni nyingi ila tuishie hapo kidogo..

Kwenye upande wa Extrovert napo kuna makundi mawili ambayo ni Sanguine na Choleric..
Kiufupi ni kuwa introvert ni kinyume cha extrovert!
Hapa sifa utakazo kutananazo ni kinyume cha hayo makundi mawili niliyoyaandika hapo juu..
Kwanza kiujumla extrovert hawana aibu,si watu wa kujitenga ni social na friendly kabisa..

CHOLERIC
Hawa kiakili pamoja na wenzao Sanguine ni za wastani japo muda mwengine ukikuta aliekengeuka unakuta ni tabu kwelikweli 😅
Choleric wapo taff sana,Hawa hawana huruma!
Sio watu wa kudekeza!
Hawapendi uvivu ni watu wa kujituma sana na hii hupelekea kuwa watu wenye mafanikio makubwa.
Wanapenda kuongoza Ila ndo vile kuongoza kwao lazima waongoze kwa mabavu au ukali,hawana macheko kazini wenyewe ni kazi kazi!.
Naomba kwa hawa niongelee hili la uongozi..
Kama nilivyoandika ni watu wenye kupenda kuongoza na huongoza kwa ukali.. nitanukuu kipande hiki kutoka kwa mwanasaikolojia Marehemu mitimingi (RIP)
Choleric wapo hivi ni "UMPISHE APITE AU AKUKANYAGE!"
Na hivyo ndivyo walivyo!! Wewe ukiwa mkaidi kwake utaumia bure maana wenyewe wanachoangalia ni mafanikio Yao tu..

Ni viongozi wazuri haswa ukimuweka aongoze sehemu ambapo hapataki masihara!..
Wanafaa sana kuongoza sehemu ngumu ila mnaweza angamia kutokana na madhaifu yao kiuongozi!!
Ukitaka uweke korabo nzuri kwenye uongozi mchanganye yeye na melancholic,kwa maana melancholic wanatafakari nzuri zaidi lkn kitakacho kukosti ni muda maana kufikiri kunahitaji muda..
Kwa maana nyengine Choleric ni watendaji wazuri ndio maana anaweza patiwa project ambayo imeshaandaliwa vizuri ye atatenda na mtaona mafanikio tena makubwa.. ila melancholic ye anaweza andika na likaishia hapohapo kwenye karatasi😎
Ni hivyo tu kwa ufupi..

SANGUINE
Hawa pia kiakili wapo wastani Ila kwangu ndio moja ya kundi la watu ambao naweza kuwatambua ndani ya muda mchache Sana!.
Sifa zao ni hawana shipa la aibu😅
Wapo social Sana..
Hupenda kuonekana..
Hawana mipangilio maalum..
Huzoeana na watu ndani ya muda mfupi sana..
Wanapenda kuwachekesha.. hawa unawezakuta wamekusanya kundi la watu na wanasikilizwa hata kama hawaongei cha maana Ila mtakaa tu😅
Kwa maana hiyo ni washawishi wazuri sana..
Wana hasira za papo kwa papo na akisha malizana na wewe yamekwisha sio kama Choleric lazima afahamike mbabe Nani😅
hawa hawawezi kukaa sehemu moja wakatulia!.
Wapo rafu ila wanapendeka Sana na wanamaneno mengi mno..
Usiombe hili kundi awe me au ke akutongoze utasifiwa na watakujaza maneno ila Sasa wakatae utasuntwa,utatukanwa zile sifa zote alizokuwa akikuambia zitaisha punde hiyohiyo utasikia tu toka na likibamia lako😂😅
(Joke kidogo)

Hawa hawana shipa la kutunza siri hivyo jitahidi kutunza siri zako usiwaambie.. ukiwaambia jua umekiambia chombo cha habari!
Kikipewa hata bia tu siri zote nje😂😅
Ndio kundi linaloongoza kuwa na watu wengi ktk jamii, I mean Sanguine ni wengi sana ktk jamii ukilinganisha na wengine..

Tuingie katika mapenzi na hayo makundi manne ya watu na humu tutakuta sifa nyengine ambazo sijaziandika..

Kitaalum inashauliwa hayo makundi yachukuane kutokana na sifa zao,ili kuweza kubalance mambo.. ili kuepuka migogoro isiyolazima ni vyema kuelewana ili kuleta uwiano stahiki..

Nini kama introvert kwa introvert wakiwa ktk mapenzi..?
Hapo ni sawa na kusema 0 + 0 sawasawa na zero!
Ila hii sio kanuni tuelewane hapo,si lazima ukiwa kundi fulani uchukuane na kundi fulani ila inashauliwa tu.

Naomba nianzie hapa
MELANCHOLIC inashauliwa aoane na SANGUINE kwa maana hii kila mmoja ataziba pengo la mwengine..
Mfano: Sanguine hawana mpangilio wa vitu ila melancholic wanampangilio wa vitu.. huyu akivuruga huyu anapanga
Sanguine huwa rafu akiamka hatandiki kitandani,hana mpangilio wa vitu nguo chafu zipo na nguo Safi n.k hivyo melancholic huziba hayo..
Pia melancholic si social sana ila sanguine ni social hivyo ataweza muwakilisha mwenzake vilivyo..
Pia inaleta uwiano wa kutegemeana ktk ufanyaji wa Jambo fulani n.k
Sanguine unaweza ukamuinua na ukampeleka huko na huko ila melancholic ni lazima uwe na sababu so ktk namna hii inaweza msaidia hata Sanguine Kama akiwa na melancholic...
Mambo ni mengi mengine tutajadili..

Pia vilevile unashauliwa CHOLERIC aoane na PHLEGMATIC..
Choleric ni taff so wakipata mtu taff hawataendana maana hilo litakuwa kama pambano la kutoana minundu😜
Hivyo Phlegmatic ndio udhaifu wa Choleric!
Ni wapole hivyo watakuwa watiifu na wanyenyekevu! Pia hii itasaidia muda mwengine kwa chorelic kutoingia kwenye ugomvi kwa maasa ya Phlegmatic..
Hii couple mnyonge ni Phlegmatic na sio kwamba anaonewa ila ni vile tu yeye anauwezo wa kuhimili mikikimikiki ya Choleric..
Phlegmatic anaweza karipiwa na asijibu huo uboya wake ndio utimilifu wake kwa maana hauwezi ukauona wa maana mpaka siku aondoke Kisha ukutane na mtu mwenye kukujibu vile atakavyo...
Hii couple pia ikiwa mke ndo Choleric na mume ni Phlegmatic hapa wanajamii ndo huita mume katiwa limbwata😅
Kwa maana mke ndo huwa Kama kichwa cha familia kila kitu kinaongozwa nae.. hapa hata mume akipata mshahara wote huweza kuupeleka nyumbani na mke ndo hupanga matumizi!!
Familia ya namna hii hupata mafanikio kwasababu ya uongozi wa Choleric na wenyewe ndani huelewana vizuri japo unaweza ona mmoja Kama anaonewa!!

Shughuli pevu ipo waoane Sanguine to Sanguine 😅
Hiyo couple kila siku majirani mtaamua ugomvi🤣
Hizo raia hudundana kinoma!
Mapenzi yao huwa Moto baridi Moto baridi maana kila mtu mjuaji!..
Kila mtu mission town na mjuzi..
Hawa huumuana minundu usiku na asubuhi wanakandana!😅

Naomba niishie hapo mengine mjadala utaendelea...

Karibuni..
Hakika
 
Back
Top Bottom