Saikolojia: Makundi manne ya watu katika mapenzi

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,171
56,754
Somo la saikolojia ni pana kama zilivyo pana tabia za viumbe husika hivyo upana wa somo hili la saikolojia inatokana na upana wa kitabia tulionao.

Ningependa kugusia makundi manne ya watu haswa katika mapenzi. Tabia zetu moja kwa moja huathiri vitu mbalimbali ktk maisha yetu,ila tu itategemea kuathiri huko kutakuwaje kutokana na tabia zetu..

Hakuna asiyefahamu nguvu ya mapenzi ktk maisha yetu. Wengi wameshanena mengi juu ya mapenzi na kila mtu na mtazamo wake.

Kwa uchache ktk mengi nitaandika nijuavyo namna makundi haya manne ya watu namna tabia zinavyoweza kuathiri sekta ya mahaba..

Kwanza kwa wasiofahamu nitaandika kiufupi kuhusu makundi haya ili walau mtu upate picha ya kile ninachoandika. Wataalum waligawa kwanza makundi mawili ya kisaikolojia ambayo ni Introvert na extrovert.

Introvert ni aina ya watu ambao wapo na haya (aibu), hupenda kukaa pekee na ni watu wenye taratibu wasiopenda kujiongezea n.k kimsingi waweza sema ni watu wenye hisia za ndani.

Katika introvert kuna makundi mawili ndani yake ambayo ni Phlegmatic na Melancholic. Nitagusia sifa zao kwa uchache kama ili tuweze kuelewana Ila sifa nilizozitaja ktk introvert ni sifa zao kiujumla ndio maana wanatoka kundi moja.

MELANCHOLIC
Kwanza ktk makundi yote hawa kiakili wapo juu!
Wana uweza mpana wa kufikiri na kutoka na majibu..
Ni aina fulani ya watu ambao ili kufanya kitu atahitaji mpangilio wenye uhakika (perfect).
Hawa ni watu wanaoishi kwa logic.. humbebi tu na kumtendesha kitu bila kukuuliza kwanini..?
Kivipi..?
Wapi..?
Itakuwaje..?
Kiufupi wanataka kujua kiundani..
Ni watu wenye kujitenga na watu.
Wapole na wataratibu ktk utendaji wao hawataki kukosea.
Hupendelea mazungumzo mapana yenye kutafakarisha Sana..
Hizo ni baadhi ya sifa zao ila zipo nyingi mno.

PHLEGMATIC
Hawa kiakili hufuata wenyewe baada ya melancholic..
Hupenda kujenga hoja na wanaweza kukushika vizuri tu kwa hoja zao!.
Wana tafakari nzuri pia..
Wapole tena upole wao unaweza ita upole wa kijinga Ila wao wanakuchora tu😅
Hawajali Sana ndio maana wanasamehe haraka tofauti na melancholic wao wanaweza samehe ila bado akabaki nalo ndani lamkereketa!.
Wepesi kuhairisha Jambo!
Sio watendaji wazuri!.
Wanapenda Sana amani,wapo radhi wakose vitu Ila wapate amani.. na hilo huwafanya kuwa wazuri ktk usuruhishi wa migogoro hasa kidiplomasia.
Wao ni kaa mezani tuyamalize na yupo radhi ile kwake lkn suruhu ipatikane..
Kwa maana nyengine ni waoga panapotokea ugomvi na kama asiposuruhisha yakimshinda hula kona moja mbaya😅
Sifa ni nyingi ila tuishie hapo kidogo..

Kwenye upande wa Extrovert napo kuna makundi mawili ambayo ni Sanguine na Choleric..
Kiufupi ni kuwa introvert ni kinyume cha extrovert!
Hapa sifa utakazo kutananazo ni kinyume cha hayo makundi mawili niliyoyaandika hapo juu..
Kwanza kiujumla extrovert hawana aibu,si watu wa kujitenga ni social na friendly kabisa..

CHOLERIC
Hawa kiakili pamoja na wenzao Sanguine ni za wastani japo muda mwengine ukikuta aliekengeuka unakuta ni tabu kwelikweli 😅
Choleric wapo taff sana,Hawa hawana huruma!
Sio watu wa kudekeza!
Hawapendi uvivu ni watu wa kujituma sana na hii hupelekea kuwa watu wenye mafanikio makubwa.
Wanapenda kuongoza Ila ndo vile kuongoza kwao lazima waongoze kwa mabavu au ukali,hawana macheko kazini wenyewe ni kazi kazi!.
Naomba kwa hawa niongelee hili la uongozi..
Kama nilivyoandika ni watu wenye kupenda kuongoza na huongoza kwa ukali.. nitanukuu kipande hiki kutoka kwa mwanasaikolojia Marehemu mitimingi (RIP)
Choleric wapo hivi ni "UMPISHE APITE AU AKUKANYAGE!"
Na hivyo ndivyo walivyo!! Wewe ukiwa mkaidi kwake utaumia bure maana wenyewe wanachoangalia ni mafanikio Yao tu..

Ni viongozi wazuri haswa ukimuweka aongoze sehemu ambapo hapataki masihara!..
Wanafaa sana kuongoza sehemu ngumu ila mnaweza angamia kutokana na madhaifu yao kiuongozi!!
Ukitaka uweke korabo nzuri kwenye uongozi mchanganye yeye na melancholic,kwa maana melancholic wanatafakari nzuri zaidi lkn kitakacho kukosti ni muda maana kufikiri kunahitaji muda..
Kwa maana nyengine Choleric ni watendaji wazuri ndio maana anaweza patiwa project ambayo imeshaandaliwa vizuri ye atatenda na mtaona mafanikio tena makubwa.. ila melancholic ye anaweza andika na likaishia hapohapo kwenye karatasi😎
Ni hivyo tu kwa ufupi..

SANGUINE
Hawa pia kiakili wapo wastani Ila kwangu ndio moja ya kundi la watu ambao naweza kuwatambua ndani ya muda mchache Sana!.
Sifa zao ni hawana shipa la aibu😅
Wapo social Sana..
Hupenda kuonekana..
Hawana mipangilio maalum..
Huzoeana na watu ndani ya muda mfupi sana..
Wanapenda kuwachekesha.. hawa unawezakuta wamekusanya kundi la watu na wanasikilizwa hata kama hawaongei cha maana Ila mtakaa tu😅
Kwa maana hiyo ni washawishi wazuri sana..
Wana hasira za papo kwa papo na akisha malizana na wewe yamekwisha sio kama Choleric lazima afahamike mbabe Nani😅
hawa hawawezi kukaa sehemu moja wakatulia!.
Wapo rafu ila wanapendeka Sana na wanamaneno mengi mno..
Usiombe hili kundi awe me au ke akutongoze utasifiwa na watakujaza maneno ila Sasa wakatae utasuntwa,utatukanwa zile sifa zote alizokuwa akikuambia zitaisha punde hiyohiyo utasikia tu toka na likibamia lako😂😅
(Joke kidogo)

Hawa hawana shipa la kutunza siri hivyo jitahidi kutunza siri zako usiwaambie.. ukiwaambia jua umekiambia chombo cha habari!
Kikipewa hata bia tu siri zote nje😂😅
Ndio kundi linaloongoza kuwa na watu wengi ktk jamii, I mean Sanguine ni wengi sana ktk jamii ukilinganisha na wengine..

Tuingie katika mapenzi na hayo makundi manne ya watu na humu tutakuta sifa nyengine ambazo sijaziandika..

Kitaalum inashauliwa hayo makundi yachukuane kutokana na sifa zao,ili kuweza kubalance mambo.. ili kuepuka migogoro isiyolazima ni vyema kuelewana ili kuleta uwiano stahiki..

Nini kama introvert kwa introvert wakiwa ktk mapenzi..?
Hapo ni sawa na kusema 0 + 0 sawasawa na zero!
Ila hii sio kanuni tuelewane hapo,si lazima ukiwa kundi fulani uchukuane na kundi fulani ila inashauliwa tu.

Naomba nianzie hapa
MELANCHOLIC inashauliwa aoane na SANGUINE kwa maana hii kila mmoja ataziba pengo la mwengine..
Mfano: Sanguine hawana mpangilio wa vitu ila melancholic wanampangilio wa vitu.. huyu akivuruga huyu anapanga
Sanguine huwa rafu akiamka hatandiki kitandani,hana mpangilio wa vitu nguo chafu zipo na nguo Safi n.k hivyo melancholic huziba hayo..
Pia melancholic si social sana ila sanguine ni social hivyo ataweza muwakilisha mwenzake vilivyo..
Pia inaleta uwiano wa kutegemeana ktk ufanyaji wa Jambo fulani n.k
Sanguine unaweza ukamuinua na ukampeleka huko na huko ila melancholic ni lazima uwe na sababu so ktk namna hii inaweza msaidia hata Sanguine Kama akiwa na melancholic...
Mambo ni mengi mengine tutajadili..

Pia vilevile unashauliwa CHOLERIC aoane na PHLEGMATIC..
Choleric ni taff so wakipata mtu taff hawataendana maana hilo litakuwa kama pambano la kutoana minundu😜
Hivyo Phlegmatic ndio udhaifu wa Choleric!
Ni wapole hivyo watakuwa watiifu na wanyenyekevu! Pia hii itasaidia muda mwengine kwa chorelic kutoingia kwenye ugomvi kwa maasa ya Phlegmatic..
Hii couple mnyonge ni Phlegmatic na sio kwamba anaonewa ila ni vile tu yeye anauwezo wa kuhimili mikikimikiki ya Choleric..
Phlegmatic anaweza karipiwa na asijibu huo uboya wake ndio utimilifu wake kwa maana hauwezi ukauona wa maana mpaka siku aondoke Kisha ukutane na mtu mwenye kukujibu vile atakavyo...
Hii couple pia ikiwa mke ndo Choleric na mume ni Phlegmatic hapa wanajamii ndo huita mume katiwa limbwata😅
Kwa maana mke ndo huwa Kama kichwa cha familia kila kitu kinaongozwa nae.. hapa hata mume akipata mshahara wote huweza kuupeleka nyumbani na mke ndo hupanga matumizi!!
Familia ya namna hii hupata mafanikio kwasababu ya uongozi wa Choleric na wenyewe ndani huelewana vizuri japo unaweza ona mmoja Kama anaonewa!!

Shughuli pevu ipo waoane Sanguine to Sanguine 😅
Hiyo couple kila siku majirani mtaamua ugomvi🤣
Hizo raia hudundana kinoma!
Mapenzi yao huwa Moto baridi Moto baridi maana kila mtu mjuaji!..
Kila mtu mission town na mjuzi..
Hawa huumuana minundu usiku na asubuhi wanakandana!😅

Naomba niishie hapo mengine mjadala utaendelea...

Karibuni..
 
Somo zuri sana ningependa kujua upo kundi gani ndugu mwandishi
 
Ss kuna wenye tabia aina zote 4 ushauri kwao tafadhali

Hiyo mixing sijawahi iona. Kwakuwa nimeelezea kwa uchache ndio maana unaona hivyo.

Tayari umeshaanza kuangalia tabia za watu ninavyofahamu mtu anaweza mix tabia za makundi mawili wapo wengi wanaitwa Ambivert,lkn ukimchunguza vizuri utakuta kundi fulani ndio lipo juu zaidi ya sifa za kundi jengine alilonalo..
Umeziangalia harakaharaka ndio maana unaona hayo.

Mtu pia tabia huchagizwa na eneo pia hivyo ni vyema kuwa makini ktk kuchambua.. kundi jepesi kuwahi kulijua ni Sanguine na Choleric
 
Kwahyo huko kubadilika kutokana na mazingira hakupelekei mtu kuonesha tabia zote kwa vipindi tofauti?!
Mtu huonyesha tabia alizonazo kutokana na mazingira kuna tabia mtu atazionyesha mbele ya watu na nyengine nje na pale.. itategemea na kundi lake

Hata wewe ukiwa ugenini kuna vitu hutavionyesha mpk uzoee anaeweza hayo ni Sanguine muda mchache tu mwenzio ameshaunda urafiki na watu shazi mitaa anaijua yote! N.k

Mazingira yanatoa msimamo mkubwa ktk tabia za watu kuanzia malezi,hali za hewa,sheria au utamaduni wa watu husika n.k
 
We ndo upo pande zipi?....mana kila kundi kuna ka behaviour lazima utakuwa nako
Itakuchukua muda kujijua Anza taratibu anzia kwenye general kati ya introvert na extrovert ndo uje kwengine..
 
somo zuri Sana ningependa kujua upo kundi gani ndugu mwandishi
Elimu inakupa njia ya kutafuta majibu!
Tumia hayo nilioandika kunijua kundi langu!.. huwa ni ngumu sana kumuambia mtu kundi alilopo hata kama namjua ndio ila simwambii!! mimi pia siwezi jibainusha.
 
Elimu inakupa njia ya kutafuta majibu!
Tumia hayo nilioandika kunijua kundi langu!.. huwa ni ngumu sana kumuambia mtu kundi alilopo hata kama namjua ndio ila simwambii!! mimi pia siwezi jibainusha.
sawa
 

Swala la Introverts na Extroverts, Sijazielewa vizuri Bado

I'm on that good kush and alcohol
Introvert na extrovert ndio makundi ya awali yanayoelezea mgawanyo wa tabia mbalimbali tulizonazo na ktk hayo makundi ndani yake kuna makundi tena mawilimawili...

Ipo hivi ktk introvert kuna kundi la melancholic na phlegmatic kuwa hivi inamaana haya makundi mawili yaliyomo ktk introvert kuna tabia wanalandana ndio maana wapo kundi moja ambapo sifa zao kiujumla ktk kundi la introvert ni hizi..
Ni watu ambao hawapo social,hawapendi kujichanganya na watu kwani wanaaibu sana!.
Ni watu wapole na wataratibu..
Mara nyingi huwa si waongeaji mpk wakuzoee vilivyo..
Hupenda mambo ya kutafakarisha sana I mean introvert wana peo nzuri za kufikiri.
Hizo ni baadhi ya sifa za introvert Sasa pia ktk makundi yao hayo mawili kuna sifa tofauti kwa maana ya hata kama wanatoka kundi moja la introvert ila kuna vitu vichache wanatofautiana...

Vivyohivyo hata ktk extrovert kuna makundi mawili ambayo ni Sanguine na choleric.. sifa zao kiujumla yani Kama extrovert ni kinyume cha introvert ila sio kila kitu..
Hawa hawana haya kama introvert..
Wapo social sana..
Ni wachangamfu tofauti na introvert
Kiakili wapo wastani.. sanasana hawapendi kufikiria I mean wavivu kufikiri!
Hayo ni kwa uchache nafikiri umepata kitu kidogo..

Nikuibie siri kidogo muda mwengine unaweza kumjua mtu kundi lake hata namna ya uandishi wake au ongea yake ila mpk uwe unafahamu vizuri..
Kuna baadhi ya maneno watu wa kundi fulani hupenda kuyatumia!! Na hii inatokea tu sio kwamba mtu anapenda..

Ukiweza kulijua hilo utaweza hata kuubaini uandishi wangu ni kutoka kundi lipi..!!
 
Introvert na extrovert ndio makundi ya awali yanayoelezea mgawanyo wa tabia mbalimbali tulizonazo na ktk hayo makundi ndani yake kuna makundi tena mawilimawili...

Ipo hivi ktk introvert kuna kundi la melancholic na phlegmatic kuwa hivi inamaana haya makundi mawili yaliyomo ktk introvert kuna tabia wanalandana ndio maana wapo kundi moja ambapo sifa zao kiujumla ktk kundi la introvert ni hizi..
Ni watu ambao hawapo social,hawapendi kujichanganya na watu kwani wanaaibu sana!.
Ni watu wapole na wataratibu..
Mara nyingi huwa si waongeaji mpk wakuzoee vilivyo..
Hupenda mambo ya kutafakarisha sana I mean introvert wana peo nzuri za kufikiri.
Hizo ni baadhi ya sifa za introvert Sasa pia ktk makundi yao hayo mawili kuna sifa tofauti kwa maana ya hata kama wanatoka kundi moja la introvert ila kuna vitu vichache wanatofautiana...

Vivyohivyo hata ktk extrovert kuna makundi mawili ambayo ni Sanguine na choleric.. sifa zao kiujumla yani Kama extrovert ni kinyume cha introvert ila sio kila kitu..
Hawa hawana haya kama introvert..
Wapo social sana..
Ni wachangamfu tofauti na introvert
Kiakili wapo wastani.. sanasana hawapendi kufikiria I mean wavivu kufikiri!
Hayo ni kwa uchache nafikiri umepata kitu kidogo..

Nikuibie siri kidogo muda mwengine unaweza kumjua mtu kundi lake hata namna ya uandishi wake au ongea yake ila mpk uwe unafahamu vizuri..
Kuna baadhi ya maneno watu wa kundi fulani hupenda kuyatumia!! Na hii inatokea tu sio kwamba mtu anapenda..

Ukiweza kulijua hilo utaweza hata kuubaini uandishi wangu ni kutoka kundi lipi..!!
Uzi mzuri Sana..nimejifunza kitu kipya....ngoja nikujibu uone ni Kwa kiasi gani nitakuwa nimekuelewa...

Mkuu wewe ni INTROVERT kwenye group la PHLEGMATIC

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom