Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Chama cha Wakulima (AAFP), Said Soud, amesema hakuna chama cha siasa chenye uwezo wa kuiondosha Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani kutokana na uimara na umoja wa chama hicho.
Soud alibainisha kuwa AAFP ipo tayari kushirikiana na CCM na kumuunga mkono mgombea wake wa Urais, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kutokana na rekodi nzuri aliyoionesha katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.
Aidha, mgombea huyo alikitaka chama cha ACT Wazalendo kuacha kuhamasisha fujo kwa kisingizio cha kura ya mapema, akisema kufanya hivyo ni dalili ya uchu wa madaraka.
Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake Mwera, alisema hakuna namna ya kuzuia kura ya mapema kwani jambo hilo lipo kisheria na siyo Zanzibar pekee yenye utaratibu huo.
Soud alimuomba Msajili wa Vyama vya Siasa kufuta usajili wa chama chochote kitakachohamasisha fujo na uvunjifu wa amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu
Soma pia

- GE2025 - Said Soud Said Mgombea Urais AAFP Zanzibar: Nikiwa Rais Vijana watalima bangi na si kuokota Makopo
- GE2025 - CCM imefanya maendeleo makubwa hatuwezi kuiondoa madarakani
- GE2025 - Said Soud: ACT Wazalendo hawana uwezo wa kuitoa CCM Madarakani, hivyo AAFP itakubali kumpa ushirikiano Dk. Hussein
- GE2025 - Said Soud: Nikiwa Rais Vijana wataoa kwa pesa ya serikali