Leo kwenye taarifa ya habari TBC1 (8pm) IGP Said Mwema amesikika akisema kuwa baadhi ya mabalozi wa nchi za nje na wawekezaji wamekuwa wanampigia simu kutokana na kile alichokiita hali ya usalama. According to Mwema 'wapigaji simu' hao wamekuwa wanasema 'tuondoe mali zetu' maana hakuna usalama! Kwa hiyo anakutukumbusha sisi watanzania tudumishe amani ili wawekezaji wasiondoke!
My take: Huu ni upotoshaji wa hali ya juu na madharau makubwa kwa Watanzania kutoka kwa IGP. Hivi huyu Mwema anataka kusema Iraqi kuna usalama zaidi ya Tanzania? anajuwa wawekezaji walioko Iraqi na wamewekeza kiasi gani? Na Afghanistan? Hata hapo Kenya, ambapo yeye Mwema aliwahi kuishi wakati akiwa Interpool, kuna makampuni mangapi ya nje? Hali ya ki-usalama kati ya Kenya na Tanzania ikoje? Ni lini viongozi wa nchi wataacha kuhubiri huu upuuzi na madharau kwa wananchi?
Hawsemi kweli kilichowashinda wawekezaji ni sera ya nchi mbaya kwao, hakuna mazingira ya kuridhisha na serikali yetu imekuwa ya kisanii mno wanaona ni upuuzi kuwekeza hapa, acha waondeke watarudi mambo yakiwa shwari.
Katumwa huyo Mwema na shemeji yake hana lolote
Saidi na wawekezaji inabidi waelewe kuwa mahali ambapo hakuna haki hakuwezi kuwa na amani.
Kama vijana wa Saidi wataendelea na azma yao ya kumaliza stock zilizojazwa kwenye armoury kabla ya uchaguzi nchi haitakuwa na amani.
Kama vijana wa Saidi wataendelea kufanya kazi mechanically bila reasoning hakutakuwa na amani.
Kama vijana wa Saidi wataendelea kukumbatia na kunyenyekea chama tawala basi nchi haitakuwa na amani.
Saidi, Hata upewe airtime kwenye TV zote siku nzima ukahubiri bila ya na kuzingatia masuala ya hapo juu amani nchi hii itakuwa ni ndoto ya mchana.
mkuu nimekusoma!Sasa hivi Wamarekani wanasaka uranium yetu kwa udi na uvumba, nadhani mmemsikia Kikwete akisema vyandarua kwa kila mtu by August. hii ni barter-trade toka marekani kwamba wao wanatupa net za mbu na sisi tunawapa uranium. Na mtu wetu keshalainika. Hata tungeanza kukata mapanga kila siku Mmarekani hatoondoka bila kupata Uranium. Mbona wako DRC pamoja na migogoro yote huko?
Inaniuma sana mkuu!! kilichotokea Nyamongo ni blue print ya dhuluma ya serikali ya CCM.Kuna redio na viongozi wa dini ambao wanasambaza ujumbe wa chuki dhidi ya watu wengine, na hata UwT wamekiri mbele ya wabunge kwamba udini sasa ni tatizo nchini kwetu, husikii kiongozi yeyote akikemea kwa dhati. Viongozi wamekaa mkao wa ku-insinuate kinachuzungumzwa na viongozi wa kisiasa na kuuaminisha umma kwamba tatizo letu ni viongozi wa kisiasa.
Huu uongo na propaganda vilifanikiwa kipindi cha Mrema, ktk Dunia ya leo watashindwa tu. Kama kuna mwekezaji atakimbia TZ, basi ni kwa sababu ya umeme. Halafu hii busara ya kuwajali wawekezaji kuliko wazawa imeanza lini? Ndio maana watu waliuawa kama Kuku Nyamongo na miili yao kutelekezwa barabarani ili kuwafurahisha wawekezaji?
Nafikiri hapa tatizo ni tafsiri ya neno ' amani' inawezekana mheshimiwa kashindwa kuipata vizuri! Bila haki hamna amani! Aanze kuhubiri haki kwanza!
Hamkumbuki m-b-u-m-b-u mwenzie kampeni zilipo mshinda, alienda jukwaani ameshikilia simu ambayo hata haiongei alafu anawaambia watu alikua anaongea na Obama. Ama kweli!