Unajua kwanini aliitwa Kizota ?
Kizota ulikuwa ni Ukumbi Dodoma uliokuwa unatumiwa na CCM. Mwalimu Nyerere alipokuwa akiendesha mikutano, alikuwa anauliza mara kwa mata wanachama kama 'KUNA MASWALI" jibu lilikuwa "HAPANA"
Saidi Nassoro Mwamba aliposajiliwa na Yanga, mechi ya kwanza ilikuwa Dodoma dhidi ya CDA. Mechi hiyo alikuwa akifanya vitu vya kiufundi..., kutuliza gambani..., kupiga matobo, vyanzu vya kutosha.... alafu anaondoka zake........
Kwa mtindo ule ulu wa Nyerere mashabiki wakawa wanauliza “KUNA MASWALI”, kisha wanaitikia “HAKUNA…” ndio Saidi akaitwa KIZOTA”