Said Kubenea yuko wapi sasa?

Said Kubenea yuko wapi sasa?

kwa wanamapinduzi jamani huyu jamaa anatakiwa akumbukwe kilichosababisha gazeti lao kufungiwa ni kuweka bayana jinsi tss ilivyoshiriki tukio la kutekwa na kuteswa dk ulimboka so we need to honor our heroes!!! vinginevyo mapambano dhidi ya uovu kwenye jamii yatabaki post za kwenye forum tu apa na wengine kuficha identity zao!!!
 
Yupo katika harakati za kulinusuru gazeti lake tumpe support ili aendelee kutuhabarisha.
 
Nimemuona jana wakati wanahabari walipopeleka maoni yao
kwenye tume ya katiba, sijajua anafanya nini kwa sasa...
Kweli na mimi nimemuona. Lakini wanagazeti jingine liitwalo Mseto kwa hiyo bado yupo katika sekta ya habari na huenda gazeti lake likafunguliwa kwani serikali imekosa hoja ya kulifungia kwa sababu habari ile ile ndio inayoongoza kila siku katika Tanzania Daima. Nafikiri ulikuwa ni ujinga wa kiongozi mmoja asiyekuwa na elimu sahihi. Huwezi kulifungia Mwanahalisi kwa uchochezi na wakati huo huo ukamshitaki mhariri wa Tanzania Daima kwa uchochezi lakini gazeti likiendelea likiendelea kuchapishwa! Hata kesi yenyewe ya Kibanda huenda ikafa kifo cha asili kwani kahamia kwao!
 
The punishment of the wise people who refuse to take part of the government is to leave under the rule of the foolish.
 
sifikiri kama muuliza swali utapata jibu hapa hii ndiyo jf bwana mtu kusema hafahamu kwake sumu lazima atoe japo jibu la uongo ili naye aonekane yupo ha ha ha ha ha

Nami naona kama vile JF imevamiwa na watoto sijui, hata mtu akieleza ukweli ktk hali hii mtu hataweza kujua. Basi acha tu wachangie wanayotaka, maana wameingia ktk TFF na mambo kibao. Inasikitisha sometimes.
 
JF ishavamiwa. Ona majibu yanayotolewa. Kama hujui si ukae kimya. Na si uzi huu tu!

Childish!
 
Kweli kamanda kubenea hatasahaulika kwa habari zake yakinifu. Yaani mtu wa data za ukweli. Ila seikali ione aibu kwa kukandamiza vyombo vya habari. Zile habari nzito za ukweli tunazikosa maana Mwanahalisi halipo. Wanaharakati mmefikia wapi kulifufua gazeti hili pendwa!??
 
Kumbe Dalali anasoma QT ilii kutafuta qualification ya uongozi Simba.
 
hivi sasa ni mchezaji wa Taifa Stars...ila bado kidogo ataibuka na mwanahalisi yetu!
 
Huyu jamaa ni mpigania uhuru wa karne hii. Anastahili tuzo kwa wapendao uhuru wa kifikra duniani kote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom