Said Arfi: Katiba ya CHADEMA ina mapungufu

Said Arfi: Katiba ya CHADEMA ina mapungufu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
Mbunge wa Mpanda Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demkrasia na Maendeleo CHADEMA amesema kuwa hakubaliani na katiba ya chama chake hususani kifungu kinachomzuia mwanachama kwenda mahakamani endapo ataona hajatendewa haki ndani ya chama chake.
arfi.jpg

Mbunge wa Mpanda Mjini Said Arfi

Mbunge wa Mpanda Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demkrasia na Maendeleo CHADEMA amesema kuwa hakubaliani na katiba ya chama chake hususani kifungu kinachomzuia mwanachama kwenda mahakamani endapo ataona hajatendewa haki ndani ya chama chake.
Arfi ameyasema hayo leo akiwa katika kipindi cha HOT MIX cha EATV, na kusema kuwa kifungu

hicho kilicho ndani ya Katiba ya chama hicho kinapingana na Katiba ya nchi.
"Katiba ya CHADEMA naikubali kama katiba ya chama changu, lakini kifungu hicho sikubaliani nacho" aamesema Arfi.

Mbunge huyo pia amesema kuwa hakubaliani na maamuzi ya chama hicho ya kumfukuza uanachama aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kwa kukiuka kifungu hicho tena bila kufuata utaratibu za vikao.

"Hata kama Zitto alikosea, ilikuwa ni lazima vikao halali vya chama vikae ndiyo viamue, siyo kwa utaratibu uliotumika"

Akizungumzia msimamo wake ndani ya chama hicho, Arfi amesema kuwa yeye bado ni mwanachama hai wa CHADEMA kwa kuwa bado chama hicho hakijamfukuza, na kukiri kuwa aliingia katika mgogoro na viongozi wenzake wakati akiwa Makamu Mwenyekiti wa chama

hicho kutokana na kutokubaliana na mwenendo wa baadhi ya viongozi wakuu wa chama hicho.

"Ni kweli tulikuwa na mgogoro uliotokana na mimi kutokubaliana na mwenendo wa viongozi na nikaamua kujiuzulu nafasi yangu, kwa sasa hatuna tatizo tena"
Kuhusu uwezekano wa chama hicho kumfukuza, Arfi amesema kuwa hana tatizo endapo

atafukuzwa uanachama, na kwamba hawezi kusubiri kufukuzwa ndani ya chama hicho, isipokuwa "nitatafakari kabla ya kumalizika kwa mkutano wa Bunge na nitafanya maamuzi kama ninatosha kuendelea kuwa CHADEMA, maamuzi yangu nitayatangaza kabla Bunge
halijakwisha"

Arfi ametetea uamuzi wake wa kuendelea kubaki ndani ya Bunge Maalum la Katiba na kusema kuwa alikwenda bungeni kuliwakilisha taifa na siyo chama. "Sikwenda katika bunge lile kuiwakilisha CHADEMA"

Amesema msimamo wake ni kuipinga Katiba Inayopendekezwa, kwa kuwa haijajengwa katika misingi ya muundo wa muungano wa serikali tatu.

Kuhusu Uchaguzi ujao, Arfi amesema kuwa bado hajaamua kugombea, lakini kama CHADEMA

wakiamua kumfukuza, atawaachia wananchi wa Mpanda wampe muongozo juu ya nini cha kufanya na ni chama gani ataenda kugombea.

Nje ya studio, Arfi amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa yeye kustaafu siasa.

Chanzo: EATV
 
Anajichanganya tu huyu..
Mara katiba ya chama mara katiba ya nchi mara alitofautiana na viongozi mara sina shida na viongozi aaaah.
Blaah blaah mbumbumbuuu.

Mambo ya chama yanaamuliwaga na mahakama?
Kwahiyo chama kinaendeshwa na mahakama?
 
Haha..hawezi kubaliana nayo km inayafanya meno yake kuwa butu.....haha.CDM ni kiboko..hakuna fujo tena ktk kugombea kuteuliwa kuiwakilisha CDM ktk urais wala ubunge......CCM wanaumia sana kichwa....Hawa mamluki wakija CDM wanapewa chai wansema ahsante na kuondoka...bila fujo wa vurugu...Shibuda,na Zitto walikuwa wakilia kuwa wapo kifungoni..km vile vile wametolewa majinn...
 
Aondoke kama hakubaliani au hawezi ku-comply na katiba. Ay.at.olla.h kishatangualia, Arfi anasubiri masurufu yake na yeye atimke. Ila akumbuke bunge la July ndiyo la mwisho kwake hata kama atamfuata Ay.at.olla.h
 
Arfi amekuwa mwanachama wa CHADEMA kwa zaidi ya miaka 10, amekuwa Makamu mwenyekiti wa CDM kalibuni miaka 5..na kama kiongozi ilibidi uifahamu vema katiba kuliko wanachama wa Kawaida…uliwezaje wewe kuitetea katiba ya CHADEMA wakati vipengele muhimu kama hivyo hukuvijua?

Kwa nini sasa hivi ndio uanze "kuifahamu" katiba wakati umetemwa ktk uongozi?? Sisi hatutashangaa kuwa utawaunga wasaliti wenzako huko ACT…na haitusumbui sababu huna madhara yeyote wewe msaliti.
 
Arfi ni mfuasi wa Zito,na ni mwanachama wa ACT ambaye bado hajaondoka CHADEMA,ila hana madhara yoyote.Aachwe tuu huyu mzee achukue kiinua mgongo chake.Vyama vingi duniani vimeweka katazo la kwenda mahakamani ili kuweza kuwa huru kwenye maanuzi mbalimbali, kwa sababu ukiwa na wanachama wakorofi na wenye uchu wa madaraka kama akina Zito,chama kitakuwa kinashughulikia kesi mahakamani,badala ya kujieneza kwa wanachama wengi zaidi.
 
Viongozi wa Chadema walikimbilia kumfukuza Zitto kwa tamaa ya kutaka kurithi viatu vyake.
 
Last edited by a moderator:
Katiba ya Chadema ni ya hovyo ndio maana Shibuda aliichoma moto
 
Hii katiba shibuda hakukosea kuitia moto mchana kweupe sijui nani aliandaa katiba ya hovyo kama ile.
 
Mbunge wa Mpanda Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demkrasia na Maendeleo CHADEMA amesema kuwa hakubaliani na katiba ya chama chake hususani kifungu kinachomzuia mwanachama kwenda mahakamani endapo ataona hajatendewa haki ndani ya chama chake hicho kilicho ndani ya Katiba ya chama hicho kinapingana na Katiba ya nchi.
“Katiba ya CHADEMA naikubali kama katiba ya chama changu, lakini kifungu hicho sikubaliani nacho” aamesema Arfi.

Mbunge huyo pia amesema kuwa hakubaliani na maamuzi ya chama hicho ya kumfukuza uanachama aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kwa kukiuka kifungu hicho tena bila kufuata utaratibu za vikao.

“Hata kama Zitto alikosea, ilikuwa ni lazima vikao halali vya chama vikae ndiyo viamue, siyo kwa utaratibu uliotumika”
Nimefarijika sana kumsoma Arfi akizungumzia kipengele hiki.
Mimi nilikizungumzia hapa.
[h=3]CHADEMA Ikipewa Nchi, October 2015, Hakuna Hatari Kugeu
[/h]Pasco
 
Aache ujinga wake mnafiki mkubwa. Mwenyewe alishiriki kukiweka kipengele hicho kwenye Katiba halafu analeta unafiki wake hapa. Hebu akasome katiba za FIFA, TFF, n.k. zinasemaje kuhusu kwenda mahakamani.

Kimsingi, Katiba ya Chadema haimzuii mwanachama kwenda mahakama ILA ukishindwa kesi ndio kwaheri. Hii ni nzuri kwa sababu wengine badala ya kupeleka kesi za maana mahakamani, wao hupeleka majungu na hili zee ni mmoja wao.
 
Said Arfi, Shibuda na Leticia Nyerere tunasubiri muda ufike tu tuwape mkono wa kwa heri.
 
Awahi ACT wazalendo akawe chini ya mkuu wa chama kama atapata hata nafasi ya kumuhoji mwenye chama.
 
Viongozi wa Chadema walikimbilia kumfukuza Zitto kwa tamaa ya kutaka kurithi viatu vyake.

Sio viongozi wa chama mkuu,sema katiba ya chama ndio iliyomfukuzisha zito uanachama.unashindwaje kuelewa jambo dogo namna hii?watu wanaongelea katiba wewe unaongelea viongozi,ni aibu mtu ku-comment bila kujipanga.
 
Mbunge wa Mpanda Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demkrasia na Maendeleo CHADEMA amesema kuwa hakubaliani na katiba ya chama chake hususani kifungu kinachomzuia mwanachama kwenda mahakamani endapo ataona hajatendewa haki ndani ya chama chake.

Mbunge wa Mpanda Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demkrasia na Maendeleo CHADEMA amesema kuwa hakubaliani na katiba ya chama chake hususani kifungu kinachomzuia mwanachama kwenda mahakamani endapo ataona hajatendewa haki ndani ya chama chake.

Arfi ameyasema hayo jana akiwa katika kipindi cha HOT MIX cha EATV, na kusema kuwa kifungu hicho kilicho ndani ya Katiba ya chama hicho kinapingana na Katiba ya nchi.

“Katiba ya CHADEMA naikubali kama katiba ya chama changu, lakini kifungu hicho sikubaliani nacho” aamesema Arfi.

Mbunge huyo pia amesema kuwa hakubaliani na maamuzi ya chama hicho ya kumfukuza uanachama aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kwa kukiuka kifungu hicho tena bila kufuata utaratibu za vikao.

“Hata kama Zitto alikosea, ilikuwa ni lazima vikao halali vya chama vikae ndiyo viamue, siyo kwa utaratibu uliotumika”

Akizungumzia msimamo wake ndani ya chama hicho, Arfi amesema kuwa yeye bado ni mwanachama hai wa CHADEMA kwa kuwa bado chama hicho hakijamfukuza, na kukiri kuwa aliingia katika mgogoro na viongozi wenzake wakati akiwa-

Makamu Mwenyekiti wa chama hicho kutokana na kutokubaliana na mwenendo wa baadhi ya viongozi wakuu wa chama hicho.
“Ni kweli tulikuwa na mgogoro uliotokana na mimi kutokubaliana na mwenendo wa viongozi na nikaamua kujiuzulu nafasi yangu, kwa sasa hatuna tatizo tena”

Kuhusu uwezekano wa chama hicho kumfukuza, Arfi amesema kuwa hana tatizo endapo atafukuzwa uanachama, na kwamba hawezi kusubiri kufukuzwa ndani ya chama hicho, isipokuwa “nitatafakari kabla ya kumalizika kwa mkutano wa Bunge na nitafanya maamuzi kama ninatosha kuendelea kuwa CHADEMA, maamuzi yangu nitayatangaza kabla Bunge halijakwisha”

Arfi ametetea uamuzi wake wa kuendelea kubaki ndani ya Bunge Maalum la Katiba na kusema kuwa alikwenda bungeni kuliwakilisha taifa na siyo chama. “Sikwenda katika bunge lile kuiwakilisha CHADEMA”

Amesema msimamo wake ni kuipinga Katiba Inayopendekezwa, kwa kuwa haijajengwa katika misingi ya muundo wa muungano wa serikali tatu.

Kuhusu Uchaguzi ujao, Arfi amesema kuwa bado hajaamua kugombea, lakini kama CHADEMA wakiamua kumfukuza, atawaachia wananchi wa Mpanda wampe muongozo juu ya nini cha kufanya na ni chama gani ataenda kugombea.

Nje ya studio, Arfi amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa yeye kustaafu siasa
 
Arfi,shibuda,reticia walishapuuzwa na cdm,ni bora wakaondoka zao wamfuate swaiba wao zitto
 
Back
Top Bottom