Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Mawakili Gido Semfukwe na Shaban Marijani wanaowawakilisha aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Said Issa Mohamed na wenzake wawili, kwenye kesi ya jinai namba 48250 ya mwaka 2025 walioifungua Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar dhidi ya vigogo wa CHADEMA wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake wa Tanzania Bara John Heche, wamefunguka 'mahitaji' ya wateja wao kwenye kesi hiyo
Mawakili hao wamewaeleza Wanahabari leo kuwa wateja wao wanaimba Mahakama kutoa adhabu kali kwa washtakiwa kwa kukiuka amri ya Mahakama Kuu iliyotolewa Juni 10 mwaka huu, ambapo wamesema adhabu wanayoiomba ni wahusika kukamatwa na kupelekwa gerezani hadi hapo kesi ya madai inayohusu usawa kwenye mgawanyo wa mali ndani ya chama hicho kati ya Tanzania Bara na Zanzibar iliyofunguliwa Mahakamani hapo itakapofikia tamati
Kesi hiyo ya jinai ambayo imesikilizwa leo, Jumanne Oktoba 28.2025 Mahakamani hapo chini ya Jaji Awamu Mbagwa, itatolewa hukumu yake Novemba 04.2025