kinondoniilala
JF-Expert Member
- Feb 27, 2015
- 2,138
- 3,078
View: https://www.youtube.com/live/dBta4NXZCm4?is=GaPZMNUlvYMhaq2O
=============
"Kesi ya Tundu Lissu ya uongo, imetengenezwa. Kila mtu anajua. Ni kesi ya kisiasa ukisikiliza mashahidi na wenyewe walioifungua kila kitu. Inaonyesha kabisa ya uongo. Hii kesi ndio kesi pekee ambayo ipo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kesi kubwa.
"Uhaini ni mtu ambaye anataka au kumuua Rais, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais, Spika au Jaji Mkuu au mtu anataka kupindua nchi. Hii ni kesi kubwa.
"Hii ni kesi ambayo imefunguliwa na Jamhuri ambayo ni sisi wote against Tundu Lissu. Na kama kesi ina ushahidi hii ni kesi ambayo inatakiwa ishighulikiwe haraka iishe.
"Lakini angalia Lissu amekaa kuanzia Mwezi wa Pili hadi Mwezi wa nane ndio ameitwa mahakamani. Miezi Sita yupo ndani. Inakwambia ni kesi ambayo ya uongo"- John Heche, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA).
=================