Sahihisho: Ni uongo mtupu kuwa mwanamke anapenda kuliko Mwanaume!

Ctech

JF-Expert Member
Nov 21, 2010
754
816
Poleni kwanza na majukumu ya kila siku Makamanda, Tunakumbwa na changamoto Nyingi katika utafutaji wa Mkate wa Kila siku, Pamoja na yote hayo Maisha lazima yaendelee!

Twende kwenye Mada, imezoeleka na kuaminika kwamba wanawake wakipenda wamependa yaani zaidi kuliko hata wanaume (Katika uhusiano wa Kimapenzi), Huu ni uongo na upotoshaji Mkubwa mno sawa na ule ati kwamba wanawake ni wengi duniani kuliko wanaume, kitu ambacho si kweli!

Kwa umri wangu wa Miaka 70 nimeona Mengi sana, Japo Miaka ya mwishoni wa 80 kurudi nyuma sikuweza ku observe kirahisi, hasa kwa sababu fikra zangu sikuzielekeza kule, ila baada ya kuwaza na kuwazua na kuyashuhudia matukio Mengi kwa zaidi ya Miaka 50 sasa.. Nimekuja Kugundua Wanaume tuna Upendo wa Dhati kuliko wanawake!

Miaka ya karibuni ambapo macho yenu yakiona na masikio yenu yakisikia tumeona matukio mengi ya wanaume kujiua hasa kwa sababu ya mapenzi, kiwango cha wanaume kujiua ni kikubwa kuliko cha wanawake, Hii ni ishara tosha nani anapenda kweli!

Chukulia Mfano mwepesi, Katika mahusiano yangu ya Nyuma nilikuwa hata na wanawake wa Tano, ila kati ya hao wanawake watano Nilikuwa nikimpenda sana Fatuma, nikikorofishana na Fatuma nakuwa sina hata amani na hao wengine, ni Heri niachane na wengine ila Fatu wangu abaki nami!, Hii nina imani kubwa kila mwanaume ishamtokea, yaani hata akiwa na wanawake 10, yupo tayari awapoteze wale wengine 9 abaki na yule mmoja ampendaye!

Mfano mwingine mwepesi zaidi, Ni tumaini langu wengi wetu tumewahi kucheat kingono, iwe mwanamume au mwanamke.. Nilicho observe ni kwamba wanaume tunaweza kucheat na bado mapenzi yetu yakabaki asilimia zote kwa wake zetu/wapenzi wetu, ila kwa Upande wa Dada zetu ni ngumu mno wao kusex na mwanamume ambaye hayupo Moyoni mwake, kwa maana hiyo akicheat ina maana amempenda huyo mchepuko na kumuweka Moyoni.. na ndio maana ni rahisi Mno kumtambua mwanamke anayecheat Kuliko Mwanaume!

kihalisia wanawake hawapendi ila wao wanatii hisia za mwanaume, Niwakumbushe tu Mwanamume si wa Kila mwanamke, ila mwanamke ni wa Kila mwanamume.. yaani akitongozwa kwa namna inayofaa atakubali tu hata kama huyo mwanamume hakuwa tegemeo lake!

Mwisho ili kuthibitisha Kwamba Mwanamume ndiye anayependa Kuliko mwanamke turejee Biblia Takatifu katika kitabu cha Waefeso

EFE. 5:25, 28-29
"Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake. Pia katika Wakolosai 3:18 '' Ninyi wake, watiini waume zenu, kama kanisa lilivyomtii Kristu!

Wanaume wameumbwa Kupenda, Wanawake wameumbwa kutii hisia za wanaume!

Jamii Isipotoshwe!

Your Elder Brother!

Santana
 
Uko sahihi wanawake wanapenda sana wtt wao kuliko waume zao ila kwenye wingi wanawake ni wengi kuliko wanaume
 
Mianamke ya sikuizi inacheat na mioyo yao mikavu tu
Wajinga ndo hujidanganya kuwa wanawake hupenda ndo husex
Skuiz sio hvyo
 
Mzee uwe unatupa hii elimu sisi vijana. Hongera sana pia kwa kula chumvi miaka 70 si haba. Serious, nimekuombea afya lete na Mungu azidi kukutunza. Vijana Tunakuhitaji sana.
 
Mwanamke ni wa kila mwanaume... Ila mwanaume sio wa kila mwanamke.... Sawa kumbe dume hawezi penda kila mwanamke ila ke anaweza penda dume yeyote sawa
 
Back
Top Bottom