Safarini Lindi/Mtwara

Safarini Lindi/Mtwara

kuna watoto wazuri sana kule, halafu sio wachoyo.!!@
 
Kwa basi tafuta machinga,ni mapema uko mjini,kuhusu hicho kipande ambacho hakijengwa usiwe na wasiwasi hapasumbui.
Karibu ila HAITOKI

Haitoki !!!! kitu gani? Mnatutisha tusije kwenu.
 
Miaka iliyopita, wakati usafiri wa kwenda kusini ilikuwa ni lazima upande meli hasa kipindi kama hiki cha mvua za masika, barabara ilikuwa ni ya vumbi kuanzia Mbagala hadi Mnazi moja Lindi, ilikuwa inachukua siku mbili hadi nne kufika Mtwara kwa basi.

Yapo maeneo korofi ambayo bado yapo kwenye kumbukumbu za wananchi wengi wa kusini. Moja ni eneo la kivuko cha mto rufiji, mara nyingi kivuko kilikuwa kinaharibika mara kwa mara, hivyo basi kwa bahati mbaya ndiyo umefika kivukoni mkakuta ni kibovu, basi mtakaa hapo hadi spare zifuatwe Dar na kuja kuzifunga mtapinga kambi hapo kivukoni kwa zaidi ya siku tano.

Eneo lingine korofi likuwa ni Nangurukuru chini kuna bonde kubwa la mpunga na barabara kipindi cha mvua ilikuwa haipitiki kabisa.

Ukifika Mtwara nyumba za wageni zilikuwa zinafanya biashara wakati wa msimu wa kununua korosho tu, msimu ukiisha na biashara ya guest house inasimama hadi msimu mwingine wa kununua korosho mwaka unaofuatia. Nyumba iliyokuwa inafanya kazi wakati wote wa mwaka ni Lutheran Hostel, nayo ilikuwa ni ya vyumba vichache.

Simulizi hizi nimezipata toka kwa jirani yangu mwenyeji wa Liwale.

Je unayo simulizi nyingine .........
 
Ndugu, ninategemea kusafiri kikazi kwenda mikoa wa Lindi na Mtwara wiki ijayo.

Naomba msaada wa bus zuri zinazofanya safari za mikoa ya kusini, na hotel nzuri za kulala na bei zake.

Nasikia kuna kipande cha barabara baada ya kuvuka daraja la Mkapa ambacho bado hakijajengwa kwa kiwango cha lami, je kipindi hiki cha mvua panapitika?



Be specific unakwenda wapi lindi au mtwara na wilaya gani
 
Machinga Tsh 27,000/-
Buti La Zungu Tsh 22,000/-
Seth Star Tsh 22,000/-
Maning Nice Tsh 22,000/-
Hamanju Tsh 22,000/-
Ng'itu Tsh 22,000/-
Noraiz Tsh 18,000/-
Shillingi Tsh 18,000/-
Southern Exp Tsh 18,000/-
Osaka Tsh 18,000/-

Mkuu umewasahau NAJMA (semi luxury) na WIFI NAE(ordinary)! Ama hawaendi tena kusini?
 
Be specific unakwenda wapi lindi au mtwara na wilaya gani

Lindi mjini na Mtwara mjini.

Kuna hoteli ipo Mikindani kwenye magofu ya zamani ambayo yalikarabatiwa na serikali ya Uingereza na kufanywa hotel ina swimming pool na vyumba vizuri, kuna mtu yeyote anaweza kunipatia habari zaidi za hiyo hoteli, jina lake nimelisahau.
 
Hapo Lindi vp siku hizi?miaka ya nyuma niliwahi pita hapo hakukua na hotel nzuri jirani mtu kuweza pata msosi zaidi ya vibanda vya mantilie.ikabidi tupelekwe nje kidogo ya mji nbc club ndo tulipata msosi angalau
 
Hapo Lindi vp siku hizi?miaka ya nyuma niliwahi pita hapo hakukua na hotel nzuri jirani mtu kuweza pata msosi zaidi ya vibanda vya mantilie.ikabidi tupelekwe nje kidogo ya mji nbc club ndo tulipata msosi angalau

Mkuu wakazi wa Lindi hawamaindi kulakula haswa jioni. Ukiwa Lindi hakikisha kabla ya saa 2 usiku umeshakula, ikipita basi pata gahawa ukalale. Kuna Himo restaurant ina misosi mizuri ila ndo hivyo tena saa mbili ni chai na bajia.
 
Mkuu umewasahau NAJMA (semi luxury) na WIFI NAE(ordinary)! Ama hawaendi tena kusini?

Mkuu NAJMA [Semi Luxury] bado yupo ila gari zake zinaenda Nachingwea

Wifi pia zipo ila zinafanya safari kati ya Dar na Masasi!
 
Asanteni sana wakuu, kwa ufafanuzi mzuri wa usafiri wa kwenda Kusini, bado sijaelewa nikifika Lindi na Mtwara nikalale hoteli gani yenye hadhi na huduma nzuri. Naomba ushauri wenu wakuu.
Kwa Hotel ukiwa Mtwara nenda OCEAN BREEZE LODGE-ni 20000 tu iko pouwa sana, bt mara nyingi huwa iinajaa!!
Nyingiine ni MANGOELA INN...Bei yake ni 40000 ipo sehemu nzuri sana ina utulivu!! Vinwaji na chakula ni available pia!!
Agave iko pouwa pia ina Bufee ndani!!
Free Park ni 40000 nayo ni nzuri sana...wewe tu

Welcome to Gas City Mtwara
 
Bus nzuri ni Buti la Zungu, Machinga trans na Maning Nice...na tiket zake ni 3 days before....ukichelewa hupati tikiti!! All the best
 
Bus nzuri ni Buti la Zungu, Machinga trans na Maning Nice...na tiket zake ni 3 days before....ukichelewa hupati tikiti!! All the best

Kama biashara ya usafiri kusini wameimudu na wana uhakika wa kuwepo abiria wanaowasubiria kwa siku tatu , kwa nini wasiongeze mabasi Dar - Mtwara yaondoke mabasi 5 au zaidi na Mtwara - Dar yaondoke mabasi 5 au zaidi kwa kila siku.
 
Back
Top Bottom