Safari za Columbus na Catholic Monarch’s Spain (01)

Polycarp Mdemu

Senior Member
Jun 2, 2019
165
209
Kama unafuatilia historia za Ulaya basi Ni lazima unamsikia skia mwamba wa Kuitwa Christopher Columbus nadhani ubongo wake ulifanya kazi katika kipindi muhimu ulaya cha Age Of Descovery.

Anatambulika kama Mgunduzi wa Ardhi ambaye alifanya safari zake nne akikatiza bahari ya Atlantic (voyages across the Atlantic Ocean)

Bwana Christopher alikua mjuzi na alijiamini, lakini hakuwa vizuri kifedha hivyo alihitaji wadhamini wa hizi safari zake, hizi safari zake zilipata wadhamini waliojiita Catholic Monarchs of Spain hawa walikua ni Malkia Isabella I ambaye alikua mtawala wa taifa la Castile na mwingine alikua Mfalme Ferdinand II wa taifa la Aragon.

Kumbuka Malkia Isabella na Mfalme Ferdinand walioana mwaka 1469 hivyo mataifa yao (Aragon na Castile) ndipo wakaunda Spanish Empire ambayo ilikua kama Muungano wa Kinasaba yaani si rasmi, wakaja kuungana mwaka rasmi mwaka 1707, Watawala hawa walijipatia jina jipya, watu wakawaita Catholic King and Queen.

Nataka Tuingie ndani zaidi kuwahusu hawa wawili ili tupate sababu ya udhamini wao kwenye wazo au safari za Columbus.

Sasa hawa wanandoa wote wawili walitokea nyumba moja japo walitawala mataifa mawili tofauti, Walitokea ukoo maarufu uliojiita House of Trastamara na walikua wote binamu wa upili kutoka kwa mfalme Yohana I katika Taifa la Castile lakini wao hawakulijua hilo.

Hivyo kwa ukaribu huu wa kindugu "consanguinity" pengine hata ndoa yao ilikua ni batili kulingana na Canon Law, Lakini Kwakua tayari walishaanza majukumu ya Ki'ndoa basi Walipewa "Papal dispensation" na Papa Sixtus IV hivyo wakafunga ndoa rasmi mwaka 1469 huko mjini Valladolid, Wakati wanafunga ndoa Malkia Isabella alikua na miaka 18 huku Mfalme Ferdinand akiwa na miaka 17 wataalamu wa historia husema "Hapa ndio tunaweza sema Taifa la Uhispania lilizaliwa rasmi"

Hii Papal dispensation iliyotolewa na Papa Sixtus IV tuseme huwa ni Msamaha wa muda katika kesi Fulani, Yaani niseme Papa Anakua na Uwezo wa Kusimamisha utendaji kazi wa kifungu fulani cha sheria katika kesi fulani.

Concept yake ni kuwa, Si kwamba kisa sheria ni muhimu kwa jumuiya ya watu basi humfaa kila mtu na Kila hali, hivyo legislator ana haki ya kui'despense inapohitajika, Na legislator ni Papa mwenyewe.

Pia Papal dispensation si hitaji La muda wote (permanent power) wala si haki maalumu, pia haina upendeleo, Lazima iwe reasonable na particular situation hivyo si kwamba Dispensation ikitolewa basi sheria inakua imefutwa hapana!!!.

Sasa Baada Ya hii ndoa, Mambo mengi yalifuata maana Spanish Empire sasa ilikua na nguvu. Mwaka 1478 ulikamilika Spanish Empire ikishinda vita ya Kutawala visiwa vya Canary ambavyo vipo KM 100 tu Kutoka Morocco barani Africa.

Pia ikaanza vita Maarufu kama Granada War ambayo Spanish Empire walipigana na Dola la Nasrid (Emirate of Granada) ambao walikua wakipigania imani ya Uislamu.

Mwaka 1492 wayahudi na Waislamu wanaoishi Spanish Empire (Castile au Aragon) walipewa chaguzi mbili, Kukiri Imani Katoliki au Kwenda kwao Mashariki ya kati, Hapa karibu wayahudi 200,000 walifukuzwa kurudi kwao. Mwaka 1493 wayahudi na Waislamu walioishi mjini Sicily pia walipewa uchaguzi huo, takribani wayahudi 30,000 walifukuzwa.

Mfalme Manuel I wa Ureno nae akaiga kwa Kufukuza Waislamu na Wayahudi ndani ya utawala wake. Hii ilifanya Sultan wa Granada na Boabdil na Watawala wa Uhispania kukutana na kusaini Mkataba wa Amani ulioitwa Capitulation of Granada, Mkataba huu ulihusu Uvumilivu wa Kidini Kwa Waislamu. Lakini Mkataba huo haukuwashawishi Isabella na Ferdinand kuwafukuza waislam, mwaka 1502 waislamu walifukuzwa ndani ya Spanish Empire.

Hapa Utagundua Spanish Empire Iligombana na kila jamii karibu yake.

POLYCARP MDEMU

FB_IMG_1661677870415.jpg
 
Nina, Pinta & The Santa Maria.......
Japo sidhani kama ni sahihi kusema Columbus ndiye mgunduzi wa bara la Marekani.
Utagunduaje sehemu ambayo tayari kulikuwepo mamilioni ya watu wanaishi na kupaita nyumbani ??
Ni kweli. Lakini kazi ya hili jamaa haiwezi kupuuzwa
 
Deep history inasema mtu wa kwanza kutoka ulaya kuiona America (New world) alikuwa Amerigo Vecipucci na sio Christopher Columbus.

Wakati Columbus anafika Bahamas (in the Caribbean) kwa mara ya kwanza 12 October 1492, Amerigo Vecipucci alisha pita hapo na kuingia central Northern America mwaka mmoja Kabla yaani 1491.

Christopher Columbus aliamini Amerika ilikuwa sehemu ya Bara la Asia ila Amerigo Vecipucci ndio alitoa ufafanuzi kwamba North and South America are distinct continents na hazijaungana na Asia.

Jina America inasadikika lilitoholewa kutoka Jina la Kwanza la Amerigo Vecipucci.
 
Deep history inasema mtu wa kwanza kutoka ulaya kuiona America (New world) alikuwa Amerigo Vecipucci na sio Christopher Columbus.

Wakati Columbus anafika Bahamas (in the Caribbean) kwa mara ya kwanza 12 October 1492, Amerigo Vecipucci alisha pita hapo na kuingia central Northern America mwaka mmoja Kabla yaani 1491.

Christopher Columbus aliamini Amerika ilikuwa sehemu ya Bara la Asia ila Amerigo Vecipucci ndio alitoa ufafanuzi kwamba North and South America are distinct continents na hazijaungana na Asia.

Jina America inasadikika lilitoholewa kutoka Jina la Kwanza la Amerigo Vecipucci.
Amerigo =Latin
Americus =Kiitaliano.
Umenena sawia mkuu
 
Back
Top Bottom