Safari yetu iko wapi?

pambe samanini

JF-Expert Member
Oct 27, 2015
368
169
Tulianza kwa makofi mazito WA WA WA! baadae shangwe nderemo na vifijo kumbe hatukujua faida yake! Sasa kila mtaa watu wanasonyasonya tu hawana cha kusema wala kufanya si wakulima, wafanya biashara balaa kubwa watumishi wa umma na serikali mwezi huu wamekiona cha moto huku wakikumbuka usemi ule, " kuna watu wakikuwa wanaishi kama malaika lakini katika safari yangu wataishi kama mashetani" makundi haya sasa yanakiona cha moto kufa hawatakufa.

Je wajua misururu ya safari yake magari mengi wasani wengi, mashehe wengi, wachungaji, maaskofu mbele ya rangi pendwa?

Aha, kumbe ilikuwa hisani ya maneno pembeni pesa? Sasa walipeni msiwatafutie sumu kuwaua au libwata jogoo kwa kuwatunishia misuli wapeni vyao kwa sababu vyenu mmepata.

Ala! Kumbe chungu cha zamani sio chema? Basi sawa watieni sumu ili nanyi msije tumia mbeleni. Ajabu zaidi masikini na kofia za rangi pendwa hawamini kinachotokea sasa badala kuhama walipo wagongelewa misumari ili wawe palepale huku sisi tukila na kunywa vizuri.

Je, ni lini tena tutarudi safari yetu maana ndoto zetu zimezima kabisa. Ama kweli! Adui unaishi naye.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom