Wakuu,
Katika kufunga Mwaka 2011 nilisafiri kwenda Rwanda kwa ajili ya kuona mambo mbalimbali ya nchi hiyo baada ya Mauaji ya 1994. Baadhi ya vitu nilivyoona ni kama ifuatavyo:
(1) Mpakani Rusumo:
Kwa upande wa Tanzania (hakuna benki wala Bureau de change) kuna maduka madogo madogo na Wamachinga wakiwa na fedha zao mkononi kwa ajili ya kubadilisha fedha mbalimbali (Shilingi ya Tanzania, Dollar na Faranga ya Rwanda) kutoka kwa wasafiri. Kwa upande wa Rwanda, ukivuka daraja la Akagera unakutana la Bango lisemalo "Investment Yes, Corruption No." Kuna tawi la benki na Bureau de change kadhaa.
(2) Ukitoka tu Mpakani kuelekea Kigali mara moja utaona tofauti kati ya nchi hizi:
(i) Sijaona nyumba ya NYASI au TEMBE kwa upande wa Rwanda hata baada ya Kwenda Butare kusini mwa nchi.
(ii) Umeme hadi vijijini hata kama nyumba ni ndogo tu.
(iii) Nchi ya Rwanda ina idadi kubwa sana ya watu ukilinganisha na eneo la nchi (high population density). Huwezi kuona mapori kama ya upande wa Tanzania. Kwani kutoka Benaco mpaka Rusumo ni mapori tu.
(3) Usafi: Miji ya Kigali, Gitarama, Kayonza na Butare ni misafi, bustani zikiwa zimetunzwa sana.
(4) Rushwa ni kidogo. Trafic police wa Rwanda akimkamata dereva hufanya miwili tu kumwandikia adhabu ili akalipe au kumsamehe.
(5) Nini kichocheo cha mabadiliko hayo.
Baada ya kudadisi watu mbalimbali kwa nini nchi imebadilika sana katika miaka 16 iliyopita wengi wametaja ni Uongozi madhubuti wenye nia ya kuleta maendeleo ya watu. Rushwa inapingwa kabisa na mkuu wa nchi na kila mwananchi anahamasishwa kujiletea maendeleo katika eneo lake kwa juhudi na maarifa bila kuvunja sheria.
Wakuu, haya ni baadhi ya mambo niliyoyaona katika ziara hii. Kinachonisikitisha kwa upande wa Tanzania (nchi yangu) ni kuwa pamoja na rasirimali nyingi tuliyonayo bado nchi inazidi kudodora katika nyanja mbalimbali.