Mkweche II
JF-Expert Member
- Aug 11, 2018
- 4,453
- 6,336
Aseeeee
Life ya Gaborone na Windoek Namibia hayana tofauti ni kimya na kila kitu kimenyooka.Tukiachana na ule uzi wangu wa “Nilivyokwenda South Africa bila kuwa na ndugu wala rafiki” Leo nitawaelezea safari yangu ya kwanza nchini Botswana na nilioyaona na kujifunza huko.
Kwa mara ya kwanza niliingia Botswana kupitia Boda yake na South Africa, kupitia mji mdogo wa Zeerust.
Nakumbuka tulitoka majira ya saa Sita mchana kwa Bus kutoka Park Station: Johannesburg kulipitia Pretoria hadi saa mbili usiku ndipo tulifika Mji Mkuu wao wa Gaborone, Botswana. Kama kawaida barabara zao ni nzuri na za kuvutia.
Tofauti na nilivyodhani yani Kutoka boda hadi Mji Mkuu wa Gaborone haikuwa mbali sana. Ni mwendo kama wa saa moja au usizidi.
Tofauti na picha niliyokuwa nayo kichwani mwangu, nilidhani Gaborone itakuwa Mji mkubwa sana, wenye magorofa makubwa na mataa mengi, barabara za juu na chini kama ulivyo mji wa Johanesburg, Pretoria au Capetown. Niliona Mji wao ni mdogo sana na usio na mbwembwe zozote zile. Magorofa sio mengi, Barabara zao hazina mambo mengi, hakuna mambo ya mafly over.
Hata mtu aliyejifunza kuendesha gari leo anaweza kwenda nalo hadi Mjini.
Tulishuka kwenye Bus sehemu moja inaitwa Main Mall. Nikatafuta Hotel ya karibu nikafikia hapo, nililipa kwa pesa yao inaitwa Pula. Asubuhi nilikuwa natoka nakwenda zangu kutembea, kutafuta marafiki wapya na kuona mandhari ya mji wao. Mimi napenda sana kuwa na Marafiki wengi nje ya nchi, nikirudi tena ile sehemu nakuwa sio mgeni tena.
Mambo niliojifunza pale kwa muda wa Wiki mbili nilizokaa pale.
1. Gaborone ni mji tulivu sana, watu wake ni watulivu sana. Ni mji umepoa. Mji wao ni mdogo sana. Hiyo Gaborone unaweza kuizunguka kwa masaa machache na ukaimaliza. Huwezi kuufananisha na mji kama Dar. Kwa watu wanaopenda kuishi miji isiyo na mavurugu sana, ujanja ujanja basi naweza kuwashauri kufikiria Gaborone kama Mji mzuri kwao.
2. Watu wake wengi wanaendesha Magari ya thamani sana. Niliambiwa wengi wananunua magari yao kwa kuchukua Mikopo Mikubwa Bank.
3. Pesa yao ina nguvu sana kulinganisha na ya kwetu. Kwa mfano, Elfu 10 yao, kwetu ni wastani wa Milion 1 na Laki 8. Unaweza kuona utofauti mkubwa uliopo.
4. Kwa utafiti mdogo wa siku chache, wengi walisema Botswana haina nafasi nyingi za Kazi, huwezi kufananisha na South Africa. Michongo sio mingi. Harakati sio nyingi, ni kama kila kitu kimenyooka.
5. Mji ni mdogo kiasi kwamba hakuna hata stand kubwa ya Mabus kama ilivyo stand yetu ya Magufuli. Stand yao kubwa haina tofauti sana na ile Stand ya Kibaha. Stand yao haina Mabus mengi kabisa.
6. Kwa upande wa Malls, Wana Malls kubwa kutuzidi, wanazo nyingi, huduma nyingi zinapatikana huko.
Baada ya kumaliza wiki nilitaka kuchukua Bus niende zangu Namibia, Nilikosa Bus za moja kwa moja. Kwa kifupi ukiwa Gaborone hakuna Bus ya kueleweka ya kutoka nje ya nchi yao. Ruti yao kubwa ya kutoka nje ya nchi yao ni kwenda South Africa, Zipo za kwenda Bulawayo Zimbabwe lakini pia ni chache sana. Hivyo lengo langu la kupitia njia ya Gaborone hadi Namibia lilishindikana.
Kama ningetaka kulazimisha ingenibidi nichukue Bus kutoka Gaborone hadi boda yao na Namibia, nishuke hapo, nivuke kisha upande wa pili ndiyo nichukue tena Bus kwenda Mji mkuu wa Namibia. Nikasita nikaachana na hilo wazo.
Nikasema hapa naenda Zambia. Njia ya kwenda Zambia nikakuta napo hakuna Bus, pale Stand waliambia kama unataka kwenda Zambia itakubidi uchukue Bus unapita francis Town mpaka Boda ya Kazungula bus zinaishia hapo.
Halafu pale Boda uchukue gari ndogo kama Noah, mnapanda wengi hadi upande wa pili wa Zambia.
Hapo utachukua Bus kupitia Mji wa Livingstone, Mazabuka hadi Lusaka.Nilitumia njia hii kufika Lusaka Zambia.
Ni njia ndefu sana, Kwa mfano, tulitoka Gaborone saa mbili usiku na kufika Boda ya Kazungula saa kumi na mbili Asubuhi. Hapo tukavuka, saa mbili asubuhi tukachukua Bus hadi Lusaka, tulifika saa moja jioni. Ni safari ndefu na ya kuchosha sana.
Ushauri wangu kwa mtu anayetaka kufanya safari kutoka hapa kwetu kwenda South Afrika, mpaka sasa njia nzuri na uhakika ni kutumia njia ya Zambia hadi Harare Zimbabwe ndo uingie South Africa kupitia Beit Bridge. Hizi njia nyengine hazina usafiri wa kueleweka sana. Mambo yanakuwa mengi njiani.
Imeisha
Yaaani Mimi kiukweli.....ishaalah next year baada ya china najilipua Thailand...kula Bata...ofcoz naenda kuchek na fursta ya nguo za kiume kina minyoosho mikali sana....ila haswa haswa ni kama ka vacation flani Cha low budget....lazima yaani Iko kwenye check listAchana na Bangkok hiyo sehemu ni hatari[emoji119]. Mjuzi mmoja atupe mchanganuo wake
Usisahau kutupa mrejesho mkuuYaaani Mimi kiukweli.....ishaalah next year baada ya china najilipua Thailand...kula Bata...ofcoz naenda kuchek na fursta ya nguo za kiume kina minyoosho mikali sana....ila haswa haswa ni kama ka vacation flani Cha low budget....lazima yaani Iko kwenye check list
Nchi zao zinatumia resources zao walizopewa na Mungu vizuri kama madini, e.t.c kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi kwa ujumla.!Botswana na Namibia ndio nchi pekee Afrika zenye watu wenye furaha na nchi zao.
Ma nchi mengine ya Afrika Raia wao wanaishi basi tu, kwa vile hawana namna.
Yaaan ni must....Usisahau kutupa mrejesho mkuu
Nenda Namibia hasa Windhoek ni mji mzuri sana na pia safi magaribi hasa mji wa Swakopmund utapenda mji huo wa kishua sana kwenye fukwe wa Atlantic Ocean. Namibia wanafanana mengi sana na Botswana.
Kama uko competent kwenye fani ya ualimu na una uwezo wa kujilipia nauli hadi bankok, kazi za ualimu ni nyingi kule. Mie nilifanya tu kujaribu kutuma cv zangu ingawaje sio za ualimu ila walinifanyia interview kwa njia ya zoom na nika win wakasema niende hadi bankok sema kuna mchongo wa maana zaidi nikaupata hivyo sikwenda, ilikuwa mwaka jana mwezi may.Lini unaenda Korea au Thailand...
Nenda basi kafanya utaliia uje utuoe hints namna ya kwemda
Mlinganisho wa Gaborone na Lusaka pleaseTukiachana na ule uzi wangu wa “Nilivyokwenda South Africa bila kuwa na ndugu wala rafiki” Leo nitawaelezea safari yangu ya kwanza nchini Botswana na nilioyaona na kujifunza huko.
Kwa mara ya kwanza niliingia Botswana kupitia Boda yake na South Africa, kupitia mji mdogo wa Zeerust.
Nakumbuka tulitoka majira ya saa Sita mchana kwa Bus kutoka Park Station: Johannesburg kulipitia Pretoria hadi saa mbili usiku ndipo tulifika Mji Mkuu wao wa Gaborone, Botswana. Kama kawaida barabara zao ni nzuri na za kuvutia.
Tofauti na nilivyodhani yani Kutoka boda hadi Mji Mkuu wa Gaborone haikuwa mbali sana. Ni mwendo kama wa saa moja au usizidi.
Tofauti na picha niliyokuwa nayo kichwani mwangu, nilidhani Gaborone itakuwa Mji mkubwa sana, wenye magorofa makubwa na mataa mengi, barabara za juu na chini kama ulivyo mji wa Johanesburg, Pretoria au Capetown. Niliona Mji wao ni mdogo sana na usio na mbwembwe zozote zile. Magorofa sio mengi, Barabara zao hazina mambo mengi, hakuna mambo ya mafly over.
Hata mtu aliyejifunza kuendesha gari leo anaweza kwenda nalo hadi Mjini.
Tulishuka kwenye Bus sehemu moja inaitwa Main Mall. Nikatafuta Hotel ya karibu nikafikia hapo, nililipa kwa pesa yao inaitwa Pula. Asubuhi nilikuwa natoka nakwenda zangu kutembea, kutafuta marafiki wapya na kuona mandhari ya mji wao. Mimi napenda sana kuwa na Marafiki wengi nje ya nchi, nikirudi tena ile sehemu nakuwa sio mgeni tena.
Mambo niliojifunza pale kwa muda wa Wiki mbili nilizokaa pale.
1. Gaborone ni mji tulivu sana, watu wake ni watulivu sana. Ni mji umepoa. Mji wao ni mdogo sana. Hiyo Gaborone unaweza kuizunguka kwa masaa machache na ukaimaliza. Huwezi kuufananisha na mji kama Dar. Kwa watu wanaopenda kuishi miji isiyo na mavurugu sana, ujanja ujanja basi naweza kuwashauri kufikiria Gaborone kama Mji mzuri kwao.
2. Watu wake wengi wanaendesha Magari ya thamani sana. Niliambiwa wengi wananunua magari yao kwa kuchukua Mikopo Mikubwa Bank.
3. Pesa yao ina nguvu sana kulinganisha na ya kwetu. Kwa mfano, Elfu 10 yao, kwetu ni wastani wa Milion 1 na Laki 8. Unaweza kuona utofauti mkubwa uliopo.
4. Kwa utafiti mdogo wa siku chache, wengi walisema Botswana haina nafasi nyingi za Kazi, huwezi kufananisha na South Africa. Michongo sio mingi. Harakati sio nyingi, ni kama kila kitu kimenyooka.
5. Mji ni mdogo kiasi kwamba hakuna hata stand kubwa ya Mabus kama ilivyo stand yetu ya Magufuli. Stand yao kubwa haina tofauti sana na ile Stand ya Kibaha. Stand yao haina Mabus mengi kabisa.
6. Kwa upande wa Malls, Wana Malls kubwa kutuzidi, wanazo nyingi, huduma nyingi zinapatikana huko.
Baada ya kumaliza wiki nilitaka kuchukua Bus niende zangu Namibia, Nilikosa Bus za moja kwa moja. Kwa kifupi ukiwa Gaborone hakuna Bus ya kueleweka ya kutoka nje ya nchi yao. Ruti yao kubwa ya kutoka nje ya nchi yao ni kwenda South Africa, Zipo za kwenda Bulawayo Zimbabwe lakini pia ni chache sana. Hivyo lengo langu la kupitia njia ya Gaborone hadi Namibia lilishindikana.
Kama ningetaka kulazimisha ingenibidi nichukue Bus kutoka Gaborone hadi boda yao na Namibia, nishuke hapo, nivuke kisha upande wa pili ndiyo nichukue tena Bus kwenda Mji mkuu wa Namibia. Nikasita nikaachana na hilo wazo.
Nikasema hapa naenda Zambia. Njia ya kwenda Zambia nikakuta napo hakuna Bus, pale Stand waliambia kama unataka kwenda Zambia itakubidi uchukue Bus unapita francis Town mpaka Boda ya Kazungula bus zinaishia hapo.
Halafu pale Boda uchukue gari ndogo kama Noah, mnapanda wengi hadi upande wa pili wa Zambia.
Hapo utachukua Bus kupitia Mji wa Livingstone, Mazabuka hadi Lusaka.Nilitumia njia hii kufika Lusaka Zambia.
Ni njia ndefu sana, Kwa mfano, tulitoka Gaborone saa mbili usiku na kufika Boda ya Kazungula saa kumi na mbili Asubuhi. Hapo tukavuka, saa mbili asubuhi tukachukua Bus hadi Lusaka, tulifika saa moja jioni. Ni safari ndefu na ya kuchosha sana.
Ushauri wangu kwa mtu anayetaka kufanya safari kutoka hapa kwetu kwenda South Afrika, mpaka sasa njia nzuri na uhakika ni kutumia njia ya Zambia hadi Harare Zimbabwe ndo uingie South Africa kupitia Beit Bridge. Hizi njia nyengine hazina usafiri wa kueleweka sana. Mambo yanakuwa mengi njiani.
Imeisha
Nazipenda zaidi nch za Asia....jamani.Kama uko competent kwenye fani ya ualimu na una uwezo wa kujilipia nauli hadi bankok, kazi za ualimu ni nyingi kule. Mie nilifanya tu kujaribu kutuma cv zangu ingawaje sio za ualimu ila walinifanyia interview kwa njia ya zoom na nika win wakasema niende hadi bankok sema kuna mchongo wa maana zaidi nikaupata hivyo sikwenda, ilikuwa mwaka jana mwezi may.
mm napenda sana kusafri nmejitahid mpaka saiv nmesafiri nchi kama buza' mbagala' makoka' madale' k koo shimon' mbezi na vingunvguti.Tukiachana na ule uzi wangu wa “Nilivyokwenda South Africa bila kuwa na ndugu wala rafiki” Leo nitawaelezea safari yangu ya kwanza nchini Botswana na nilioyaona na kujifunza huko.