UMASKINI HAPANA
Senior Member
- Jan 3, 2017
- 105
- 47
Hiyo mkula ipo wapi hebu funguka mkuuKuchelewa kwa mvua msimu huu ulinipa changamoto ya kutafuta mashamba katika Irrigation schemes kwani huko huwa hakutegemi mvua, kulima ni mara mbili kwa mwaka na kuvuna ni uhakika. Katika hangaika hangaika zangu nilipata wasaa wa kufika kijiji kimoja kinaitwa Mkula kwenye Mkula Irrigation scheme. Kwa kweli wanakijiji wa Mkula wana neema, maji ya uhakika pale mashamba yao yana rutuba kuvuna ni uhakika kwa kweli ni raha wana Mkula wamependelewa kwa kiasi chake sidhani kama wanaijua njaa kabisa. Tatizo ni kuwa mradi una cover ekari chache sana, niliuliza nikaambiwa ni ekari 600 tu ambazo zinamilikiwa na wanakijiji takribani 148. Mwenye kujua Irrigation schemes zingine wazimwage hapa ili tukipata wasaa watu tunatembelea na kwenda kujifunza kilimo huko.
JF Members, wakulima na wajasiriamali karibuni kuchangia.
Asanteni.
Kwa ufafanuzi: Mkula ni kijiji ambacho kipo katika tarafa ya mang'ula, wilaya ya kilombero mkoani morogoro. Ni kilometa chache tu kutoka kilipo kiwanda cha sukari cha kilombero kama unaelekea ifakara.Hiyo mkula ipo wapi hebu funguka mkuu
Hii komenti ilibidi iwepo jukwaa la siasa sio hapa!Tuombe mwenyezi Mungu ampe neema rais wetu magufuri ya kuliona hili maana lipo ndani ya uwezo wake. Kama ameweza kununua ndege kwa cash, kujenga hostel udsm kwa cash, kujenga nyumba za maaskari ukonga kwa cash ni dhahiri anaweza jenga irrigation schemes za maana kwa cash. E mwenyezi Mungu mujaarie Rais wetu alione hili.
Sifa za kupata shamba ni zipi?Naming'ongo Irrigation Scheme Momba - Songwe ambayo ina ekari zaidi ya 6000 ila kwa sasa imecover ekari 1500 tu
Nyumbani hapo baada ya kuanza wilaya ya kilombero unapita vijiji vya mkamba, Kidatu, msolwa, sanje halafu mkula, serikali ingejaribu kulizingatia hili.Kwa ufafanuzi: Mkula ni kijiji ambacho kipo katika tarafa ya mang'ula, wilaya ya kilombero mkoani morogoro. Ni kilometa chache tu kutoka kilipo kiwanda cha sukari cha kilombero kama unaelekea ifakara.
hawa jamaa wameleta uzi mzuri lakini hawataki kujibu maswaliJE KM NAITAJI KULIMA KWENYE HIZO SCHEME NI HATUA GANI NIFUATE AU MASHARTI YAKE YAKOJE
shikamoo SMUHizi ndio mambo Magu na wenzie walitakiwa kuanza nazo badala ya kukimbilia kununua mapangaboi. Serikali ingewekeza kwenye infrastructure za kilimo kama hizi tuondokane na kutegemea mvua na kulialia njaa.
Watengeneze hizi scheme za kutosha na wanaotaka kulima wanaweza kukodishwa au kuuziwa. Na kwa kilimo cha kisasa kabisa huitaji eneo kubwa sana kupata mazao mengi. Kwa watu wa susbstistence farming akiwa na eka zake mbili anazoweza kulima mara mbili kwa mwaka zinamtosha kabisa. Eka moja ya mbunga, kwa mfano, inaweza kutoa mpaka gunia 50 (kwa msimu mmoja) kwa kilimo kinachozingatia mbinu bora na za kisasa za kilimo.
Tanzania haipaswi kuwa na njaa. Tuna tatizo la vipaumbele tu.