Safari ya taifa stars kwenda brazil 2014 isiishie morocco

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,954
20,463
Timu yetu ya taifa Taifa Stars inajiandaa na mechi ya kuamua ni nani aongoze kundi na kuwa na nafasi kubwa ya kuliwakilisha bara la Afrika katika fainali za kombe hilo la Dunia zitakazofanyika nchini razil mwakani.

Endapo timu yetu itafanikiwa kuifunga Morocco tarehe 8 mwezi June mjini Marrakechi na kutoa sare na Ivory Coast, basi kuna uwezekano mkubwa wa timu yetu kwenda Brazil kucheza fainali hizo kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya mpira nchini Tanzania.

Taifa Stars inafunzwa na kocha Kim Poulsen kutoka nchini Denmark na ni hivi karibuni tu mkataba wake na TFF uliongezewa miaka miwili ili ainoe vizuri zaidi timu hiyo. Kim alichukua nafasi ya kocha mwingine Jan Poulsen ambae alirudi nchini kwao Denmark.

Kim Poulsen ameiwezesha Taifa Stars kucheza mpira mzuri unaovutia ukionyesha mpangilio wa safu za mabeki, sehemu ya kiungo na ushambulaji na uchezaji wake umekuwa ni wa kisasa zaidi. Ushahidi wa uchezaji huo ni kuona Taifa Stars sasa imepanda ngazi kwenye orodha ya FIFA inayoonyesha timu zenye ubora wa usakataji kabumbu kutoka nafasi ya 145 nafasi ya 124 hadi ya 116 jambo ambalo ni la kujivunia sana. Endapo Taifa Stars itafanikiwa kwenda Brazil basi inaweza kupanda nafasi moja au mbili zaidi juu.

Pia endapo Taifa Stars itafanikiwa kwenda Brazil basi wachezaji wake wengi wanaweza kutambulika zaidi duniani na kuweza kupata nafasi ya kucheza kwenye ligi mbalimbali duniani zenye kuweza kuwapatia kipato cha kuboresha maisha yao na familia zao.

Timu ya Morocco au Simba wa Atlas (Atlas Lions) kama inavyoitwa, imeshiriki kwenye fainali hizo maarufu duniani mara ya mwisho ikiwa ni mwaka 1998 nchini France na ikatolewa kwenye hatua za awali.

Katika mechi yake na Tanzania Morocco ilichapwa magoli 3-1 na kushtukizwa kabisa na magoli hayo.Tokea mwanzo wa mchezo hali ya timu hiyo kimchezo haikuwa sawa kabisa, hakukuwa na mpangilio na wachezaji wake walionekana kutojiamini. Wachezaji wa timu hiyo walishindwa kabisa kumiliki mpira na hata walipopata nafasi za wazi za kufunga magoli walizipoteza.

Timu zilipokwenda mapumziko kocha wa timu hiyo Eric Gerets aligomba sana kwa wachezaji wake na akawaambia kwamba ufanisi wao kiuchezaji ulikuwa ni mbovu haijapata kutokea.

Lakini kama alikuwa amepigilia misumali jeneza la timu hiyo, kipindi cha pili Morocco walishangaa kutundikwa goli la kwanza mara tu kipindi cha pili kilipoanza na Ulimwengu Thomas kwenye dakika ya 46, kala hawajakaa sawa Mbwana Samata akatundika goli la pili na baadae dakika ya 79 akatundika goli la tatu, Morocco wakawa chali!

Morocco walijitahidi kujitutumua kutafuta goli na walikuja kuambulia goli pekee la kufutia machozi dakika ya nyongeza ya 93 liliofungwa na Youssef El Arabi.

Waliporudi nchini kwa kocha Gerets akafukuzwa kazi na nafasi yake ikachukuliwa na Rachid Taoussi ambae ni Mmoroko.

Kwenye orodha ya FIFA Morocco inashika nafasi ya 74 kutoka nafasi ya 77 iliyokuwa miaka miwili iyopita na katika kutaka kutetea nafasi yake hiyo kwenye ulimwengu wa soka timu hiyo ina wachezaji wanaocheza soka kwenye ligi mbalimbali barani Ulaya kama Marouane Chamakh wa Arsenal (anachezea West Ham kwa mkopo) na Adel Taarabt wa Qeens Park Rangers ambayo imeshuka daraja msimu huu kwenye ligi kuu ya Uingereza.

Marouane Chamakh wa sasa si yule Chamakh aliekuwa akichezea Bordeaux ya France kiasi cha kuwavutia Arsenal kumsajili na hakuweza kuchezea timu hiyo mara zote. Chamakh amecheza mechi 67 na kufunga magoli 14 tu. Arsenal ikamtoa kwenda West Ham kwa mkopo hadi mwisho wa msimu wa 2012/13 na amecheza mechi tatu tu na hajafunga goli hata moja.

Kocha wa Morocco Taoussi alikwishamtoa mshambuliaji huyo kwenye timu hiyo kwa sababu za kwamba hajacheza mechi nyingi kwenye ngazi ya klabu.

Mchezaji mwingine ni Taarabt ambae nae amezunguka kwenye timu za Tottenham na QPR nchini Uingereza ambae nae hana rekodi nzuri ya ufungaji magoli inagwa kwa Taifa Stars ni lazima waangalie hili.

Wapo wachezaji wengine wanaocheza Ulaya kama Youssouf Hadji mchezaji wa kiungo anaechezea Al Arabi ya Qatar, mshambuliaji Youssef El Arabi anaechezea Granada ya Spain ambae alicheza mechi na Taifa Stars na mshambuliaji Mounir El Hammoudi anaechezea Fiorentina ya Italy kwenye ligi ya Serie A.

Itakumbukwa mshambuliaji huyu ndie alieifunga Taifa Stars goli pekee kwenye uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa kufuzu kucheza fainali za mataifa huru ya Afrika yaliyofanyika mwaka 2012.

Pia kwenye timu hiyo alikuwemo Younes Belhanda mchezaji wa kiungo anaechezea Motepellier ya France ambae aliondolewa na kocha wa sasa Taoussi ambae amewapa kipaumbele wachezaji wanaotoka ndani ya nchi hiyo. Yumo Oussama Assaidi ambae ni mshambuliaji wa pembeni wa timu ya Liverpool ya Uingereza na Karim El Ahmadi ambae huchezea nafasi ya mlinzi kiungo (defensive midfielder) wa timu ya Aston Villa pia ya Uingereza.

Wapo walinzi Mehdi Benatia wa Udinese ya Italy na Ahmed Kantari ambae ni mkoba anaechezea timu ya Stade Brest ya France.

Kocha Taoussi ana rasilimali ya kutosha kuchezesha timu nzima ya wachezaji kutoka mamtoni lakini katika timu yake yenye wachezaji 24, 16 kati yako wanatoka nchini Morocco. je alikuwa anajaribu wachezaji hao na jariio limegonga mwamba?

Safari ya kwenda Brazil si ya kuichezea hata kidogo na Taifa Stars ian wajibu wa kukaza uzi uleule iliyoukaza kwenye uwanja wa nyumbani wa Ben Mkapa mpaka kufikia kuwatungua Morocco 3-1.

Kama kawaida ya waarau hawa wakiwa kwao ni lazima Taifa Stars wajiandae kukabiliana na vitimbwi na kelele za kuwachanganya kutoka kwa maelfu ya wamoroko ambao watakuwa nyuma ya timu yao kutaka ifidie magoli hayo matatu.

Lakini nina imani na kocha Poulsen ataiandaa timu yetu vizuri na kuhakikisha kwamba malengo yetu ya kuwadhibiti Morocco kwenye mtindo wao wa kutumia kona, mipira ya adhabu na mashambulizi ya kushtukiza yanatimizwa.

Kila la kheri timu yetu ya Taifa Stars.
 
Kazi ya kwenda Brazil bado ni ngumu sana kwetu,nafikiri washindi wa kwanza wa kila kundi watakutana tena raundi nyingine ya mtoano.Kwa sasa kuna makundi 10 na Africa tutawakilishwa na timu 5,so tukifanikiwa kuongoza kundi letu bado tutakutana na vigogo wengine wa Afrika
 
Napenda kusema ukweli unaoniumiza hata mimi mwenywe....Ni ndoto sisi kwenda huko kwa sasa!! Kwanini?? kwasababu tumefanya almost zero invetsment kwenye soccer, huu unatakiwa uwekezaji wa muda mrefu sio hii ya kukusanyana, i stand to be challanged
 
Kazi ya kwenda Brazil bado ni ngumu sana kwetu,nafikiri washindi wa kwanza wa kila kundi watakutana tena raundi nyingine ya mtoano.Kwa sasa kuna makundi 10 na Africa tutawakilishwa na timu 5,so tukifanikiwa kuongoza kundi letu bado tutakutana na vigogo wengine wa Afrika

Tena bado sana

Napenda kusema ukweli unaoniumiza hata mimi mwenywe....Ni ndoto sisi kwenda huko kwa sasa!! Kwanini?? kwasababu tumefanya almost zero invetsment kwenye soccer, huu unatakiwa uwekezaji wa muda mrefu sio hii ya kukusanyana, i stand to be challanged
ninaiona concern yenu katika hili,lkn hebu tujaribu kujipa matumaini badala ya kukata tamaa!tuunagene tujaribu kushauri ni nini kinaweza kufanyika katika hili hata kama ni kwa kuchelewa!tunayo nafasi,mpira unadunda ndugu zangu!!
 
ninaiona concern yenu katika hili,lkn hebu tujaribu kujipa matumaini badala ya kukata tamaa!tuunagene tujaribu kushauri ni nini kinaweza kufanyika katika hili hata kama ni kwa kuchelewa!tunayo nafasi,mpira unadunda ndugu zangu!!
mpwa sijakata tamaa ila ninachosema ni kwamba hatuja invest kwahio tusitegemee muujiza wowote
 
Haiwezekani kwa Tz kwenda Brazil, bado soka letu ni lile la kajamba nani a.k.a bila bangi mchezazi anakuwa under performance.! Wakienda Brazil mie nakunywa sumu
 
mpwa sijakata tamaa ila ninachosema ni kwamba hatuja invest kwahio tusitegemee muujiza wowote

Hilo ndilo kosa la wabongo tunategemea maajabu hata kwenye mambo ya kawaida tu.
 
Ni kweli unavyosema mkuu Belo.

Ni timu 5 tu ndizo zitaliwakilisha bara letu la Afrika.

Nafikiri cha msingi ni timu yetu ya Taifa Stars kuhakikisha inaifunga Morroc huko kwao na pia iombe Ivory Coast ifungwe na Gambia jambo ambalo haliwezekani.

Baada ya hapo kutakuwa na timu za nchi 10 ambazo zitacheza mwezi wa October kwa raundi 2 za nyumbani na ugenini ambazo ndizo zitakazotoa timu 5 za kwenda Brazil.

Kamati ya maandalizi ingekazania kushirikiana na FA kutafuta mechi nyingi za kirafiki kati ya sasa na mwezi wa tano mwakani kabla ya fainali hizo.

Mechi hizi ni lazima ziwe na angalau timu za Ulaya mashariki kama Latvia, Bosnia, Poland, Greece, Turkey, uarabuni -Qatar na hata kule Scandinavia- Denmark anakotoka Poulsen kama sio Norway au Finland.

Zitafutwe mechi ambazo halitaingiza gharama kubwa katika nauli, malazi na chakula.

Huu ndio wakati wa kuiangalia timu hiyo ambayo inaonekana ina wachezaji ambao wanasikiliza maelekezo.
 
ninaiona concern yenu katika hili,lkn hebu tujaribu kujipa matumaini badala ya kukata tamaa!tuunagene tujaribu kushauri ni nini kinaweza kufanyika katika hili hata kama ni kwa kuchelewa!tunayo nafasi,mpira unadunda ndugu zangu!!
Kwa mtazamo wangu nafikiri kabla hatujafikiria kwenda WC ,focus yetu kwanza ingekuwa kwenda African Cup ambapo nafasi zipo nyingi na upinzani sio mkubwa kama wa WC.Jirani zetu kama Kenya,Rwanda,Mozambique,Malawi,Congo wamefanikiwa kushiriki Afcon kwa miaka ya karibuni then tukifanikiwa ndio tuhamie kwenda World Cup
 
Kwa mtazamo wangu nafikiri kabla hatujafikiria kwenda WC ,focus yetu kwanza ingekuwa kwenda African Cup ambapo nafasi zipo nyingi na upinzani sio mkubwa kama wa WC.Jirani zetu kama Kenya,Rwanda,Mozambique,Malawi,Congo wamefanikiwa kushiriki Afcon kwa miaka ya karibuni then tukifanikiwa ndio tuhamie kwenda World Cup
usemayo ni kweli mkuu,lkn kama muwindaji huwezi kukutana na swala porini na kumuacha aende kwa kigezo cha kutafuta uzoefu kwa kuwinda sungura kwanza!mashindano yalio mbele yetu sasa ni WC hatuwezi kukunja miguu kusubiri AFCON!tujaribu hili lililo mbele yetu tukiwa tunajenga timu kwa kila mashindano yanayokuja!
 
mpwa sijakata tamaa ila ninachosema ni kwamba hatuja invest kwahio tusitegemee muujiza wowote
mkuu mi nina roho ya daktari!!hata akiona mgonjwa anaakufa bado atawapa moyo ndugu kuwa hali si mbaya sana!!
 
Hilo ndilo kosa la wabongo tunategemea maajabu hata kwenye mambo ya kawaida tu.

Jambo la msingi tuongoze kwanza hili kundi, mtoano ni hatua rahisi sana kuliko ligi. Tunaweza kumfunga mtu goli 3-0, tukienda kwake hata akitubamiza 2-0 huyo kesha toka. Wachache mno walioamini kuwa Chelsea angekuwa bingwa mwaka jana. Katika soka lolote laweza tokea: go, go, go Taifa Stars; tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele, Aluta continua!
 
wakuu tunaipenda sana nchi yetu lakini cha kushangaaza ni kwamba serikali yetu suala la soka wanalipuzia sana wanabenzi sana katika siasa sasa utaona timu yetu ya tanzania hua haifiki popote na wachezaji walioo katika timu mara nyingi utaona ni watoto wa vogogo au watu maarufu ambao walikua ni wachezaji marufu mpira hapa tanzania au ni watoto wa ccm naamini kwamba nchi yetu ni kubwa sana na kuna watoto wana vipaji katika tanzania hii ila hawaonekani kutokana na ukiritimba wa nchi yetu na ufisadi mwingi samahani kama itakua nimeongea vibaya
mungu ibariki tanzania mungu ibariki africa mungu wabariki watoto wa tanzania .
tanzania.PNG
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom