Safari ya Songea

Safari ya Songea

zwangandaba

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2023
Posts
750
Reaction score
1,425
Nimepanda basi la Songea. Ni New force linapitia mikoa ya kusini.

Kilichonishangaza nikuona abiria wenzangu karibia 10 wamenunua maembe pale Mbagara na kuanza kuyafakamia.

Huyu dada niliekaa nae pamoja na kuwa sista duu nae yuko bize na maembe yake kutafuna na kutema maganda nje ya kioo. Nyie wangoni kwani huko Songea hakuna maembe? Halafu hii tabia ya kula vyakula hovyohovyo mbona kama imekaa kishamba sana?

Kama ni njaa, maembe yanatibu njaa? Kwanini usivumilie mpaka Nangurukuru kwenye restaurant ukapate breakfast.

Nimesafiri sana na mabasi ya kaskazini, Iringa, mpaka Mwanza sikuwahi kuona abiria wakila maembe tena kwa kung'ata na meno ndani ya usafiri wa umma.
 
Nimepanda basi la songea. Ni New force linalipitia mikoa ya kusini.

Kilicho nishangaza nikuona abiria wenzangu karibia 10 wamenunua maembe pale mbagara na kuanza kuyafakamia.

Huyu dada niliekaa nae pamoja na kuwa sista duu nae yuko bize na maembe yake kutafuna na kutema maganda nje ya kioo.

Nyie wangoni kwani huko songea hakuna maembe?

Halafu hii tabia ya kula vyakula hivyohovyo mbona kama imekaa kishamba sana?

Kama ni njaa, maembe yanatibu njaa? kwann usivumilie mpaka Nangurukuru kwenye restaurant ukapate breakfast.

Nimesafiri sana na mabasi ya kaskazini, iringa, mpaka mwanza sikuwahi kuona abiria wakila maembe tena kwa kung'ata na meno ndani ya usafiri wa umma
Kila mtu ashinde mechi zake.
 
Kwanini usingepanda super feo kupitia Iringa?? Hiyo njia siipendi

Nikipita huko nahisi nimepanda daladala,kila kituo basi linashusha na kupakia.
 
Kwasqbabu huku songea maembe yetu ni si matamu kama yq huko,


Kule safarini inategemea binafsi nikisafiri kutoka kwetu chai nitakunywa njombe au makambako, mchana nitakula Iringa.
 
Back
Top Bottom