Safari ya mwisho ya Yusuf Asukile Seleman

U know nothing, pamoja na kuaa huko "nje" nimegundua bado huna la kuisaidia jamii yako ya ulipotoka.
Labda tuanzie hapa ulitaka azikwe vipi?
Maana hata kama ni Dini, bado ingemtenga na Dini nyingine. Hivi askari anapofariki binafsi ungependa azikwe vipi? Maana kwa hoja zote ulizojenga hapo juu inamaana hata maziko ya askari wetu tunakua tunakosea.

Leo unataka tuige mfumo wa maziko huko nje, hivi ni kwa nini wao wanakua wanatoa mwaliko kwa baadhi ya watu flani ndio wahudhurie maziko ya marehemu, na si jamii au ndugu na jamaa wote wa marehemu, kama tufanyavyo huku?
Shukuru Mungu umezaliwa Tanzania. Otherwise kama imekuumiza sana, funga vilivyo vyako hama nchi, ukahudhurie maziko ya marehemu wa huko "nje" ulipopendezwa napo.

Kwa Africa, hasa Tanzania ni Dini na Siasa mbali ya Harusi na Misiba ndio matukio yanayowakutanisha watu na jamii mbali mbali na kujikuta watu wamefahamiana na kua jamii moja.
umeongea point sana mkuu.
 
R.I.P kamanda tutakuenzi tarehe 1 ya ukuta

R.I.P kamanda Asukile
Jamani kifo chake kimetokana na nini?

Nitakumbuka daima harakari zake za siasa tangu tukiwa chuo cha uhasibu Arusha.

Mungu awape faraja wana familia kipindi hichi kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.
 
Kwa Africa, hasa Tanzania ni Dini na Siasa mbali ya Harusi na Misiba ndio matukio yanayowakutanisha watu na jamii mbali mbali na kujikuta watu wamefahamiana na kua jamii moja.
kama unasema Afrika misiba hukutanisha watu na jamii mbali mbali basi huu msiba ulikutanisha watu na jamii ya CHADEMA!

Utageuzaje msiba kuwa kama sherehe ya chama? Cheki jamaa ni kama wana dance nyimbo za CHADEMA na mabendera juu juu.

Hili halipendezi na ndio mambo yanayoleta matatizo nchini. Mwana C.C.M. anamuona mwana CHADEMA adui, mwana CHADEMA anamuona mwana C.C.M. adui. Mpasuko tulionao nchini sasa hivi unapaliliwa na mambo haya ya vyama mpaka misibani.

Mkuu ulihudhuria maziko ya Balali?
Hapana sikuhudhuria maziko ya Bilali lakini najua ulikuwa msiba fulani private kwa sababu wafiwa waliona marehemu alisakamwa akiwa hai na akasakamwa akiwa amekufa ikidaiwa maiti ilikuwa msukule. Kwani zaidi ya mitafaruku ya shutuma za ufisadi kulikuwa na siasa za vyama?
 
Hapana sikuhudhuria maziko ya Bilali lakini najua ulikuwa msiba fulani private. Kwani zaidi ya mitafaruku ya shutuma za ufisadi kulikuwa na siasa za vyama?
Mpasuko unajengwa na roho ya mtu mwenyewe. Ulikuwepo kwenye huo msiba, au uliambiwa kuna mwana CCM alikuja akafukuzwa, au unaendeshwa na hisia tu.? Nikiwambia kuna baadhi ya wana CCM wametoa rambi rambi utakataa?
Vile umeona baadhi ya watu wamevaa nguo za chama cha CHADEMA, basi umekuja na majumuisho yako, kwamba msiba umeendeshwa kichama?
Kwahiyo hata marehemu hakufanyiwa ibada ya mazishi?
 
img-20160827-wa0123-jpg.388929

Ndio, msiba umeendeshwa ki chama chama, jeneza limefunikwa bendera ya chama, wakina mama wanne na kijana mmoja wanaofukia kaburi wote wana ma vilemba na mashati ya chama, huyo anaepewa pole na kila mtu ( au sijui ndio anaekaribisha wageni ) na yeye ni nguo za CHADEMA mwanzo mwisho. Hakuna mwana C.C.M. aliyefukuzwa lakini mandhari na munkari wa CHADEMA msibani haukaribishi wasio CHADEMA.

Ningekuwa mimi ni mwana kamati ya mazishi ningesema jamani kama tunataka kuenzi kazi ya ndugu yetu, kama tunataka kulionyesha Taifa kwamba CHADEMA ilifanya kazi za kutumikia nchi kupitia marehemu wetu basi tulivalishe jeneza bluu, nyeusi, kijani na njano.

Tupambe msiba na alama za Taifa, tumfunike marehemu bendera ya Taifa, tusimame wima tuimbe mwimbo wa Taifa. Hiyo inge pay a more powerful tribute to his legacy than the divisive and parochial partisan themes. Kwa sababu alitumikia chama, ndio, lakini mwisho wa siku his ultimate goal was grander than party, kalitumikia Taifa.
 
Ndo
Nd
img-20160827-wa0130-jpg.388948

Sidhani kama ni sawa kuzikwa ki CHADEMA-CHADEMA.

Ukienda kwenye nchi ambazo tumeiga haya mambo ya vyama vingi haya kwa mfano Marekani, kwa nini huwezi kukuta msiba wa Republicans??? Unadhani wafu wao hawana vyama? Nimeishi nje miaka mingi sana lakini gwanda rasmi la Democrats silijui wala bendera ya Republicans siijui inafananaje, Taifa lao lina bendera moja tu, red, white and blue.

Waafrika ni wepesi wa kugawanywa na mambo ambayo kwanza tumeiga, siyo ya kwetu, pili wao wenyewe huko kwao hawayavalii njuga; dini zao zinatugawa, demokrasia za vyama vingi zinatugawa.

Ukija kwenye makundi yetu ya asili kama makabila unakuta mara nyingi hayatugawi, ni upinzani wa watani kwa watani tena wa upendo na mzaha na uko very mild, hakuna msiba wa Mchaga ambae anazikwa na mabendera ya Kichaga! Rafiki za marehemu ambao ni Wahehe wangejisikiaje kwenye hayo mazishi?

What if, I don't know, but let's say mwanae mmoja au mke wa huyu Marehemu ni C.C.M. damu, kwa nini mumkalie kooni amzike mumewe ki-Chadema Chadema? We are looking at everything through the prism of politics and everything political, resulting in massive problems for ourselves.
Ndio maana abdul jumbe aliacha wosia namna ya kuzikwa
 
img-20160827-wa0123-jpg.388929

Ndio, msiba umeendeshwa ki chama chama, jeneza limefunikwa bendera ya chama, wakina mama wanne na kijana mmoja wanaofukia kaburi wote wana ma vilemba na mashati ya chama, huyo anaepewa pole na kila mtu ( au sijui ndio anaekaribisha wageni ) na yeye ni nguo za CHADEMA mwanzo mwisho. Hakuna mwana C.C.M. aliyefukuzwa lakini mandhari na munkari wa CHADEMA msibani haukaribishi wasio CHADEMA.

Ningekuwa mimi ni mwana kamati ya mazishi ningesema jamani kama tunataka kuenzi kazi ya ndugu yetu, kama tunataka kulionyesha Taifa kwamba CHADEMA ilifanya kazi za kutumikia nchi kupitia marehemu wetu basi tulivalishe jeneza bluu, nyeusi, kijani na njano.

Tupambe msiba na alama za Taifa, tumfunike marehemu bendera ya Taifa, tusimame wima tuimbe mwimbo wa Taifa. Hiyo inge pay a more powerful tribute to his legacy than the divisive and parochial partisan themes. Kwa sababu alitumikia chama, ndio, lakini mwisho wa siku his ultimate goal was grander than party, kalitumikia Taifa.
We kweli "nje" pamekuharibu. Unajua matumizi ya bendera ya Taifa katika mazishi?
Sasa kwa kua hakuna mwana ccm aliyefukuzwa msibani ndio ujue ulikua msiba wa wote katika jamii iliyomzumguka marehemu na majirani. Kuvaa sare ya chama, hakumuondolei raia aliyekua na mapenzi mema na marehemu kuhudhuria maziko au msiba wake.
Na hapo ukiangalia kwa haraka unaona au walio kwenye kaburi ni watu ambao either walikuja tayari watu wamekwisha zika na wao wakaona ni bora kuweka udongo wa mwisho.
Kwa aina ya maandishi uliyoandika humu inaonesha ni mtu mpenda kutengenezea chuki na utengano baina ya watu.
Umeshindwa kukemea ziara za Raisi kama serikali kwanini zinasindikizwa na wajumbe wa chama CCM, unakuja kutafutia Kiki kwenye msiba ya raia ambao ni wanachama wa Chadema.
Huko "nje" wameona mengi, na sijui kwa hao raia wa kigeni ulipo kua walipata picha gani ya Taifa la Tanzania.
 
Jibu lina faida kwangu.

Ukiangalia hizo picha taratibu nyingi zilizofuatwa hazipo kwenye mazishi ya muislam.
Wanyakyusa pamoja na kuupokea ustaarabu wa Waarabu hawajaacha Desturi zao kama Makabila mengine hapa nchi hasa wale wa Mwambao wa Pwani.

Kuna msiba ulitokea kijiji cha Kapugi, Marehemu alikuwa Mzee (Mwanaume) wa kiislam, ulipofika muda wa mazishi tulijumuika wote wanawake kwa wanaume [emoji12]

Tunachagua mazuri tu, haya mwengine bakini nayo wanaume wa Dar es Salaam
 
kama unasema Afrika misiba hukutanisha watu na jamii mbali mbali basi huu msiba ulikutanisha watu na jamii ya CHADEMA!

Utageuzaje msiba kuwa kama sherehe ya chama? Cheki jamaa ni kama wana dance nyimbo za CHADEMA na mabendera juu juu.

Hili halipendezi na ndio mambo yanayoleta matatizo nchini. Mwana C.C.M. anamuona mwana CHADEMA adui, mwana CHADEMA anamuona mwana C.C.M. adui. Mpasuko tulionao nchini sasa hivi unapaliliwa na mambo haya ya vyama mpaka misibani.

Hapana sikuhudhuria maziko ya Bilali lakini najua ulikuwa msiba fulani private kwa sababu wafiwa waliona marehemu alisakamwa akiwa hai na akasakamwa akiwa amekufa ikidaiwa maiti ilikuwa msukule. Kwani zaidi ya mitafaruku ya shutuma za ufisadi kulikuwa na siasa za vyama?
Maziko ya Aboud Jumbe unayalinganishaje na Balali kwa maana ya mtizamo wa jamii juu ya kila mmoja wao wakati wa uhai wao i.e Alhaji alishutumiwa na serikali lakini jamii ikiona anaonewa ilihali Balali "ilidaiwa na serikali" kuwa alisakamwa kwa maneno na raia huku jamii ikiiona kauli hiyo ya serikali ni ghilba!!!!

Mwishowe Aboud Jumbe kuacha wosia ulioifedhehesha serikali (kukataa kuzikwa kiserikali)
Liambie jukwaa tafadhali.
 
Poleni sana wafiwa mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina.
 
Habari imenishtua saana! I was on my way to mby yesterday but I wasn't aware on what was happening there up until I gotten this message! Very painful for Christ sake!
 
RIP

Alikuwa muislam au mkristo?
Alikuwa mtanzania
Safari ya maisha ya kamanda YUSUF ASUKILE SELEMAN ilifikia tamati jana jumamosi tarehe 27/8/2016. Alizikwa jimboni kwake Rungwe kata ya kinyala.
Yusuf Asukile alikuwa mgombea wa CHADEMA JIMBO LA RUNGWE 2010.. NA MWAKA 2015 ALIJITOKEZA KUGOMBEA BILA MAFANIKIO. AMEFARIKI AKIWA NI MTUNZA HAZINA WA CHAMA KANDA YA NYASA..

View attachment 388928 View attachment 388929 View attachment 388945 View attachment 388946 View attachment 388947 View attachment 388948

Back
Top Bottom