Asante
JF-Expert Member
- Dec 18, 2009
- 2,086
- 1,081
Waungwana ninatajia kusafiri mikoa ya kusini ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kikazi; kusudio la waraka huu ni kuomba kupatiwa taarifa kwa yeyote anayeijua barabara inayotoka Masasi, Nanyumbu, Tunduru hadi Songea kama inapitika kipindi hiki cha mvua, na kama inapitika ni basi gani zuri linalofanya safari zake kutoka Mtwara/Masasi hadi Songea. Sina tatizo na sehemu ya kulala Lindi, Mtwara na Masasi lakini Songea ni mgeni kabisa naomba kujua hotel au lodge nzuri ya kulala wageni bei yake isizidi 50,000 kwa siku.