joshydama
JF-Expert Member
- May 10, 2016
- 4,623
- 5,037
Habari za usiku mabibi na mabwana. Ni matumaini yangu kwamba hamjambo wote humu ndani. Pia poleni sana kwa majukumu ya hapa na pale katika ujenzi wa taifa letu.
Wana JF, bila kupoteza muda ni kwamba 2007 mpaka 2014 nilipata nafasi ya kutembelea Baadhi ya Nchi za bara la Ulaya na Nchi za Asia.
Kama mjuavyo kuna msemo wa Kiswa hili unasema kwamba "mtu ambaye hajawahi kusafiri anafikiri/ anaamini kwamba mama yake ni mpishi bora" ( the person who has never travelled widely thinks/ believes that his or her mother is the best cook).
Kusafiri siyo anasa bali ni chanzo cha maarifa. Ukisari utakutana na mambo mapya yaani utamaduni wa watu fulani, watu wapya na utapata wasaa wa kujifunza mambo mengi sana.
Nikianza na safari yangu ya Bara la Asia hasa nchini India ambapo nilibahatika kujifunza kuhusu suala la utamaduni wao hasa katika utendaji kaji na suala la kujituma katika kazi kitu ambacho kipo tofauti sana na huku nchini kwetu.
Nchini za wenzetu watu wanajua kuthamini na kuheshimu kaza zao, wafanyakazi wana nidhamu kubwa sana katika katika, wanajua kujali wateja (they do really care their customers). Pia wanathamini na kuzingatia muda wao sana. Hawataki kupoteza muda wao.
Kadhalika utendaji kazi wao ni mkubwa sana ukilinganisha na wafanyakazi wa nchini Tanzania. Unapewa huduma iliyo bora na ya kiwango cha hali ya juu.
Aidha, katika utendaji kazi zao hasa Madaktari wana nidhamu na wanapenda sana kazi zao. Mfano ukiwa katika chumba cha matibabu muda wote umezunugukwa na wauguzi na madaktari. Kila chumba chao cha matibabu kina kengele ambayo ukigusa tu hiyo kengele utaona madaktari, wauguzi na viongozi wengine wanavyokimbizana kuja kuangalia kuna nini. Watakuja watakuzunguka wakikuuliza unataka nini n.k.
Kitu ambacho ni tofauti sana na hapa nchini kwetu ambapo madaktari, wauguzi, na viongozi wengine wana viburi, hawajali wateja wao, wana lugha mbaya kwa wateja wao, utendaji mbovu katika kazi, hawajitumi, hawazingatii maadili taaluma zao mfano hivi karibu katika hospitali kubwa tu hapa nchini walifanya kitu cha ajabu ambapo walisababisha mwana mama kupoteza maisha kwa sababu ya ujinga wa Madakatari wetu.
Ilikuwa hivi kuna mwana mama mmoja alienda hospitali kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji. Katika kufanyiwa upasuaji wale Madaktari walikata utumbo wa yule mwana mama. Sijui ilikuwa ni bahati mbaya au ilitokana na uzembe wao.
Kilichofanyika ni kwamba baada ya kukata ule utumbo hawakushughulika tena na tatizo walilolisababisha bali walipotezea na wakamshona kidonda chake na kuacha ule utumbo ukiwa na jeraha kwa ndani. Kitu ambacho kilisababisha mwanamama kuoza utumbo na kupelekea kifo chake.
Kadhalika, nchi za wenzetu wanazingatia sana utendaji kazi, ujuzi na uwezo juu ya kitu fulani hawazingatii sana katika vyeti. Kwa upande wao certificates are just nothing. They don't really care about certificates. Wakati nchini Tanzania tunaangakia vyeti sana badala ya ujuzi na utendaji kazi. Ndiyo maana Leo hii tuna mainjinia wengi ambao wana vyeti vizuri tu lakini hawajui hata kuweka(fixing) kitasa cha mlango ila fundi wa kawaida toka VETA au mwenye utaalamu wake anauwezo wa kutengeneza hicho kitasa vizuri sana. Ila huyu fundi kwa ambaye ana uwezo na ufanisi mkubwa katika kazi atadharaurika kwa sababu hana cheti cha uinjinia. Kitu ambachi ni upuuzi mtu.
Wadau wa JF, kwa machache niliyoelezea hapo juu ni dhahiri kuwa ukitembea utajifunza mengi sana. Hata kama ulikuwa na kasumba fulani kichwani mwako hakika ukifika Nchi za wenzetu ukaona wanavyoishi hakika utabadilika sana. Mfano kwa upande wangu mimi huwa naamini katika utendaji na siyo vyeti kama baadhi ya watanzania wanavyoamini na kuthamini vyeti kuliko ujuzi wa mtu. Na ndiyo maana tu watendaji kazi wa hovyo sana nchini kwetu.
Aidha, Nchini Tanzania waajiri hawana exposure hata kidogo na ndiyo maana wanathamini vyeti kuliko ujuzi. Kadhalika badala ya kufanya practical interview wao wanapenda theory interview ambayo ni upuuzi mtu. Mfano dakatari anataka kazi mpe practical ya upasuaji, mpishi anataka kazi mpe chakula apike uone kama anaweza au la na siyo mahojiano yasiyo na tija.
Ahsanteni na karibuni kwa michango.