Safari ya 315: Rais Kikwete kuelekea Namibia?

hata sisi tunaweza kumpangia sema bado tumelala angekuwa kila akitaka kuondoka au kurudi anatukuta uwanja wa ndege na mabango ya kutosha angepunguza huu ujinga na watanzania fanyeni kamawanachofanya usa
 
Nashauri akatwe mshahara wa mwaka mmoja kwa vile hakuwa kazini - literally !!.
 
Hii kweli inauma.Sasa Watz kuna mpango gani na hizo safari?Tuambieni tutawasaidieni japo kwa mbali.
 
Moderator!
Kama unavyojua raisi wetu Jakaya Kikwete kila kukicha safari za kwenda nje ya nchi haziishi. In average anasafiri at least kwa wiki mara moja kwenda nje ya Tanzania.
Cha ajabu kila taarifa ya safari ya huyu bwana mkubwa ikianikwa hapa jamvini immediately umekuwa unaitoa ama unai-combine na threads za safari zake za nyuma. Kwa nini usiache kila thread yenye safari yake ijitegemee?
Mfano: Jana hapa jamvini iliwekwa thread ya JK kuelekea Namibia next Monday, tayari umeshainyofoa jamvini na kui-combine na threads za nyuma. Kwa nini usiache kila safari iwe na thread yake hata kama hizo safari zitafika 1,000,000????
Ama hamtaki mkuu wa nchi kuambiwa ukweli kuhusu safari za nje ya nchi zisizoisha wala kuwa na tija?
Nawasilisha
 

Mimi niliomba na naomba tena iwekwe kwenye sticky kama trip counter.
 
Kumbukeni maneno ya baba wa taifa aliyoyasema wakati alipofanya press conference pale Mlimani kuhusu NYUFA KATIKA UONGOZI WA NCHI : alituonya lakini hatukusikia.
 
Acheni kumuonea gere prezidaa!!!

Yeye kwenye CV yake ameweka hobbies zake ni safari moja wapo!! Sasa swali ni kwenu kwani wakati anagombea mweaka 2005 hamkuona kwenye CVii na mkamkataa!!!

Acheni ale bata zake, towards 2015!!!
 
Mkuu kwa kweli kama Watanzania kazi tunayo kwa kuwa na rais mtalii.
 
Nadhani lengo la mods si baya, ameiweka kama special thread! Nashauli hii thread iende kwa mtindo huuhuu mpaka siku ya kumuaga huyu vasco da gama hii itasaidia kuwa na ushahidi wa kutosha siku ya kumkabidhi cheti chake cha kutambua mchango wake kwa taifa kwa kuvunja recod ya dunia ya kusafiri safari nyingi zaidi nje ya tz zisizo na mafaa!
 
Bajeti ya Matumizi ya Ofisi ya Rais kwa mwaka wa fedha 2011/2012 ni Shs. bilioni 139 kama sikosei. Hii figure haina mnyambulisho. Kwa hiyo hapo akitaka kusafiri sawa, akitaka atoe Shs. bilioni 20 kwa wajasiriamali ziitwe MABILIONI YA JK napo pia sawa. Hakuna mtu wa kumuuliza kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

Kumbukeni, zinahitajika Shs. bilioni 3 tu ili kila mwanafunzi wa shule ya msingi na sekondari nchini akae kwenye dawati. Ningekuwa mimi ndio Rais ningemega kutoka kwenye hilo fungu ''nikachangia madawati'' na kupata umaarufu zaidi.
 
Rais wetu kipenzi cha wengi na chaguo la Mungu leo kahamia Namibia kuendelea na zoezi lake la kufuturisha wakati huu wa mfungo mtukufu alikoalikwa kwenye mkutano wa wenyeviti wa vyama vilivyotawala muda mrefu tangu uhuru katika nchi za afrika akiliacha taifa likiangamia kwa ukosefu wa mafuta
 
AS USUAL MR. PRESIDENT TO TRAVEL, I HEARD DA NWZ HE AT NAMIBIA. Whe is he making more safaris while we are in FUEL SHORTAGE without his speech?
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
hata sisi tunaweza kumpangia sema bado tumelala angekuwa kila akitaka kuondoka au kurudi anatukuta uwanja wa ndege na mabango ya kutosha angepunguza huu ujinga na watanzania fanyeni kamawanachofanya usa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…