Safari City Project Arusha: Wapi tumekosea kama nchi?

Safari City Project Arusha: Wapi tumekosea kama nchi?

Miradi kadha ya Kikwete ilitupiliwa mbali ikiwemo ya Kigamboni, Arusha Satellite City, majengo ya Kawe, Mchuchuma na Liganga, Malagarasi Hodro power n.k.

To be honest with you, nakubaliana na uamuzi wa kusitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo kwani pale tungeingizwa mkenge mkali sana kama walivyoingizwa wa-China na Waingereza walipowaachia Hong Kong na Macau.

Sasa basi, kama yeye alivyoitelekeza miradi ya mwenzake, asitegemee kuona mwenzake atakayekuja kumaliza miradi yake yote kwa ukamilifu. Si ajabu SGR ikaishia Tabora tu au ikapelekwa Kigoma ambako ndio kwenye biashara kubwa. Au akaja akayauza madège yote baada ya kuona kuwa labda hayajiendeshi.

Ningependa kungekuwa na continuation ya miradi iliyoasisiwa na raisi anayeondoka kuliko kuiona mijumba ya NSSF na NHC ikioza bila kujali pesa ya walipa kodi iliyotumika. Miradi mipya ya awamu ya tano nai-support na hata ndege nimepanda, ila tu, ingependeza kama angemalizia miradi aliyoacha mwenzake. Na hii ndio maana halisi ya kupokezana kijiti.
 
Hiyo miradi ingekua mwanza au popote kandaya ziwa ingeendelea.
Mbona Mwanza kasitisha ujenzi wa soko kuu la kisasa, stand ya mabasi ya kisasa ambayo ni miradi muhimu zaidi kuliko hizo nyumba za matajiri! Na penyewe utasema ingekuwa wapi asingesitisha?!
 
Habari wana jamvi,

Miaka ya 2015-2016 shirika la nyumba la taifa(NHC) lilikuja na plan ya kulifanya jiji la Arusha kuwa miongoni mwa majiji yenye mvuto Afrika.

Wakaja na kitu kinaitwa safari city Arusha au Satellite City, ambapo wangejenga hotels, shopping malls, kumbi za mikutano, makazi bora kwa ajili ya apartment, maduka ya biashara, barabara za kiwango cha juu, maji, umeme pamoja na mambo mengine mengi. Kwa matarajio yao walisema mradi ungeisha ndani ya miaka 3 lakini mpaka leo 2020, haijulikani shirika walifia wapi na mradi wao.

Maana walichofanya ni kujenga tu nyumba zisizozidi 50 wakisema eti ni za mfano na kuwaambia wananchi wanunue viwanja badala ya (NHC) kama shirika wao ndo wajenge nyumba wauze ili waweze kuliingizia taifa pesa

Je, ile plan yao ya mara ya kwanza waliachana nayo? Kama kuna anaejua chochote kuhusu hili jambo atusaidie sisi tusiofahamu maana ata Kenya wana project kama hiyo(Konza City project) nao pia mpaka sasa wamejenga jengo moja tu toka mwaka 2013.

View attachment 1500492View attachment 1500494
Tuna mtu mwenye maamuzi mabaya sana, mkabila na mwenye wivu hata ndani ya nchi yake. Ukimsikiliza anavyoongea utamjua ni mtu gani. Miradi mingi ameiua kwasababu tu haipo kwake. Anashindwa kuelewa miaka 5 ni kesho tu.
Hiyo project ni moja ya projects nyingi ( ikiwemo ya Dungu residents, Dege eco Village etc) ambayo proposal yake iliandaliwa toka awamu ya JK lakini imekuja kula mweleka baada ya awamu ya JPM kuingia madarakani!

Shida kubwa ni kukosa visión ya kitaifa ktk sekta mbalimbali bila kujali utawala utakaokuwepo madarakani, kwasbb hio miradi yote imefeli/kusitishwa kwa kutokupewa kipaumbele na utawala huu kama ulivyomsikia Mh Jpm alishatoa maelekezo kwa haya mashirika kugeukia upande wa viwanda kama dirá kuu ya utawala wake na kuachana na majumba.
Mwenye nchi si aliufurumusha uongozi wa nhc? Unajua tena, wengine wote ni wezi na hawawezi kufanya mambo, ila kila kitu ni yeye tu!
Tatizo Jiwe, sekta yote ya ujenzi imedumaa kuanzia mtu mmoja mmoja, mashirika, taasisi binafsi n.k.

Hata Dar sasa zile skyscrapers alizoacha Jakaya zimejengwa au kuanza kujengwa ndio hizo hizo zilizobaki. Zilizokuwa proposed na mashirika ya umma zote zimepigwa marufuku.
Kwaiyo ulitaka akubali ule wa bagamoyo port wa miaka 99?
Au mrad upi
Luoman,

Kama nchi tulitakiwa tuwe na plan ya kujenga miji ya kisasa kama hii miaka 30 iyopita, matokeo yake ni ujenzi holela,open space zote tumeuza zimejengwa petrol station au pub, huwa najuliza hivi hawa viongozi wetu huwa hawatembei huko dunia kuona miji ya wenzetu njisi ilivyopangwa vizuri.
Luoman,

Mkuu kulikuwa na project mbili kama sikose Safari city ambayo ndio ilikuwa ianze ingefuatiwa na Sattelite city ambayo ilikuwa ijengwe USA. Kusema kweli hizo project zingekamilika zingefanya jiji la Arusha kuwa na hadhi ya kitali, Arusha ya sasa haifanani na hadhi yake.

kuna mji wa nchi jirani kwa sasa umekuwa kivutio kutokana na usafi na mpangilio wa majengo, kama NHC wangemaliza project zao basi na sisi tungekuwa na cha kujivunia katika majiji yetu mfano ni Dodoma tumeona kazi inayofanyika soon litakuwa jiji la mfano nashauri kuwe na project kubwa sana ya kupanda miti hususani kandokando ya barabara au katikati ya barabar kwa zile barabara pana, ikiwezekana kuwe na kampuni itakayohusika na upandaji na usimamizi wa miti hiyo tena kama itapendeza hiyo tenda wapewe JKT maana kazi zao huwa ni bora siku zote.
Hiyo miradi ingekua mwanza au popote kandaya ziwa ingeendelea.
 
Kukosa Vision ya kitaifa hilo ndio jibu KUU.

Bila shaka na yeye anajua kama alivyositisha miradi ya watangulizi nae wakiingia wengine madarakani hio miradi yake wataisitisha tu ndio maana anakwambia nimeamua kugombea urais tena ili nimalizie miradi niliyoianza maana sioni wakuiendeleza. Hahah.
Wacha aikamilishe tu.
 
Tatizo Jiwe, sekta yote ya ujenzi imedumaa kuanzia mtu mmoja mmoja, mashirika, taasisi binafsi n.k.

Hata Dar sasa zile skyscrapers alizoacha Jakaya zimejengwa au kuanza kujengwa ndio hizo hizo zilizobaki. Zilizokuwa proposed na mashirika ya umma zote zimepigwa marufuku.
Wewe skyscrapers zinakusaidia nini? Huoni ni busara kutekeleza miradi inayogusa watu wengi?
 
Sasa nyie mnataka papaa aweke ela kwe maproject walioanzisha wenzao. Unajua fika project km izo watu wameshalenga wanakulaje pesa. Sasa ni lazima jamaa azipige stop aanzishe za kwake ale na wenzake.
Hi miradi ilikuwa ni chocho za kupiga fedha. Unaambiwa kiwanja cha bei ya 20 Milioni kilikuwa kinauzwa kwa zaidi ya 50 milioni.
 
Kusema ukweli Jpm ameivuruga sana nchi,yaani kuna miradi mingi sana imesimama bila sbb za msingi,amesahau kabla ya mkapa na kikwete walikuwa wanaenda kwao kanda ya ziwa kupitia Nairobi Kenya. Wenzake wamemjengea barabara lkn Leo anaingia madarakani nakutaka kutuaminisha kuwa wenzake hawajafanya lolote.
 
Hakuamishia ATC ofisini kwake, alijua akinunua ndege kwa jina la ATCL zitataifishwa na wadai kwa aababu ATCL ina madeni ya kipumbavu yasiyolipika aliyoacha mtu kama MATAKA na wenzake.

Kwa hyo ndege zimenunuliwa na serikali wakazikodishia ATCL kukwepa hilo, na waliliongeleaga mwanzoni kabisa sema Watz tuu wajuaji sana na tunapenda kushikilia kitu kimoja hata kama hakina ukweli
Kwani Serikali airuhusiwi kukaguliwa?
 
Yeye Mwanza haimuhusu,kunakomuhusu ni chato tu!!
Mbona Mwanza kasitisha ujenzi wa soko kuu la kisasa, stand ya mabasi ya kisasa ambayo ni miradi muhimu zaidi kuliko hizo nyumba za matajiri! Na penyewe utasema ingekuwa wapi asingesitisha?!
 
Hi miradi ilikuwa ni chocho za kupiga fedha. Unaambiwa kiwanja cha bei ya 20 Milioni kilikuwa kinauzwa kwa zaidi ya 50 milioni.
Sasa hivi viwanja vinapatikana huko kwa shilingi ngapi?
 
Hi miradi ilikuwa ni chocho za kupiga fedha. Unaambiwa kiwanja cha bei ya 20 Milioni kilikuwa kinauzwa kwa zaidi ya 50 milioni.
sasa hivi kinavyouzwa kwa hiyo mil.20 wewe na mke wako mumenunua vingapi? umaskini mbaya sana..Soko lilikuwa linapanga bei na vinauzika shida iko wapi maana uchumi ulikuwa vizuri,leo je
 
Hakuamishia ATC ofisini kwake, alijua akinunua ndege kwa jina la ATCL zitataifishwa na wadai kwa aababu ATCL ina madeni ya kipumbavu yasiyolipika aliyoacha mtu kama MATAKA na wenzake.

Kwa hyo ndege zimenunuliwa na serikali wakazikodishia ATCL kukwepa hilo, na waliliongeleaga mwanzoni kabisa sema Watz tuu wajuaji sana na tunapenda kushikilia kitu kimoja hata kama hakina ukweli
Deni ni deni hata uhamishie nyumbani kwako, utadaiwa tuu, dawa ni kulipa, mbona kule Canada na South Afrika walizidaka?
 
Miradi mingi ya NHC na mashirika ya pension ilikuwa ni upigaji tu. Haikuwa kibiashara. Numba ya 30m wao wanajenga kwa 50-60.
 
Mbona Mwanza kasitisha ujenzi wa soko kuu la kisasa, stand ya mabasi ya kisasa ambayo ni miradi muhimu zaidi kuliko hizo nyumba za matajiri! Na penyewe utasema ingekuwa wapi asingesitisha?!
Hiyo miradi ya masoko na stend pesa yake na utekelezaji wake ulishaanza na ni kwa awamu Mwanza awamu hii haikuwepo, kumbuka ni pesa za wafadhili hizo. Miradi kwenye awamu hii ilikuwa Morogoro (soko na stend), Katavi (stend), Dar (stend), Iringa (stend) etc
 
Back
Top Bottom