Safari City Project Arusha: Wapi tumekosea kama nchi?

Luoman

Member
Jul 2, 2020
20
44
Habari wana jamvi,

Miaka ya 2015-2016 shirika la nyumba la taifa(NHC) lilikuja na plan ya kulifanya jiji la Arusha kuwa miongoni mwa majiji yenye mvuto Afrika.

Wakaja na kitu kinaitwa safari city Arusha au Satellite City, ambapo wangejenga hotels, shopping malls, kumbi za mikutano, makazi bora kwa ajili ya apartment, maduka ya biashara, barabara za kiwango cha juu, maji, umeme pamoja na mambo mengine mengi. Kwa matarajio yao walisema mradi ungeisha ndani ya miaka 3 lakini mpaka leo 2020, haijulikani shirika walifia wapi na mradi wao.

Maana walichofanya ni kujenga tu nyumba zisizozidi 50 wakisema eti ni za mfano na kuwaambia wananchi wanunue viwanja badala ya (NHC) kama shirika wao ndo wajenge nyumba wauze ili waweze kuliingizia taifa pesa

Je, ile plan yao ya mara ya kwanza waliachana nayo? Kama kuna anaejua chochote kuhusu hili jambo atusaidie sisi tusiofahamu maana ata Kenya wana project kama hiyo(Konza City project) nao pia mpaka sasa wamejenga jengo moja tu toka mwaka 2013.

12abc_i_07.jpg
12abc_i_06.jpg
 
Hiyo project ni moja ya projects nyingi ( ikiwemo ya Dungu residents, Dege eco Village etc) ambayo proposal yake iliandaliwa toka awamu ya JK lakini imekuja kula mweleka baada ya awamu ya JPM kuingia madarakani!

Shida kubwa ni kukosa visión ya kitaifa ktk sekta mbalimbali bila kujali utawala utakaokuwepo madarakani, kwasbb hio miradi yote imefeli/kusitishwa kwa kutokupewa kipaumbele na utawala huu kama ulivyomsikia Mh Jpm alishatoa maelekezo kwa haya mashirika kugeukia upande wa viwanda kama dirá kuu ya utawala wake na kuachana na majumba.
 
Kukosa Vision ya kitaifa hilo ndio jibu KUU.

Bila shaka na yeye anajua kama alivyositisha miradi ya watangulizi nae wakiingia wengine madarakani hio miradi yake wataisitisha tu ndio maana anakwambia nimeamua kugombea urais tena ili nimalizie miradi niliyoianza maana sioni wakuiendeleza. Hahah.
 
Tatizo Jiwe, sekta yote ya ujenzi imedumaa kuanzia mtu mmoja mmoja, mashirika, taasisi binafsi n.k.

Hata Dar sasa zile skyscrapers alizoacha Jakaya zimejengwa au kuanza kujengwa ndio hizo hizo zilizobaki. Zilizokuwa proposed na mashirika ya umma zote zimepigwa marufuku.
 
kukosa Vision ya kitaifa hilo ndio jibu KUU.

Bila shaka na yeye anajua kama alivyositisha miradi ya watangulizi nae wakiingia wengine madarakani hio miradi yake wataisitisha tu ndio maana anakwambia nimeamua kugombea urais tena ili nimalizie miradi niliyoianza maana sioni wakuiendeleza. Hahah.
Kwaiyo ulitaka akubali ule wa bagamoyo port wa miaka 99?
Au mrad upi
 
Tatizo Jiwe, sekta yote ya ujenzi imedumaa kuanzia mtu mmoja mmoja, mashirika, taasisi binafsi n.k.

Hata Dar sasa zile skyscrapers alizoacha Jakaya zimejengwa au kuanza kujengwa ndio hizo hizo zilizobaki. Zilizokuwa proposed na mashirika ya umma zote zimepigwa marufuku.
Ukimwambia mwenyewe atakujibu ule ulikua ni uchumi feki, huu sasa ndio halisi.
 
Yani kwa hiyo picha ndo ingechukua miaka 3 kukamilika? Mbona Kama uongo huo.
 
Kwa hio ndio ikamfanya aihamishie na Atcl ofisin kwakei ili isikaguliwe mahesabu na CAG sio?
Hakuamishia ATC ofisini kwake, alijua akinunua ndege kwa jina la ATCL zitataifishwa na wadai kwa aababu ATCL ina madeni ya kipumbavu yasiyolipika aliyoacha mtu kama MATAKA na wenzake.

Kwa hyo ndege zimenunuliwa na serikali wakazikodishia ATCL kukwepa hilo, na waliliongeleaga mwanzoni kabisa sema Watz tuu wajuaji sana na tunapenda kushikilia kitu kimoja hata kama hakina ukweli
 
Acha ujinga wewe unachanganya madesa tu.

Wewe unaongelea Serikali kuikodishia ATCL hizo ndege,mimi naongelea Atcl kuhamishiwa ofisi kuu.

Jaribu kua unasoma kwa umakini.
 
Luoman,

Kama nchi tulitakiwa tuwe na plan ya kujenga miji ya kisasa kama hii miaka 30 iyopita, matokeo yake ni ujenzi holela,open space zote tumeuza zimejengwa petrol station au pub, huwa najuliza hivi hawa viongozi wetu huwa hawatembei huko dunia kuona miji ya wenzetu njisi ilivyopangwa vizuri.
 
Luoman,

Mkuu kulikuwa na project mbili kama sikose Safari city ambayo ndio ilikuwa ianze ingefuatiwa na Sattelite city ambayo ilikuwa ijengwe USA. Kusema kweli hizo project zingekamilika zingefanya jiji la Arusha kuwa na hadhi ya kitali, Arusha ya sasa haifanani na hadhi yake.

kuna mji wa nchi jirani kwa sasa umekuwa kivutio kutokana na usafi na mpangilio wa majengo, kama NHC wangemaliza project zao basi na sisi tungekuwa na cha kujivunia katika majiji yetu mfano ni Dodoma tumeona kazi inayofanyika soon litakuwa jiji la mfano nashauri kuwe na project kubwa sana ya kupanda miti hususani kandokando ya barabara au katikati ya barabar kwa zile barabara pana, ikiwezekana kuwe na kampuni itakayohusika na upandaji na usimamizi wa miti hiyo tena kama itapendeza hiyo tenda wapewe JKT maana kazi zao huwa ni bora siku zote.
 
Kukosa Vision ya kitaifa hilo ndio jibu KUU.

Bila shaka na yeye anajua kama alivyositisha miradi ya watangulizi nae wakiingia wengine madarakani hio miradi yake wataisitisha tu ndio maana anakwambia nimeamua kugombea urais tena ili nimalizie miradi niliyoianza maana sioni wakuiendeleza. Hahah.
Hiyo miradi ingekua mwanza au popote kandaya ziwa ingeendelea.
 
Back
Top Bottom