Safari City Project Arusha: Wapi tumekosea kama nchi?

Safari City Project Arusha: Wapi tumekosea kama nchi?

Hi miradi ilikuwa ni chocho za kupiga fedha. Unaambiwa kiwanja cha bei ya 20 Milioni kilikuwa kinauzwa kwa zaidi ya 50 milioni.
Mbona hata sasa wanapiga? JK mnasema serikali yake ilikuwa ya wapigaji, but watu walikuwa na pesa na serikalini mambo yalikuwa yanaenda kila kona.
 
Mbona hata sasa wanapiga? JK mnasema serikali yake ilikuwa ya wapigaji, but watu walikuwa na pesa na serikalini mambo yalikuwa yanaenda kila kona.
Sasa hivi ndio zaidi.
Tofauti nikuwa wapigaji wamebadilika,hawa wa sasa ni wapya na wanapiga masafa marefu.
 
Hiyo miradi ya masoko na stend pesa yake na utekelezaji wake ulishaanza na ni kwa awamu Mwanza awamu hii haikuwepo, kumbuka ni pesa za wafadhili hizo. Miradi kwenye awamu hii ilikuwa Morogoro (soko na stend), Katavi (stend), Dar (stend), Iringa (stend) etc
Mwanza pesa ishakuja zamaaani wakakaa nazo tu pale wakibishana standi ipanuliwe pale pale au iamishiwe nyashishi au usagara, matokeo yake baada ya kuona pesa zinazengeazengea mzee baba akazinyakua na kuzihamishia serikali kuu kwenye miradi mingine.
 
Ipo haja ya kuangalia upya hii project kwa kina.

Kama kulikuwa na upigaji uhakiki wa mahesabu ufanyike mradi uendelee.

Ni vyema pia shirika likawa na nyumba za bei halisia, huwezi muuzia mtu kajumba ka vyumba viwili kwa millioni mia na zaidi, haina uhalisia kabisa.
 
Habari wana jamvi,

Miaka ya 2015-2016 shirika la nyumba la taifa(NHC) lilikuja na plan ya kulifanya jiji la Arusha kuwa miongoni mwa majiji yenye mvuto Afrika.

Wakaja na kitu kinaitwa safari city Arusha au Satellite City, ambapo wangejenga hotels, shopping malls, kumbi za mikutano, makazi bora kwa ajili ya apartment, maduka ya biashara, barabara za kiwango cha juu, maji, umeme pamoja na mambo mengine mengi. Kwa matarajio yao walisema mradi ungeisha ndani ya miaka 3 lakini mpaka leo 2020, haijulikani shirika walifia wapi na mradi wao.

Maana walichofanya ni kujenga tu nyumba zisizozidi 50 wakisema eti ni za mfano na kuwaambia wananchi wanunue viwanja badala ya (NHC) kama shirika wao ndo wajenge nyumba wauze ili waweze kuliingizia taifa pesa

Je, ile plan yao ya mara ya kwanza waliachana nayo? Kama kuna anaejua chochote kuhusu hili jambo atusaidie sisi tusiofahamu maana ata Kenya wana project kama hiyo(Konza City project) nao pia mpaka sasa wamejenga jengo moja tu toka mwaka 2013.

View attachment 1500492View attachment 1500494
ulikua mradi wa mabeberu au nasema uongo ndugu zanguuu
 
Huwa naona pale TRA watu wana hiyo mikataba ya Safari City wakilipia ushuru.
Ila NHC walipewa onyo kwamba wasiwe na miradi mingi isiyomalizika, waweke focus kwenye mradi mmoja na kuumaliza, kisalha wahamie mwingine
 
Kwaiyo ulitaka akubali ule wa bagamoyo port wa miaka 99?
Au mrad upi
Una ambiwa sekta ya ujenzi ww una leta bandari .... Ktk sekta ya ujenzi nchi kuwa na miji ambayo ni planned ni kitu ambacho nchi zilizo endelea na hata baadhi za africa hapa hapa SSACs wana ipa kipaumbele ...
 
Miradi kadha ya Kikwete ilitupiliwa mbali ikiwemo ya Kigamboni, Arusha Satellite City, majengo ya Kawe, Mchuchuma na Liganga, Malagarasi Hodro power n.k.

To be honest with you, nakubaliana na uamuzi wa kusitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo kwani pale tungeingizwa mkenge mkali sana kama walivyoingizwa wa-China na Waingereza walipowaachia Hong Kong na Macau.

Sasa basi, kama yeye alivyoitelekeza miradi ya mwenzake, asitegemee kuona mwenzake atakayekuja kumaliza miradi yake yote kwa ukamilifu. Si ajabu SGR ikaishia Tabora tu au ikapelekwa Kigoma ambako ndio kwenye biashara kubwa. Au akaja akayauza madège yote baada ya kuona kuwa labda hayajiendeshi.

Ningependa kungekuwa na continuation ya miradi iliyoasisiwa na raisi anayeondoka kuliko kuiona mijumba ya NSSF na NHC ikioza bila kujali pesa ya walipa kodi iliyotumika. Miradi mipya ya awamu ya tano nai-support na hata ndege nimepanda, ila tu, ingependeza kama angemalizia miradi aliyoacha mwenzake. Na hii ndio maana halisi ya kupokezana kijiti.
Inafikirisha sana
 
Hakuamishia ATC ofisini kwake, alijua akinunua ndege kwa jina la ATCL zitataifishwa na wadai kwa aababu ATCL ina madeni ya kipumbavu yasiyolipika aliyoacha mtu kama MATAKA na wenzake.

Kwa hyo ndege zimenunuliwa na serikali wakazikodishia ATCL kukwepa hilo, na waliliongeleaga mwanzoni kabisa sema Watz tuu wajuaji sana na tunapenda kushikilia kitu kimoja hata kama hakina ukweli

Huyo alie iachia ATCL madeni yupo gereza gani??
 
Msimamizi mkuu wa NHC amerudishwa ni wakati wake sasa kuiangalia miradi yake iliyosimama akiona ina maslahi na Taifa aiendeleze. Ninapenda kuona miji yetu ikiwa misafi na yenye kuvutia. Mipango miji wangeweka sheria kila anayejenga ahakikishe anaacha sehemu ya kupanda walau miti miwili au mitatu kwa ajili ya kuifanya nchi iwe ya kijani.
 
Back
Top Bottom