SAFARI CHANNEL IMEANZA KUHARIBU MAMBO.

Tyupa

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
802
653
Channel mpya ya Safari Channel ilipoanza ilionekana kama chaneli tishio kwa sababu watu wengi sana wanapenda kuangalia wanyama na matukio ya utamaduni wetu.Watu wengi awali walikuwa waking alia chaneli za wanyama za nje lakini baada ya kufunguliwa hii chaneli ya kwetu watu walihamia nyumbani.Baada ya muda mfupi tayari waandaji wa vipindi vya chaneli hii wameanza kuharibu kwa kasi ya ajabu na tayari watu wameanza kurudi kwenye chaneli zao za nje.Vipindi vingi vya Safari Chaneli vinarudiwa rudiwa mno hadi inakuwa chukuzi.Kuna makabila mengi Tanzania ambayo yote yana utamaduni wao lakini nafasi hayapewi.Mikanda ya wanyama iko mingi na mizuri mno lakini yote haioneshwi kamwe.Waandaji wanashindwa hata kumuenzi mzungu alietengeneza mkanda mashuhuri wa wanyama uliojulikana kwa jina la SERENGETI SHALL NEVER DIE.Huyu mzungu simkumbuki jina lakini katika harakati zake za kupiga picha za wanyama katika mbuga ya Serengeti kwa kutumia helicopter yake binafsi alipata ajali baada ya ndege kugongwa na mapopo na kuanguka na yeye alifarika dunia.Baada ya ndugu zake kufika toka Ulaya waliamua azikwe Tanzania na kujengewa mnara wa kumbukumbu pale pale alipoangukia na ndege yake.Mtoto wake mkubwa katika kutoa neno kwa serikali ya Tanzania alitamka neno la ajabu na la kishujaa mno.Nanukuu alivyosema mtoto huyo, " Baba amekufa lakini Serengeti haitakufa.Alichukua mikoba ya baba yake na kumalizia kazi ya kupiga picha wanyama.Filamu yake aliita SERENGETI SHALL NOT DIE!!.Ni picha iliovutia mno watazamaji kipindi kile.Waandaji wa vipindi vya Safari Chaneli sidhani hata kama wanafahamu kumbukumbu hii muhimu na si ajabu hata nakala ya ya picha hawana.Ni aibu kufuta kumbukumbu ya jinsi hii.Nawasihi itafuteni ili vijana wa sasa waweze kujifunza kutoka kwenye mkanda huo wa kusisimua.Kwa sasa time choke mno na na mavipindi ya kurudia yale yale kila siku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom