Ukitembelea Hifadhi ya Taifa Arusha hutatamani kurudi nyumbani

Funa the Great

Senior Member
Aug 1, 2022
160
271
Septemba 03, 2023, hii ilikuwa ni tarehe ambayo nilipata nafasi ya kuwapeleka watalii ndani ya hifadhi ya taifa Arusha inayopatikana mkoa wa Arusha. Hifadhi ambayo Mfalme Charles wa III na malkia wake walikanyaga ndani ya ardhi iyo.

Ni siku ambayo iliacha kumbukumbu kwa kila aliyekwepo hakuna aliyetamani kurudi nyumbani kwa wakati ule zaidi ya kuendelea kujionea mengi juu ya uumbaji wa mwenyezi Mungu lakini ni vile hawakuwa na namna kwa kuwa package na budget ya safari yao ilikuwa ni ya siku moja yaani DAY TRIP.
IMG_20231022_115426_397.jpg


Tulitembelea karibia vivutio vyote vinavyopatikana ndani ya hifadhi iyo ikiwemo,

1. Maporomoko ya Maji Tululusia
2. Serengeti ndogo
3. Uwanja wa mbogo
4. Ziwa Momella
5. Creta ya Ngurdoto
6. Museum ya Ngurdoto
IMG_20230908_171617.jpg
IMG_20230909_003141.jpg

Vivutio vyote hapo nimevielezea kwenye makala ya "YALIYOJIFICHA JUU YA HISTORIA YA HIFADHI YA TAIFA ARUSHA NA MAAJABU YA VIVUTIO VYAKE" kama hujapata nafasi ya kupitia unaweza pitia.

Tuliona wanyama kwa kutumia magari na kutembea kwa miguu na kuwapiga Picha kwa ukaribu.

IMG_20230909_014333.jpg
IMG_20230909_012456.jpg
IMG_20230909_014122.jpg


Tanzania imebarikiwa kuwa na maeneo mengi yenye kuvutia una kila sababu ya kujipa nafasi na kwenda kutembelea vivutio vya utalii. Acha kujifungia ndani kuna mengi unapishana nayo.

IMG_20230924_174417.jpg
IMG_20230909_011857.jpg
IMG_20230909_005048.jpg
IMG_20230909_013035.jpg


KWA HUDUMA ZA SAFARI ZA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII CHEKI NAMI +255622174613.

SAFARI ZA MARAFIKI, FAMILIA, COUPLES, SHULE/VYUO, KIOFISI N.K

KARIBU TUTEMBELEE HIFADHI YA TAIFA MIKUMI NA MAPOROMOKO YA MAJI CHOMA NDANI YA MKOA WA MOROGORO KUANZIA TAREHE 16-17 DECEMBER 2023. MAELEZO ZAIDI +255622174613
 
Babu hao uliopost picha zao umewaomba ruhusu au unakanyaga wakikubana mbavu uanze kulalamika watu hawana jema...?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom