Saed Kubenea: Sina mpango wa kuondoka CHADEMA

Mimi sasa hivi magazeti sinunui tena wala sisikilizi habari za magazeti redioni maana habari zao zinaonekana kabisa zina" maelekezo kutoka juu"
 
Taarifa kwa umma

NIMEONA picha yangu kwenye gazeti la leo Jumanne la MWANANCHI likinihusisha mimi na kutaka kuhama chama changu na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Napenda kueleza masikitiko yangu kuona gazeti lililokuwa linaheshimika katika jamii, linajiingiza katika kuandika habari ambazo chanzo chake ni mitandao ya kijamii ya Whats App na Jamii Forum na zinazosambazwa na watu wenye nia ovu dhidi yangu.

Narejea tena na tena, kwamba sina mpango wa kuondoka Chadema. Sijawahi kuzungumza na mtu yoyote yule wa CCM kuwa nataka kujiunga na chama chao.

Hii ni kwa sababu, mpaka sasa, mimi binafsi, sijaona sababu zinazojitosheleza kunishawishi kuondoka Chadema na kujiunga na chama kingine.

Ninafahamu wazi kuwa wapo watu ndani ya Chadema wanaotaka nikihame chama changu, ili kukidhi maslahi yao binafsi.

Napenda kuwahakikishia kuwa siondoki na hakuna wa kuniondoa.

Wanaodhani kuwa mimi kuwamo kwangu huku ni kero kwao, basi nawaomba waondoke wao.

Watuachie sisi chama tutakaosalia. Tunaahidi tutakijenga, kikiimarisha na kukiendeleza hadi kuelekea kushika dola.

Nitaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa Chadena na nitaendelea kuwatumikia wananchi wangu wa Ubungo, hadi nimalize kipindi changu cha Ubunge.

Kuhusu gazeti la MWANANCHI, naomba kulishauri mambo mawili makuu:

Liache kuandika habari za kuokoteza juu yangu zinazohusu madai ya kuhama chama.

Litumie muda huu, kufanya uchunguzi yakinifu wa wapi alikofichwa; na au nani waliomteka na kumshikilia mwandishi wao wa habari mahiri za uchunguzi aliyetoweka takribani miezi mitano iliyopita, huko Kibiti, mkoani Pwani.

Hiyo ndio kazi ya kitume ambayo gazeti kama MWANANCHI linapaswa kuifanya.

Saed Kubenea, mbunge wa Ubungo.
Kwani hakuna waliowahi kukanusha hivi na kesho yake wakahama?
 
Nchi hii inavurugwa na Jiwe na huenda sasa kaanza kutumia media katika njama zake hizo.
Wewe sasa umezidi, lililoandika ni gazeti ambalo hata wewe ulikuwa unalisifia.

Kubenea hii ni mara ya 5 anakanusha hizi habari, na leo ameweka wazi kuwa kuna watu ndani ya CHADEMA HAWAMTAKI na wanafanya kila mbinu kumchonganisha na chama chake, mbona hilo hulizungumzii.
 
Kubenea ana haki ya kulifungulia mashataka hili gazeti, lakini ameonyesha msimamo wake mara nyingi, na leo ameweka uwazi kuwa kuna mbinu ndani ya chama chake ya kumharibia jina, na sio ccm ama serekali, amesema haja zungumza wala hajafuatwa na ccm kuhusu kuhama, ila kuna wasiomtaka ndani ya chadema.
 
Afadhali amewaumbua.. Hawezi kuwa shoga huyu

Ila angefunguka zaidi aliposema kuna wanaotaka aondoke. Ina maana kuna watumishi wa sisiemu ndani ya Cdm??
 
Taarifa kwa umma

NIMEONA picha yangu kwenye gazeti la leo Jumanne la MWANANCHI likinihusisha mimi na kutaka kuhama chama changu na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Napenda kueleza masikitiko yangu kuona gazeti lililokuwa linaheshimika katika jamii, linajiingiza katika kuandika habari ambazo chanzo chake ni mitandao ya kijamii ya Whats App na Jamii Forum na zinazosambazwa na watu wenye nia ovu dhidi yangu.

Narejea tena na tena, kwamba sina mpango wa kuondoka Chadema. Sijawahi kuzungumza na mtu yoyote yule wa CCM kuwa nataka kujiunga na chama chao.

Hii ni kwa sababu, mpaka sasa, mimi binafsi, sijaona sababu zinazojitosheleza kunishawishi kuondoka Chadema na kujiunga na chama kingine.

Ninafahamu wazi kuwa wapo watu ndani ya Chadema wanaotaka nikihame chama changu, ili kukidhi maslahi yao binafsi.

Napenda kuwahakikishia kuwa siondoki na hakuna wa kuniondoa.

Wanaodhani kuwa mimi kuwamo kwangu huku ni kero kwao, basi nawaomba waondoke wao.

Watuachie sisi chama tutakaosalia. Tunaahidi tutakijenga, kikiimarisha na kukiendeleza hadi kuelekea kushika dola.

Nitaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa Chadena na nitaendelea kuwatumikia wananchi wangu wa Ubungo, hadi nimalize kipindi changu cha Ubunge.

Kuhusu gazeti la MWANANCHI, naomba kulishauri mambo mawili makuu:

Liache kuandika habari za kuokoteza juu yangu zinazohusu madai ya kuhama chama.

Litumie muda huu, kufanya uchunguzi yakinifu wa wapi alikofichwa; na au nani waliomteka na kumshikilia mwandishi wao wa habari mahiri za uchunguzi aliyetoweka takribani miezi mitano iliyopita, huko Kibiti, mkoani Pwani.

Hiyo ndio kazi ya kitume ambayo gazeti kama MWANANCHI linapaswa kuifanya.

Saed Kubenea, mbunge wa Ubungo.
Hii business ya utumwa vipi mbona viti maalum hawaungi mkono juhudi za jiwe .saed well said hizi deal zao zinaangamiza taifa sio chadema katu usikubali kununuliwa kama vitisho umeshapewa sana
 
Kweli mambo hubadirika! Yani leo hii chadema ndio wanatiwa jambajamba na ccm kiasi hiki?
Habari kama hizi ilitakiwa tuwe tinaona zinasomeka hivi katika magazeti: "WABUNGE 10 WA CCM KITIMKIA UPINZANI MUDA WOWOTE"

Badala yake ni kinyume chake!
 
Back
Top Bottom