Saed Kubenea kugombea ubunge 2015 kupitia CHADEMA

Saed Kubenea kugombea ubunge 2015 kupitia CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Tatizo hapa ni 'credibility' ya mleta mwanzisha uzi katika masuala yanayoihusu CHADEMA. Hivyo ninapata shida kuitilia maanani habari hii.
 
Japo mtoa hoja utakua umetoa kwa mtazamo hasi,lkn ukwei utabaki kuwa huyu jamaa ni Jembe na hata ww unafahamu kama akigombea ubunge basi chama chenu cha magamba kitapata asilimia 0.5 ya kura zote. Karibu Kibaha kaka kura yangu unayo.
 
ukweli husemwa:

Waandishi wa habari wa bongo bana,

Kumbe kelele zote za kumfuatilia Mh.Zitto zilikuwa na malipo ya chini ya meza.

Ama kweli jambo usilolijua ni kama usiku wa giza.

Haiwezi kuwa ni habari njema kwa tasnia ya habari katika jamii. Inatufanya tuwe na wasiwasi na kile kinachoandikwa kwenye magazeti.

Kama nchi itajaa waandishi wa habari walionunuliwa kwa malipo ya chini ya meza lakini wanapiga kelele kuwa wanasimamia misingi ya uandishi wa habari, huu ni kama usaliti katika jamii.
 
Hiyo ndio demoklasia, Mimi nataka kugombea jengo la Magogoni kabla alijapangishwa kwa wanaoitwa WAWEZEKAJI
 
Kama ilivyo kwa urais hata ubunge bado hatujaanza kufikiria nani anawania wapi. Anayeliongelea leo ni mfinyu wa mawazo. Embu tudiskass kuhusu Gas na wanamtwara pia
 
KUBENEA5.JPG

Wanabodi.

Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwanahalisi Saed Kubenea, inasemekana amejapanga kugombea Ubunge Jimbo la Kibaha Mjini kupitia CHADEMA mwaka 2015. kwa hivi sasa Jimbo hilo linaongozwa na Silvestry Koka [CCM].

Hii itakuwa habari njema kwa tasnia ya habari kujiingiza katika masuala ya uongozi wa kisiasa, Kubenea kapata msukumo wa kugombea Ubunge baada ya kushauriana na Dr Slaa na kumuakikishia kuwa anaweza kushida Ubunge Jimbo la Kibaha Mjini kama akijipanga vizuri na kupata msaada wa CHADEMA.

Kila la Heri Saed Kubenea.

Asante sana mkuu Ritz kwa habari nzito hizi. Ila hapo red inaonekana hazijathibitishwa kwa hiyo ni tetesi!! Ila mkuu si alikuwa agombee kupitia SSM huko Mkuranga???!! Kwa hiyo ina maana baada ya kumchoma na tindikali na kufungia lile gazeti maarufu ameamua kuwakimbia? Tusubiri tukisogea 2015 tutasikia Mengi.
 
Tatizo hapa ni 'credibility' ya mleta mwanzisha uzi katika masuala yanayoihusu CHADEMA. Hivyo ninapata shida kuitilia maanani habari hii.
Hata mimi nimeshangaa mkuu MpigaKelele maana tetesi zilizokuwepo alikuwa anategemea kugombea kupitia SSM!!! Ila kwa hakika atashinda kama ana base kule Kibaha!!! Wanamfahamu lakini? Siasa zina mipangilio yake mkuu. Ila Koka mwisho wake wa Siasa za Ubunge ni 2015. Hatakiwi kule kabisa hata mikutano ya hadhara anaogopa na polisi walimwambia wazi!!
 
Na atakua kwenye moja ya wizara katika baraza la mawaziri 2016.Viva CDM
 
KUBENEA5.JPG

Wanabodi.

Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwanahalisi Saed Kubenea, inasemekana amejapanga kugombea Ubunge Jimbo la Kibaha Mjini kupitia CHADEMA mwaka 2015. kwa hivi sasa Jimbo hilo linaongozwa na Silvestry Koka [CCM].

Hii itakuwa habari njema kwa tasnia ya habari kujiingiza katika masuala ya uongozi wa kisiasa, Kubenea kapata msukumo wa kugombea Ubunge baada ya kushauriana na Dr Slaa na kumuakikishia kuwa anaweza kushida Ubunge Jimbo la Kibaha Mjini kama akijipanga vizuri na kupata msaada wa CHADEMA.

Kila la Heri Saed Kubenea.

acha umbea wewe............. tunajua unachokitafuta
 
Unaweweseka kupata the dream team ya 2015 eeeh
 
Amekutuma au umejituma? Ana jipya lipi analeta kwenye ubunge? Na ndoa yake na CCM itaishia wapi? Je ndiyo anaanza kampeni au anatafuta kampani? Kwanini asigombee kwao? Mara Kibaha mara Mafia who is he to think that he can win wherever he deems fit?Huyu jamaa si jembe bali amepata umaarufu kwa bahati mbaya hasa baada ya kumwagiwa tindikali. Ajaribu aone kilichomshinda bosi wake Ndimara Tegambwage. Siasa imekuwa kimbilio la kila msaka ngawira. Heri angejisomea kwanza akaachana na ukihiyo na kusaka umaarufu.
KUBENEA5.JPG

Wanabodi.

Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwanahalisi Saed Kubenea, inasemekana amejapanga kugombea Ubunge Jimbo la Kibaha Mjini kupitia CHADEMA mwaka 2015. kwa hivi sasa Jimbo hilo linaongozwa na Silvestry Koka [CCM].

Hii itakuwa habari njema kwa tasnia ya habari kujiingiza katika masuala ya uongozi wa kisiasa, Kubenea kapata msukumo wa kugombea Ubunge baada ya kushauriana na Dr Slaa na kumuakikishia kuwa anaweza kushida Ubunge Jimbo la Kibaha Mjini kama akijipanga vizuri na kupata msaada wa CHADEMA.

Kila la Heri Saed Kubenea.
 
bwana Kubenea hapewe kura zote naye ni mhanga wa ccm kamwagiwa tindikali shauri ya ukweli wake kafungiwa gazeto c zaidi ya mara moja mpeni kura za ndio akatoe ushuda wake bungeni ni mhanga huyo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom