SADC ina faida gani kwa nchi yetu?

Kwa hisani ya Gazeti la Mwananchi
.."Sadc ilianzishwa kupitia mkataba uliosainiwa Agosti 17, 1992 na wakuu wa nchi na serikali kumi na moja Tanzania ikiwamo na makao makuu yake yakiwa Gaborone, Botswana.

Tangu wakati huo, idadi ya nchi wanachama imeongezeka hadi kufikia 16 (Angola, Botswana, Comoro, DR-Congo, Eswatini, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Afrika Kusini,

Tanzania, Zambia na Zimbabwe) na kuunda soko la bidhaa na huduma la takribani watu 330 milioni.

Mtangamano wa nchi za Sadc

Chimbuko la Sadc ni mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na utawala wa mabavu wa makaburu nchini Afrika Kusini. Mapambano hayo yaliongozwa na Kundi la Nchi za Mstari wa Mbele (Frontline States) lililoanzishwa mwaka 1970, Tanzaniaikiwa taifa kiongozi wa kundi hilo. Pamoja na Tanzania, nchi nyingine zilikuwa Angola, Botswana, Lesotho, Msumbiji, Swaziland (Hivi sasa inaitwa Eswatini) na Zambia iliyojiunga miaka 10 baadaye.

Tanzania ilichukua jukumu la uongozi wa mapambano Kusini mwa Afrika kutokana na ukweli kwamba, nchi nyingi zilizounda Kundi la Nchi za Mstari wa Mbele, kijiografia, kiuchumi na kijeshi hazingeweza kuhimili vishindo vya serikali ya kibaguzi na mabavu ya Afrika Kusini bila ushiriki wa dhati na makini wa Tanzania.

Baadaye kundi hilo lilijizatiti zaidi kwa kuanzisha Jukwaa la Kuratibu harakati hizo (Sadc) ili kujenga uwezo wa kujitegemea kiuchumi na hatimaye kujigeuza tena kuwa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc). Kwa mantiki hiyo, Sadc ya sasa na siku zijazo dhima yake kuu ni maendeleo na ustawi wa jamii miongoni mwa nchi wanachama.

Kinadharia, Mtangamano wa Kikanda (Regional Integration) una hatua tano, ambazo ni eneo huru la biashara,umoja wa forodha, soko la pamoja, umoja wa kiuchumi na umoja wa kisiasa. Utekelezaji wa hatua hizo za mtangamano hutofautiana kutokana na hali ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ya nchi washiriki.
Aidha, baadhi ya jumuiya huinyambulisha hatua ya nne katika makundi madogo zaidi. Mathalani, umoja wa kifedha na sarafu moja au kuruka baadhi ya hatua kama ilivyofanyika katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iliyoanzia hatua ya umoja wa forodha.

Dhamira ya nchi za Sadc ilikuwa kuifikia hatua ya eneo huru la biashara ifikapo mwaka 2008, ikifuatiwa na umoja wa forodha(2010), kisha soko la pamoja (2015), umoja wa fedha (2016) na hatimaye sarafu moja mwaka 2018. Hali halisi ya utekelezaji inaonyesha kuwa Sadc iko hatua ya kwanza sawia na utekelezaji wa baadhi ya vipengele vya hatua ya pili. Kwa mfano, uondoaji wa viza kwa wasafiri wa nchi wanachama.

Faida za ushiriki wa Tanzania Sadc

Sera ya Taifa ya Biashara ya Tanzania inaainisha kuwa miongoni mwa nyenzo zake kuu za ukuzaji nauendelezaji mauzo nje ni mtangamano wa kikanda. Nyenzo zingine katika muktadha huu ni ushirikiano kati ya Tanzania na nchi nyingine mojamoja (bilateral co-operation) na Mikataba ya Shirika la Biashara Duniani (WTO Agreements).

Kimsingi, nyenzo hizo tatu, ikiwamo ile ya mtangamano wa kikanda, hujumuisha kuondolewa vikwazo vya kiforodha na visivyo vya kiforodha miongoni mwa nchi husika jambo ambalo huhamasisha uzalishaji, ufanyaji biashara na uwekezaji kwa jumla.Kwa kutambua dhana hiyo, takriban nchi zote za Sadc ziliondoleana ushuru wa forodha ilipofika mwaka 2012, isipokuwa kwa bidhaa chache zilizoonekana nyeti katika mapato ya kodi na ulinzi wa viwanda vichanga ambazo ushuru wa forodha uliondolewa taratibu hadi kufikia zero hivi sasa.

Sambamba na kuondoa vikwazo vya kiforodha miongoni mwa nchi wanachama, hatua zimechukuliwa pia kuondoa vikwazo visivyo vya kiforodha. Kwa mfano, taratibu za kiforodha zimerahisishwa ikiwamo uanzishwaji wa vituo vya forodha vya pamoja (one stop border posts) kama kile kilichopo Tunduma; mpakani mwa Tanzania na Zambia.

Hatua hiyo imeifaidisha Tanzania kibiashara. Mathalan, takwimu za sekretarieti ya Sadc zinaonyesha kuwa mauzo ya Tanzania katika Jumuiya yaliongezeka kwa zaidi ya maradufu, kutoka Dola za Marekani 432 milioni kwa mwaka 2007 hadi Dola 1,013 milioni mwaka 2016. Aidha, takwimu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinaonesha kuwa Tanzania imeendelea kuwa na urari chanya wa biashara kati yake na Sadc, ikimaanisha kuwa mauzo yake ni makubwa kuliko ununuzi.

Vilevile, Bohari Kuu ya Dawa (MSD) imeingia mkataba na Sadc wa kuuza na kusambaza dawa, vifaa tiba na vifaa vya maabara katika nchi zote 16 wanachama. Fursa hii inatoa mwanya pia wa kuvutia uwekezaji katika sekta hii jambo ambalo litachangia uendelezaji viwanda na teknolojia nchini katika tasnia ya dawa, vifaa tiba na maabara.
 
Imekaa vizuri. Na jumuia ya Africa mashariki nayo inamalengo hayohayo. Kuunda eneo huru la biashara, umoja wa forodha, sarafu moja nk. Sasa Tanzania itakuwa na sarafu ngapi kama kote mipango ikifanikiwa. Na ukuaji wetu wa biashara na SADC/nchi za SADC. Unatokana na juhudi za umoja huo au ni natural course ya mambo tu!
Maana kama ulivyosema, hata hatua moja ya mapengo yake haujapiga!
 
SADC leaders arrive in Malawi for summit​

Aug 16, 2021 Mwayi Mkandawire Politics 0

Suluhu-Hassa.jpg

Presidents of South Africa, Zimbabwe, Tanzania and Botswana have arrived in Malawi today for the Southern African Development Community (SADC) Summit.
President Cyril Ramaphosa of South Africa, Zimbabwe’s Emmerson Mnangagwa, Botswana’s Mokgweetsi Masisi and Samia Suluhu Hassan of Tanzania have all jetted in this afternoon. Vice President of Namibia Nangolo Mbumba is also in Malawi for the summit.
All the SADC leaders were welcomed by cabinet ministers at the Kamuzu International Airport in Lilongwe.
Mnangagwa.jpg
Mnangagwa
President of the Democratic Republic of Congo (DRC) Felix Tshisekedi is expected to arrive later today and will hold talks with President Lazarus Chakwera.
Mokgweetsi-Masisi.jpg
Mokgweetsi Masisi
Before that meeting, the Malawi leader will hold bilateral talks with President Andry Rajoelina of Madagascar.
Cyril-Ramaphosa.jpg
Ramaphosa (L)
This evening, Chakwera will host a private dinner at Kamuzu Palace for the Heads of State
The 41st Ordinary Southern Africa Development Community (SADC) Summit started on 9th August, 2021 at Bingu International Convention Centre (BICC) in Lilongwe and will end on 18th August, 2021.
It is being held under the theme “Bolstering Productive Capacities in the Face of COVID-19 Pandemic for Inclusive, Sustainable, Economic and Industrial Transformation”.
The theme seeks to accelerate the implementation of the SADC Regional Indicative Strategic Development Plan (RISDP) 2020–2030, in particular, the Industrialization and Market Integration pillar.
During the summit, Chakwera, will take over the chairpersonship of SADC from Filipe Jacinto Nyusi, President of the Republic of Mozambique who assumed the chairpersonship of SADC on 17th August, 2020.
The Summit will take stock of progress made in promoting and deepening Regional Integration in line with SADC’s aspirations as espoused in the RISDP 2020–2030 and Vision 2050, which envisage a peaceful, inclusive, competitive, middle- to high-income industrialized Region where all citizens enjoy sustainable economic well-being, justice, and freedom.

Source : SADC leaders arrive in Malawi for summit | Malawi 24 - Malawi news
 
Kwa hisani ya Gazeti la Mwananchi
.."Sadc ilianzishwa kupitia mkataba uliosainiwa Agosti 17, 1992 na wakuu wa nchi na serikali kumi na moja Tanzania ikiwamo na makao makuu yake yakiwa Gaborone, Botswana.

Tangu wakati huo, idadi ya nchi wanachama imeongezeka hadi kufikia 16 (Angola, Botswana, Comoro, DR-Congo, Eswatini, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Afrika Kusini,

Tanzania, Zambia na Zimbabwe) na kuunda soko la bidhaa na huduma la takribani watu 330 milioni.

Mtangamano wa nchi za Sadc

Chimbuko la Sadc ni mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na utawala wa mabavu wa makaburu nchini Afrika Kusini. Mapambano hayo yaliongozwa na Kundi la Nchi za Mstari wa Mbele (Frontline States) lililoanzishwa mwaka 1970, Tanzaniaikiwa taifa kiongozi wa kundi hilo. Pamoja na Tanzania, nchi nyingine zilikuwa Angola, Botswana, Lesotho, Msumbiji, Swaziland (Hivi sasa inaitwa Eswatini) na Zambia iliyojiunga miaka 10 baadaye.

Tanzania ilichukua jukumu la uongozi wa mapambano Kusini mwa Afrika kutokana na ukweli kwamba, nchi nyingi zilizounda Kundi la Nchi za Mstari wa Mbele, kijiografia, kiuchumi na kijeshi hazingeweza kuhimili vishindo vya serikali ya kibaguzi na mabavu ya Afrika Kusini bila ushiriki wa dhati na makini wa Tanzania.

Baadaye kundi hilo lilijizatiti zaidi kwa kuanzisha Jukwaa la Kuratibu harakati hizo (Sadc) ili kujenga uwezo wa kujitegemea kiuchumi na hatimaye kujigeuza tena kuwa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc). Kwa mantiki hiyo, Sadc ya sasa na siku zijazo dhima yake kuu ni maendeleo na ustawi wa jamii miongoni mwa nchi wanachama.

Kinadharia, Mtangamano wa Kikanda (Regional Integration) una hatua tano, ambazo ni eneo huru la biashara,umoja wa forodha, soko la pamoja, umoja wa kiuchumi na umoja wa kisiasa. Utekelezaji wa hatua hizo za mtangamano hutofautiana kutokana na hali ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ya nchi washiriki.
Aidha, baadhi ya jumuiya huinyambulisha hatua ya nne katika makundi madogo zaidi. Mathalani, umoja wa kifedha na sarafu moja au kuruka baadhi ya hatua kama ilivyofanyika katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iliyoanzia hatua ya umoja wa forodha.

Dhamira ya nchi za Sadc ilikuwa kuifikia hatua ya eneo huru la biashara ifikapo mwaka 2008, ikifuatiwa na umoja wa forodha(2010), kisha soko la pamoja (2015), umoja wa fedha (2016) na hatimaye sarafu moja mwaka 2018. Hali halisi ya utekelezaji inaonyesha kuwa Sadc iko hatua ya kwanza sawia na utekelezaji wa baadhi ya vipengele vya hatua ya pili. Kwa mfano, uondoaji wa viza kwa wasafiri wa nchi wanachama.

Faida za ushiriki wa Tanzania Sadc

Sera ya Taifa ya Biashara ya Tanzania inaainisha kuwa miongoni mwa nyenzo zake kuu za ukuzaji nauendelezaji mauzo nje ni mtangamano wa kikanda. Nyenzo zingine katika muktadha huu ni ushirikiano kati ya Tanzania na nchi nyingine mojamoja (bilateral co-operation) na Mikataba ya Shirika la Biashara Duniani (WTO Agreements).

Kimsingi, nyenzo hizo tatu, ikiwamo ile ya mtangamano wa kikanda, hujumuisha kuondolewa vikwazo vya kiforodha na visivyo vya kiforodha miongoni mwa nchi husika jambo ambalo huhamasisha uzalishaji, ufanyaji biashara na uwekezaji kwa jumla.Kwa kutambua dhana hiyo, takriban nchi zote za Sadc ziliondoleana ushuru wa forodha ilipofika mwaka 2012, isipokuwa kwa bidhaa chache zilizoonekana nyeti katika mapato ya kodi na ulinzi wa viwanda vichanga ambazo ushuru wa forodha uliondolewa taratibu hadi kufikia zero hivi sasa.

Sambamba na kuondoa vikwazo vya kiforodha miongoni mwa nchi wanachama, hatua zimechukuliwa pia kuondoa vikwazo visivyo vya kiforodha. Kwa mfano, taratibu za kiforodha zimerahisishwa ikiwamo uanzishwaji wa vituo vya forodha vya pamoja (one stop border posts) kama kile kilichopo Tunduma; mpakani mwa Tanzania na Zambia.

Hatua hiyo imeifaidisha Tanzania kibiashara. Mathalan, takwimu za sekretarieti ya Sadc zinaonyesha kuwa mauzo ya Tanzania katika Jumuiya yaliongezeka kwa zaidi ya maradufu, kutoka Dola za Marekani 432 milioni kwa mwaka 2007 hadi Dola 1,013 milioni mwaka 2016. Aidha, takwimu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinaonesha kuwa Tanzania imeendelea kuwa na urari chanya wa biashara kati yake na Sadc, ikimaanisha kuwa mauzo yake ni makubwa kuliko ununuzi.

Vilevile, Bohari Kuu ya Dawa (MSD) imeingia mkataba na Sadc wa kuuza na kusambaza dawa, vifaa tiba na vifaa vya maabara katika nchi zote 16 wanachama. Fursa hii inatoa mwanya pia wa kuvutia uwekezaji katika sekta hii jambo ambalo litachangia uendelezaji viwanda na teknolojia nchini katika tasnia ya dawa, vifaa tiba na maabara.
maneno mbona mengi hivi sio fix kwel.

Mimi kwakwel faida sijaziona, japokuwa ninajilazimisha kwel kuamini kama maneno yako.

Notisi hizo hata mimi nilizitumia kujibu maswal
nilipokuwa nasoma.

Ila uhalisia wake ni ngumu kwa raia wa kawaida kujua kutumia fursa ya angola au namibia ktk jumuiya yeye kujikwamua.

Wapo wtz juzijuzi hapo walifurumushwa nchini msumbiji na kuporwa kila walichochuma utafikir sio majiran

Wasauz weusi nao hawawataki waafrika wenzao wasogee kwao.
sasa hayo mashirikiano yatastawije.
 
Habari wakuu.

Naomba kujuzwa faida za SADC kwa nchi yetu.
Kuna Watu sijui huko Vyuo Vikuu mlifikaje na kwanini mlipata hata hivyo Vyeti vyenu vya Kitaaluma.

Umeshaambiwa SADC ni Southern African Development Community ( Jumuia ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika ) halafu na Ubongo wako wenye Utapiamlo unakuja tena Kuuliza Faida yake kwa Tanzania ni ipi.
 
Sawa SADC ni jumuia ya maendeleo, ina faida gani kwa nchi yetu? Kusema ni jumuia ya maendeleo hakuifanyi iwe na faida autimatically.
 
maneno mbona mengi hivi sio fix kwel.

Mimi kwakwel faida sijaziona, japokuwa ninajilazimisha kwel kuamini kama maneno yako.

Notisi hizo hata mimi nilizitumia kujibu maswal
nilipokuwa nasoma.

Ila uhalisia wake ni ngumu kwa raia wa kawaida kujua kutumia fursa ya angola au namibia ktk jumuiya yeye kujikwamua.

Wapo wtz juzijuzi hapo walifurumushwa nchini msumbiji na kuporwa kila walichochuma utafikir sio majiran

Wasauz weusi nao hawawataki waafrika wenzao wasogee kwao.
sasa hayo mashirikiano yatastawije.
Mi mwenyewe kama ni kupotezeana wakati tu. Miaka 30 ya SADC ni kitu gani mwananchi wa kawaida anaweza akasema ni faida ya SADC?
 
Halafu mapumbavu kama hili lipo hapa JF na uzi wa kimatako namna hii?

Jitu limesoma O'Level,hili swali lipo kwenye Civics na tulifanya na kila mtoto alipata A

Eti still huyu mpumbavu alielipiwa ada hajui faida ya regional groupings kama SADC?

Rudisha ada ya mzazi wako kabisa,

Mapumbavu kama haya inatakiwa muuawe kabisa yaani!

Keshokutwa utakuja hapa kutuomba kura tukuchague uwe Mbunge,kichwa maji kama wewe,like really?
Nadhani yeye ameuliza kujuzwa.. ni jukumu lako kama unajua unawesa kumjuza.. ila kusema auwawe.. hili siyo powa..

Tutauwa wangapi sasa mkuu?
 
Kuna Watu sijui huko Vyuo Vikuu mlifikaje na kwanini mlipata hata hivyo Vyeti vyenu vya Kitaaluma.

Umeshaambiwa SADC ni Southern African Development Community ( Jumuia ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika ) halafu na Ubongo wako wenye Utapiamlo unakuja tena Kuuliza Faida yake kwa Tanzania ni ipi.
Nadhani hapa tatioz la wengi siyo kujua kirefu au kujua maana ya kirefu au kujua malengo yake. Wengi tungependa kutajiwa, kwa mfano Tanzania kwa miaka imefaidia na ni vitu gani kwenye huo umoja. Kwa mafano hebu taja orodha ya mambo matano amabyo nchi yetu imeshafaidika nayo.
 
Kwa kweli kabisa Jumuia ya kikanda inayotufaa sisi ni EAC, hii ya SADC ni mwendelezo tu wa vugu vugu la ukombozi wa nchi za kiafrika ambapo manufaa tunayoyapata huko ni kidogo mno.
 
Back
Top Bottom