Sabondo kwa CHADEMA ni sawa na Karimjee kwa TANU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sabondo kwa CHADEMA ni sawa na Karimjee kwa TANU

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SubiriJibu, May 7, 2012.

 1. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,124
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Nipo hapa nasoma hotuba na article mbalimbali za Julius Nyerere zilizowekwa pamoja kama kitabu kikaitwa FRREDOM AND UNITY (ISBN: 9976400187).

  Kwenye pg. 119, Kuna hotuba yake aliyotoa July 29, 1961, yeye kama Waziri Mkuu wa Tanganyika anazindua Kivukoni College.

  Umuhimu wa hotuba ile si msingi wa post yangu leo. Umuhimu kwangu ni jinsi fund ya kukijenga chuo hicho ilivyopatikana.

  Kwamba ilitolewa rai wananchi wachangie sehemu mbalimbali za Tanganyika. Wako waliotoa senti moja, mayai, mahindi na mifugo kulinangana na uwezo wao, tena wakati ule. Lakini Karimjee na familia yake walitoa UK pounds 60,000.

  Huo ni mchango mmoja wa Karimjee ulioelezwa ndani ya kitabu hicho. Vilevile siku hizohizo kabla ya uhuru, Karimjee alijenga jengo lenye ukumbi mkubwa enzi zile. Ukumbi ambao ulitosha kubeba mihadhara mingi na akautoa kama zawadi kwa Municipal Council of D'Salaam.

  Serikali japo haikutumia jengo zima, iliamua kupata nafasi ya ukumbi tu tangu uhuru hadi October 1995, ikautumia ukumbi kwa Mikutano ya Bunge. Kwa heshima ya family ile jumba lile likaitwa na hata leo linaendelea kuita KARIMJEE HALL. Liko linatazamana na Hospital ya Ocean Road.


  Sasa, ametokea mtu anaitwa Mustafa Sabondo. Wapenzi wa CHADEMA si wenye kipato kikubwa kama ilivyokuwa wapenzi wa TANU. Yeye peke yake Sabondo ameshatoa zaidi ya mamia ya mamilioni ya shilingi kwa kuisaidia CHADEMA. Kajitolea uchimbaji wa visima. Nasikia atasaidia ujenzi wa ofisi mpya ya CHADEMA pale Mwenge.

  Nimetumia neno nasikia, kwani siko hapa kuwafundisha JF mchango wa Sabondo katika CHADEMA wakti mimi si mfuatiliaji sana hivyo mna haki ya kunifundisha matoleo ya Sabondo huko CHADEMA, baadhi yamejadiliwa humu.

  Lengo, langu ni kulinganisha, pia kuweka kumbukumbu sawa, hasa wale wenye kauli za kutaka Sabondo afanyiwe hiki au kile kama njia ya kumkwamisha asiisaidie CHADEMA. Mara, wengine nasikia wanashauri anyang'anywe kadi ya CCM na mengine tele myajuayo.

  Hivyo, wenye kutaka tusahahu, basi tukumbushe kwa kulinganisha kwa watu kama KARIMJEE na si kumsakama Sabondo kama wakoloni amabvyo wangemsakama KARIMJEE, kama ambavyo pia kuisakama JAMII FORUM ni kama wakoloni walivyosakama magazeti kama SAUTI YA TANU hadi Julius Nyerere akafunguliwa kesi ya kukashifu serikali ndani ya gazeti hilo (Toleo. No. 18, 1958).

  NAWATAKIA MJADALA MWEMA
   
 2. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mustafa Sabodo.........
   
 3. H

  HIPPO Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Napendekeza JINA LA OFFICE MPYA YA CDM MWENGE IPEWE JINA LA SEBODO COMPLEX
   
 4. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Taabu ya chama tawala ni kama mtoto mwenye roho mbaya! Kama Mjomba amezoea kuukununulia wewe viatu (as a political party) akininunulia mie mtoto mwenzako uniform (another political party) wewe inakukera nini?

  Inaonesha ubinafsi wa CCM; mwagombea hata msaada ambao haukuwa meant kwa ajili yenu?

  Shame on you CCM
   
 5. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Sabodo not sabondo
   
 6. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Ccm ni kama mgojwa wa ukimwi aliyekosa matumaini na akaamua maradhi yake aambukize na wengine ili wafe pamoja,makusudi ya Mungu ni kuiteketeza kama barafu juani.tena nawashangaa wanaodai ccm itakuwepo hadi 2015
   
 7. S

  Starn JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 400
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  KAma hujaelewa kilichoandikwa hapo juu ni bola ukae kimya.
   
 8. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  kumbe ofisi itajengwa mwenge? Kipande ipi hiyo na ukubwa upi?
   
 9. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  heri yake mstapha sabodo
   
Loading...