Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Mnamkumbuka Sabodo, yule kada wa CCM ambaye alikuwa anakilea CHADEMA kwa kukipa misaada kadhaa? Si mnamkumbuka? Kafanya mengi CHADEMA. Katoa fedha zaidi ya bilioni 2 kwa ajili ya kujenga makao makuu ya CHADEMA lakini zimetafunwa na Mbowe. Katoa fedha kwa ajili ya kuchimba visima vya maji zaidi ya 1000 kwenye kata ambazo CHADEMA walishinda uchaguzi wa 2010 lakini mpaka sasa hakuna hata kisima kimoja kimechimbwa. Katoa mamilioni ya fedha kwa ajili ya kugharamia harakati za kisiasa za CHADEMA lakini mpaka sasa haijulikani fedha hizo zilipo.
Ndoa ya Sabodo na CHADEMA ilivunjika rasmi mara baada ya chama hicho kumpokea fisadi Lowasa na kumteua kuwa mgombea Urais. Imani ya Sabodo ilikuwa kwa Dr Slaa na aliahidi kuwamwagia mabilioni ya pesa kama wangesimamisha mtu mwadilifu kugombea urais.
Baada ya Sabodo kumwaga mboga, CHADEMA kwa maelekezo ya Edward Lowasa imeanza mkakati wa kumshughulikia mwanasiasa huyo kupitia miradi yake ya biashara ambayo ipo Kinondoni, Temeke na Ilala ambapo kwa kiasi kikubwa ukiondoa Ilala, manispaa hizo zinaongozwa na CHADEMA. Taarifa zilizopo ni kwamba, Lowasa ametoa maagizo kwa Manispaa zinazoongozwa na CHADEMA kuhakikisha kuwa wanamkaba koo Sabodo na ikiwezekana wahakikishe anafilisika kabisa.
Katika kuanza kutegeleza mkakati huo, manispaa ya Kinondoni imeanza kumuweka uchi Sabodo ambapo kupitia orodha ya wadaiwa wa Manispaa hiyo, SABODO ametajwa kudaiwa shilingi 3,920,400/=. Kwamba, Sabodo ameshindwa kulipia matangazo ya biashara zake kwenye Manispaa hiyo na hivyo manispaa imelazimika kulianika jina lake pamoja na makampuni mengine ili kumlazimisha alipe.
Hata hivyo, Sabodo alipopewa taarifa juu ya Kampuni yake kudaiwa kiasi hicho, alisikika akisema kuwa walichofanya CHADEMA ni udhalilishaji. Amewasaidia mabilioni ya pesa sasa walishindwa nini kumuona na kumjulisha kuwa kampuni yake inadaiwa kiasi hicho? Anasema kuwa kama wangemuona na kueleza tatizo hilo, angewalipa hata kodi ya miaka 5 na wasingefikia hatua ya kudhalilishana. Amewashauri CHADEMA kuwa makini na maamuzi yao ya pupa.
Kupata majina ya wadaiwa wote mnaweza kufuata linki hii iliyopo kwenye mtandao wa CHADEMA BLOG
Chadema Blog