Sabodo atunukiwa Medali na CHADEMA: Aahidi kuchangia tena mil. 150

Xuma

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
683
225
Chama cha demokrasia na maendeleo kimetunuku Medali ya heshima na ujasili Mzee sabodo kwa kukichangia chama hicho waziwazi.

Pia ameahidi kukichangia tena chama hicho Milioni 150.

ITV.
 

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,230
2,000
Katika taarifa ya habari ya saa mbili jioni hiikupitia TBC1 nimeona viongozi wa CHADEMA wakimtunuku nishani Mzee Sabondo alie kichangia chama mil 200 kipindi cha kampeni na amea ahidi kuchangia mil 100 kwaajiri ya ujenzi wa chuo cha viongozi wa CHADEMA...Mwenye taarifa zaidi juu ya chuo hicho atujuze tafadhali
 

NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,668
0
Chama cha demokrasia na maendeleo kimetunuku Medali ya heshima na ujasili Mzee sabodo kwa kukichangia chama hicho waziwazi.

Pia ameahidi kukichangia tena chama hicho Milioni 150.

ITV.


Nilichopenda ni comment moja ya Dr. Slaa ambayo nadhani haistahili kupita bila kujadiliwa. Dr amesema Sabodo ni mfano wa kuigwa kwani anajitokeza wazi kuchangia huku akikiri wazi kuwa ni mwana-CCM na hivyo kuwa tofauti na wengine ambao wanachangia lakini hawajitokezi wazi.

Hii inamaanisha kuwa wako watu wengine ndani ya CCM wanaochnagia CHADEMA lakini hawajitokezi wazi. Na kama kweli wapo basi mimi nadhani ni vema wakajitokeza kwani huenda mchango wao wakijitokeza utakuwa mkubwa tofauti na kama hawatajotokeza
 

nyasatu

Member
May 15, 2009
72
0
Taratibu Chadema inaanza kutengeneza Mafisadi
mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu...kweli ww ni mwana fisadi damu mana kuona mtu kachangia tu ukahisi ni kama mfanyavyo uko kwenu,kwanza nachefuka ona iyo rangi ya profile yako na iyo nyundo na yako ambayo soon itakumaliza mwenyewe.....ila kwa leo nmekusamehe sio kosa lako
 

Shinto

JF-Expert Member
Dec 6, 2010
1,781
0
Ingekuwa huyu mwana CCM damu kawafadhili CUF hapa tungesema CCM A wamewahonga CCM B hivyo si wapinzani wa kweli. Lakini hapa mwana CCM anawapa CDM mnachekelea! EPITOME OF HYPOCRISY!
 

Xuma

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
683
225
Taratibu Chadema inaanza kutengeneza Mafisadi

Mafisadi ni kwenu huko mbona wanaochangiaga huko watuwasikii! kwa nini wanakosa ujasiri au kwa nini chama chenu (CCM) hakiwasemi/hakiwaweki hadharani??

Si mnajificha kwa sababu nyie ni mafisadi......................................
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,931
2,000
Taratibu Chadema inaanza kutengeneza Mafisadi
Atoaye kwa uwazi na Kupongezwa hadharani hawezi kutengenezwa kuwa fisadi. Sio wale wanaokwapua 40 bil na kuipa Chama twawala 10 bil kisha wanapewa uwezo hata wa kuhakikisha wanamweka Spika wa Bunge au waziri wamtakaye wao.
 

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,016
2,000
Lakini asikia kuwa Sabodo ni mfanyabisha mkubwa ambaye hakwepi kodi.

Isiwe ikawa zinatoka mkono wa kulia zinapelekwa mkono wa kushoto

Chadema jiridhishe na wat wanaochangia ni SAFIIIII?
 

zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,062
0
Wanazi wa Chadema humuhumu JF washa msema sana huyo jamaa kuwa ni fisadi, na posts zipo, labda mamods wazibandue kwa kuona haya.

Leo kimekuwaje Fisadi kutunukiwa?

Haya ndio kama ya Mtikila na RA, alipojidai kumsema RA, alipoonyeshwa ushahidi kuwa na yeye huwa anavuta huko huko, akaufyata.

Sasa tunaona jamaa wanavyoufyata, waswahili walinena "pesa mwana haramu".
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom