Kuna watu bado wanatetea gazet la uhuru , liliweka kichwa cha taarifa hv, sabodo hatawapa tena chadema msaada ila ataenda kuwekeza dodoma $5b [emoji849][emoji849]na kuwaita wawekaZaji wengine.
Sasa mm nashindwa kuelewa hivi hata mzee mwanakijiji kichwani hamna kitu siku hizi maana alielezea hivi kukaa kote nje alikuwa hajui ukubwa wa 5 use billion ninyingi mno jamani Mzee MM udini utamua
MFANYABIASHARA maarufu, Mustapha Jaffer Sabodo ametangaza kutoa dola za Marekani bilioni 5 (Sh trilioni 10) kwa ajili ya kuwekeza mkoani Dodoma, ikiwa ni njia ya kumuunga mkono Rais John Magufuli kuhamisha makao makuu ya serikali kwenda mkoani humo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Sabodo alisema atawekeza kiasi hicho cha fedha, iwapo serikali yote itahamia mkoani humo, itakuwa ametimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambaye alitamani kuona mkoa huo unakuwa makao makuu ya nchi.
Alisema alichofanya Rais Magufuli, kimewashinda marais wengine waliomtangulia, hivyo yeye kama mfanyabiashara na mtu mwenye mapenzi makubwa kwa nchi yake, lazima aunge mkono hatua hiyo ya Serikali kuhamia Dodoma ambayo aliita ‘Azimio la Dodoma’.
“Niliposikia anatangaza kwenye televisheni ya taifa kwamba Serikali itahamia Dodoma, ilikuwa mara yangu ya kwanza baada ya miaka mingi kupita, nilitabasamu moyoni, jambo ambalo lilinitokea miaka 10 ya kwanza ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere. “Leo nimesikia kutoka kwako nimeona ile roho ya Nyerere imezaliwa tena. “Kwa hiyo natangaza kuunga mkono Azimo la Dodoma kwa kuwekeza dola za Marekani bilioni 5, ambazo zitatumika kwa ajili ya uwekezaji mkubwa katika huduma mbalimbali za jamii mkoani humo,” alisema Sabodo.
Sabodo alisema atatoa fedha hizo ili zitumike kuwekeza kwenye viwanda kama vya mvinyo, viwanda vya kusindika mihogo na viwanda vingine ambavyo vitahitajika katika mkoa huo.
Alisema kuwepo kwa huduma hizo mkoani Dodoma, kutasaidia kuufanya mji huo kukidhi matakwa ya watumishi wa umma watakaohamia huko.
Mfanyabiashara huyo aliongeza kuwa atafanya uwekezaji mkubwa huo kwa sababu lengo lake ni kuona mji wa Dodoma, unaungana na miji ya jirani kama Mpwapwa, Kondoa na Manyoni ili kutoa fursa ya kupanua huduma mbalimbali katika makao makuu hayo ya nchi.
Sabodo alisema kwamba juhudi zake za kuwekeza katika huduma za jamii kama shule, pia ataziendeleza katika mkoa huo kwa kuhakikisha kwamba zinajengwa shule kadhaa za kisasa, ambazo zitamudu mahitaji ya watu wa eneo hilo.
Kwa upande wa huduma ya afya, Sabodo alisema atatumia umaarufu wake kuwashawishi wamiliki wa Hospitali ya kimataifa ya Apollo ya India ili waje nchini wakashirikiane naye kujenga hospitali ya kisasa, ambayo itakuwa inatoa huduma za kisasa mkoani humo.
“Mnaifahamu hospitali ya Apollo ni wawekezaji wakubwa katika huduma za afya, kwa kusukumwa na hatua hii ya Rais nitaongea nao tushirikiane katika kujenga huduma za jamii katika mji huo,” alisema Sabodo.
Pia alisema atawashawishi wawekezaji wengine kutoka nchi za India, Singapore na kwingineko kuja kuwekeza katika mji huo wa Dodoma katika sekta ya viwanda, kuhakikisha kwamba azma ya Rais Magufuli ya kujenga uchumi wa viwanda inatimia.
Sabodo ambaye alisema wazi kuwa utendaji wa Rais Magufuli, umemvutia kutokana na hatua yake ya kupiga vita rushwa, alitangaza kuwa kuanzia sasa hatatoa tena msaada kwa vyama vya upinzani kama ambavyo amefanya miaka ya nyuma kama njia ya kuimarisha demokrasia nchini.
“Huko nyuma nilikuwa nawapa Chadema fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kuimarisha demokrasia, sasa natangaza tena kwamba sitawapa tena fedha, niwape za nini wakati Rais aliyeko madarakani anafanya kazi ambayo ndio nilikuwa naipigania? alihoji Sabodo.
Sabodo ni mfanyabiashara wa kitanzania mwenye asili ya Kihindi ambaye alizaliwa mkoani Lindi. Katika maisha yake amekuwa anafanya biashara katika nchi za Kenya, Ufaransa, India, Sudan na Zimbabwe.
Pamoja na biashara zake, Sabodo amekuwa anajihusisha kuchangia katika miradi ya maendeleo ya huduma za jamii, uimarishaji wa demokrasia nchini na pia alishiriki kutunisha mfuko wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere kwa kuanzisha bahati nasibu.
Hilo nalo limo. Lazima angefuatiliwa vyanzo vyake vya kipato, ukizingatia kwamba ana historia ya kuwapa pes wapinzani (kitu ambacho chama twawala hakipendi kusikia)
Akizungumza jana katika mahojiano maalumu nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam, Sabodo alisema hana fedha za kutoa kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa miundombinu mkoni Dodoma.
Dar es Salaam,
Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo ameitaka Serikali kuwachangisha wananchi ili kupata fedha za kuhamishia makao makuu ya Serikali mjini Dodoma.
Akizungumza jana katika mahojiano maalumu nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam, Sabodo alisema hana fedha za kutoa kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa miundombinu mkoni Dodoma.
“Nataka niweke suala hili vizuri, sina fedha za aina hiyo popote pale. Ninazo mali kadhaa lakini sina fedha zote hizo. Watu wengi wanakuja kwangu, wanakuja hapa, nipe pesa, nipe pesa, hakuna pesa hapa,” alisema Sabodo na kuongeza:
“Mimi ni kama kichocheo tu, kama ndimu unatia kwenye soda. Nilichosema ni kutafuta juhudi kutoka kwa kampuni za India na Singapore kufanikisha ujenzi wa makao makuu ya Dodoma, lakini sina kiasi chote hicho cha fedha,” alisema.
Hivi, unawezaje kutangaza uhamisho wa wizara, serikali na hata kuwatishia wengine watakaobakia Dar kwamba watakuwa wamefukuzisha kazi, na hata ukasema utauza wizara ya takwimu, kumbe hata hujui fedha za kutimiza hiyo mambo zinatoka wapi?
Ninadhani kuna watu wanahobby ya kutishia watu au la wanafurahia watu wanapokuwa katika hali mbaya, hekaheka na kusoneneka.
Ninaanza kupata harufu ya Narcissistic Personality Disorder!.
Wataalamu wa magonjwa ya viungo vya kichwani, tunaomba mtusaidie. Inawezekana kumbe tunasumbuliwa na maradhi yasiyojulikana hapa.
tatizo ni la waandishi wetu wengi ni ****** waliofeli ndio wabobezi wa hii taaluma .kwa akili ya kawaida hii habari ilikuwa ya kinadharia zaidi,nilishtuka nilipo isoma hii habari...
Ukilaza sio wa waandishi tu hata wapuuzi waliojipa kazi yakutangaza ujinga unaosifia Watawala....nasubiri aliejitolea kutangaza kila kitu cha Serikali hata kama cha kijinga....aje humu na Gazeti lake la Juzi
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.