Sabodo Akanusha Kuahidi Kuwekeza $5B Dodoma

Bukanga

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
2,857
1,936
Kwa ufupi

Akizungumza jana katika mahojiano maalumu nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam, Sabodo alisema hana fedha za kutoa kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa miundombinu mkoni Dodoma.

Dar es Salaam,
Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo ameitaka Serikali kuwachangisha wananchi ili kupata fedha za kuhamishia makao makuu ya Serikali mjini Dodoma.

Akizungumza jana katika mahojiano maalumu nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam, Sabodo alisema hana fedha za kutoa kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa miundombinu mkoni Dodoma.

“Nataka niweke suala hili vizuri, sina fedha za aina hiyo popote pale. Ninazo mali kadhaa lakini sina fedha zote hizo. Watu wengi wanakuja kwangu, wanakuja hapa, nipe pesa, nipe pesa, hakuna pesa hapa,” alisema Sabodo na kuongeza:

“Mimi ni kama kichocheo tu, kama ndimu unatia kwenye soda. Nilichosema ni kutafuta juhudi kutoka kwa kampuni za India na Singapore kufanikisha ujenzi wa makao makuu ya Dodoma, lakini sina kiasi chote hicho cha fedha,” alisema.

Chanzo: Mwananchi

MsemajiUkweli Mzee Mwanakijiji Pasco joka kuu The Boss Mag3
 

Attachments

  • sabodo.jpg
    sabodo.jpg
    47.5 KB · Views: 110
Nilijua hawezi na mkuu hela hzi za misaada misaada ya kibagacholi huwa hapendi!!!
 
tatizo ni la waandishi wetu wengi ni vilaza waliofeli ndio wabobezi wa hii taaluma .kwa akili ya kawaida hii habari ilikuwa ya kinadharia zaidi,nilishtuka nilipo isoma hii habari...
 
Dola b5 waandishi mliichukulia powa? Hiyo ni hela haswa Sabodo huyu angeipata wapi?

Ila kuna mwandishi mmoja aliliweka sawa kwamba sabodo atashawishi marafiki zake wa Italy, Egypt, India n.k. ili wawekeze Dodoma ambapo wakikubali investment zao itafikia hizi $b5
 
Lugha ya watu ngumu sana. Mleta mada hujaelewa kilichoandikwa ndio mana umekurupuka kuja na taarifa ya upotoshaji
 
Sabodo anasema atawaleta wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania hususan Dodoma yeye akiwemo. Na taarifa ya awali ilieleza hivyo. Sasa wewe kwa kuwa hujui unakuja na hisia binafsi unaandika uongo wenzako wanakuunga mkono
 
Nilishambuliwa sana, baada ya kusema sabodo hana iyo pesa!
Mkuu katika ile taarifa alisema yeye na wawekezaji wenzake wataenda kuwekeza Dodoma na hii amesema atawaleta wawekezaji kuwekeza Tanzania hususan Dodoma. Hakuna tofauti ila mleta mada hajaelewa kiingreza
 
yaani serikali na ubalozi wetu nchini India hauwezi kushawishi wawekezaji mpaka wasaidiwe na Sabodo? Na kama Sabodo ana uwezo huo na ni mzalendo wa kweli wa nchi yetu kwa nini miaka yote hiyo asilete hao wawekezaji? yeye ni nani mpaka aaminiwe na wawekezaji wa nje kuliko serikali?
 
Back
Top Bottom